Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Atagombana na mrithi wake kwa kuwa hana kifua cha kuvumilia vijembe vya Wapambe wa Rais ajae.

Cyprian Musiba wa Awamu ya 6 atakuwa anam provoke nae 'atajaaa'.

JK alitumia busara na subira ya hali ya juu sana kukwepa kuchonganishwa na Mrithi wake, sijui kama Yeye atakuwa na hicho kifua kama cha Jk
 
Sidhani Kama Kuna ufisadi sikuizi
Utausikia wapi bila kuibuliwa kama zamani, taasisi zote zinazo under perform zianhamishiwa chini ya ofisi ya raisi ambayo haiwi audited na CAG, ukitaka kujua kuna ufisadi hata wastaafu wanahangaika na pension zzao kuliko kipindi cha kikwete wengine washakata tamaa kabisa.
 
Atagombana na mrithi wake kwa kuwa hana kifua cha kuvumilia vijenbe vya Wapambe wa Rais ajae....
Kama itatokea bahati nzuri awe na "mrithi" kama unavyopendekeza (mimi siamini kwamba ataondoka, kwa hiyo hatakuwa na mrithi akiwa hai)

Lakini kama kweli itatokea kama hivyo, bahati nzuri ya mrithi wake ni kuwa atakayekuwa amemrithi hatakuwa tena na mabunduki na mabomu yanayompa kiburi sasa. Hapo atakuwa mpole sana kama alivyokuwa wakati akiwa waziri chini ya Pinda na Kikwete.

Hata watetezi kama alionao Kikwete, huyu atakuwa hana wakati huo.
 
Ataondoka Sheikh wangu usiwe na hofu,

dalili zote za kubaki madarakani hazipo na ndio sababu hata vurugu za ndani ya Chama zimeisha

Musiba, Nkamia na Mh.Kessy wameondolewa kwny ramani strategically maana hawa walikuwa kama petrol kwny moto

Wazee wamerudisha visu kwny Ala!
Kama itatokea bahati nzuri awe na "mrithi" kama unavyopendekeza (mimi siamini kwamba ataondoka, kwa hiyo hatakuwa na mrithi akiwa hai)

Lakini kama kweli itatokea kama hivyo, bahati nzuri ya mrithi wake ni kuwa atakayekuwa amemrithi hatakuwa tena na mabunduki na mabomu yanayompa kiburi sasa.
Hapo atakuwa mpole sana kama alivyokuwa wakati akiwa waziri chini ya Pinda na Kikwete.
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?
Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Kwani ana mpango wa kutoka lini?
 
Ukiijua elimu ya namba na cords zake huwezi kuumiza saana kichwa.

Kwa ufupi baada ya namba 5 kutoka nchi haitatengemaa na kupata uchumi imara, hadi atakapo ingia Rais wa 8.
Rais wa 6 anaweza kua rais asiejiamini kuliko ote,na atakua mwenye hasira na kukulupuka kuliko ote.kutokana na kutojiamini kwake atayumbishwa sana.

Ila atakuza elimu, sanaa, biashara, mambo ya watoto.nk.

Mbaya zaidi yakitokea maladh kama haya ya sasa atashindwa kuyadhibiti.

Ajira, watu wajiajili wenyewe na wachapekaz wenyewe tena kwa bidii hasa.

Maana tusipoangalia hali itakua ngumu mala 2 ya sasa.
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?
Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Maisha yataendelea tu kwani kabla hajakuwepo watu hawakuishi?? Maisha huwa yanaendelea tu usihofu
 
Pamoja na kuwa tunamlaumu kwa maneno kibao ila JPM akistaafu nchi inarudi kuwa utopolo, nchi itabaki kuliwa na wajanja kuliko saivi, itabaki kuwa nchi ya connection kwa asilimia kubwa, watoa huduma wataanza kuwa viburi, uonevu utakuwa haukatazwi, maskini watadhurumiwa hali zao ikiwemo mashamba n.k.

