Habari wadau wa JF siasa.
Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?
Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Pata picha tu ndio kwanzaaa miezi miwili tu imepita tangu muhula wa pili wa awamu ya tano uanze tayari tushaanza kupoteana sipati picha mwaka mmoja ujao tutakuwaje ase!!!
Sikwambii hiyo mitano ikiisha hali itakuwaje maana mpaka sasa tumepoteana vibaya mno, haieleweki tunaelekea wapi [emoji3062][emoji3062][emoji3062]
Kuna wachapa viboko, wengine hawataki barakoa kwenye mikutano mara wengine wanazuia mazishi kwanza mpaka uchunguzi ijulikane kauwawa au kafa tu kawaida chini ya mikono yao [emoji3062][emoji3062][emoji3062]
Hatujakaa vizuri wengine wametangaza tutakagulia hapahapa wakaguzi wahuko mkataba umekwisha sasa wakati unajiuliza kulikoni wakati unajiuliza hilo ghafla wengine wanazuka tu ooh mawakala wa shopping centers jamani kweli tutafika hivi [emoji3062][emoji3062][emoji3062]
Mfano mpaka sasa haileweki Corona ipo au haipo licha ya kuwa tuna wataalamu wa afya na takwimu ambao kiusalama wanapaswa kujua tishio la ugonjwa huu nchini lipo au hapana
Tunatangaziwa aina mpya ya maambukizi ya Nimonia lakini mpaka sasa hatujaelezwa nimonia hiyo ni mpya au ni kama ile ya zamani
Hatujakaa vizuri mwingine kaibuka na jiko la mkaa anachemsha mchaichai anakwambia Season 3 ya kujifukiza sasa hatuelewi yaani ni vuluvulu
Mara ooh madaktari sijui wanasomeshwa na serekali kwa hiyo hawatakiwi kwenda kule hali ya kuwa wengine wamejaa kibao mtaani sasa na kule nako wakiogopa kuwachkuwa waliosomeshwa na serikali itakuwaje
Wakati huohuo popote watakakapokuwa iwe seeikalini au kule still bado HELSB inawahusu sasa sijui ipoje yaani kila kukicha tunapoteana
Dereva mbona kama kaacha njia gari lina halieleweki linaelekea wapi wazi kabisa tunaona usukani unamshinda tutafika salama kweli huko unapopaulizia maana bado parefu 2022 tutatoboa ???