hadi leo hii Februari 3 2021 bado sijaona mtanzania ambaye ana weza kuvaa viatu vya JPM, bado sijaona mtu jasiri na mchapakazi mfuatiliaji kila kitu bila woga kama yeye. samahani kwa kusema kama nitamkwaza yeyote kwa kusema bado walio wengi wana kosa sifa ya ujasiri, ushupavu na uthubutu, kwani mafanikio makubwa ya Rais JPM yamechagizwa sana na tabia yake binafsi ya kujiamini bila kukubali kuyumba au kuyumbishwa, mzalendo imara asiye mnafiki,mwenye kujali na kuwazingatia watu wa chini zaidi kuliko walio juu, asiye kubali kuletewa taarifa tu bila kujiridhisha, asiye endekeza majungu wala fitina, kwa kifupi kiti cha Urais kakitendea haki,
pamoja na "miluzi" mingi ya kumtoa nje ya "reli" lkn bado amebaki kwenye "reli".
hajawahi kuchezeshwa "ngoma" asiye ijua.
tunamuombea Mungu amtunze akamilishe kipindi chake salama salimini,
Sent using
Jamii Forums mobile app