Wajanja wataweka maafisa wa TRA kwenye payroll zao hivyo hawatalipa kodi tena kama ilivyo sasa.

Kuna wakati inauma sana lakini katiba lazima iheshimiwe na watu wote.
 
Ndio maana mnaambiwa jengeni mifumo badala ya personalities. Binadamu tunapita; nchi na mifumo yake hudumu.

Kwenye hili CCM mmekwama completely toka enzi za Mwalimu. Anyway, sio kwa bahati mbaya ila makusudi mazima ili muendelee kutawala kijanja janja. Ila mwisho upo.
Yanayoendelea middle east kwa Sasa ndiyo yatakuja kutoka Africa 20 years to come. It will get even worse than this. Kama unaweza kuwatafutia makazi wanao nje ya hili bara this is the right time. Mark my words!!
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?
Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Pata picha tu ndio kwanzaaa miezi miwili tu imepita tangu muhula wa pili wa awamu ya tano uanze tayari tushaanza kupoteana sipati picha mwaka mmoja ujao tutakuwaje ase!!!

Sikwambii hiyo mitano ikiisha hali itakuwaje maana mpaka sasa tumepoteana vibaya mno, haieleweki tunaelekea wapi [emoji3062][emoji3062][emoji3062]

Kuna wachapa viboko, wengine hawataki barakoa kwenye mikutano mara wengine wanazuia mazishi kwanza mpaka uchunguzi ijulikane kauwawa au kafa tu kawaida chini ya mikono yao [emoji3062][emoji3062][emoji3062]

Hatujakaa vizuri wengine wametangaza tutakagulia hapahapa wakaguzi wahuko mkataba umekwisha sasa wakati unajiuliza kulikoni wakati unajiuliza hilo ghafla wengine wanazuka tu ooh mawakala wa shopping centers jamani kweli tutafika hivi [emoji3062][emoji3062][emoji3062]

Mfano mpaka sasa haileweki Corona ipo au haipo licha ya kuwa tuna wataalamu wa afya na takwimu ambao kiusalama wanapaswa kujua tishio la ugonjwa huu nchini lipo au hapana

Tunatangaziwa aina mpya ya maambukizi ya Nimonia lakini mpaka sasa hatujaelezwa nimonia hiyo ni mpya au ni kama ile ya zamani

Hatujakaa vizuri mwingine kaibuka na jiko la mkaa anachemsha mchaichai anakwambia Season 3 ya kujifukiza sasa hatuelewi yaani ni vuluvulu

Mara ooh madaktari sijui wanasomeshwa na serekali kwa hiyo hawatakiwi kwenda kule hali ya kuwa wengine wamejaa kibao mtaani sasa na kule nako wakiogopa kuwachkuwa waliosomeshwa na serikali itakuwaje

Wakati huohuo popote watakakapokuwa iwe seeikalini au kule still bado HELSB inawahusu sasa sijui ipoje yaani kila kukicha tunapoteana

Dereva mbona kama kaacha njia gari lina halieleweki linaelekea wapi wazi kabisa tunaona usukani unamshinda tutafika salama kweli huko unapopaulizia maana bado parefu 2022 tutatoboa ???
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?
Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?

Amani na upendo wa kweli utarejea na sio hofu na nidhamu za kinafiki. Utawala wa sheria utarejea na sio sheria zinazomfurahisha rais. Ccm itarejea kuwa chama cha siasa, na sio kikundi cha dola kilichojificha kwenye koti la siasa kupitia madaraka ya urais. Uhuru wa vyombo vya habari utarejea na serikali itarudi kuwa ya uwazi. Bunge latarudi kuwa Muhimili unaojitegea na sio hekalu la kumsifia rais na kutii kila atakacho. Mahakama itarejea na kutekeleza wajibu wake wa kutoa haki, na sio kuwa taasisi ya kukomoa wote wasiomsujudia rais. chaguzi za nchi zitarudisha heshima yake, na sio kama sasa kuwa maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Back
Top Bottom