Nini kitatokea endapo litachimbwa shimo kubwa kutokea upande wa pili wa dunia?

Nini kitatokea endapo litachimbwa shimo kubwa kutokea upande wa pili wa dunia?

fungi6

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2017
Posts
287
Reaction score
266
Tukiachana na layer na sifa zake kwa kuongezeka joto kadri mtu unavyo zidi teremka chini ya ardhi

Layer zenyewe zikiwa zinajulikana kama,
-mantle(2)
-crust(1)
-core(3)

Je unaisi itakuaje mtu akichimba shimo kutoka pande moja ya dunia shimo litokee upande wapili je akiruka kudumbukia kutoka point A atatokaje kwenye point B???
main-qimg-2e745f08d3dde3cf0d2a9708443be873.png

Jje unajua kulingana na iyo picha apo juu mtu ataweza kutoka
>new york kutokea london ndani ya dk 42
>tokyo to Montreal ndani ya dk 42
>dublin kwenda Sydney dk 42
Nb: japo nchi nyingi zitatokea baarini

Wazungu wenzetu wameanza iki kitu wakitaka toboa izo sehemu sizani kama itawezekana ila naisi akiikomalia i kazi ktu kama Elon Musk basi litaeza wezekana

Ila mimi binafsi bado siamini kama dunia ni mduara embu waza ilo shimo ukiruka unatokeaje upande wa pili?

Je atatokea kama eruption akitupwa juu mbali angani afu arudi tena ardini au?

images (1).jpeg
 
Kwa ajili ya mjadala, kama ulivyosema, tufanye (assume) katikati ya dunia hakuna moto na pia hakuna Centre of gravitation yaani hakuna nguvu ya uvutano.

Ukitoboa dunia tundu la moja kwa moja (through hole) hiyo ni sawa uchukue Chungwa na utoboe tundu kuanzia kwenye ncha moja hadi kutokea kwenye ncha nyingi ya upande wa pili, ni kitu hicho hicho kitakuwa katika dunia kama utatoboa tundu na kama utatumbukia katika hilo tundu kwa kutanguliza miguu utatokeza upande wa pili kwa miguu kutangulia kutokeza.

Kama utatoboa dunia katika hali ilivyokuwa sasa ukibahatika kufika kwenye Core wewe ni mwanaume, hilo Joto utakimbia mwenyewe na kuacha hilo shimo likitoa moshi na moto kama chimney.

Kama ukiondoa Moto katika hiyo Core na kuacha nguvu ya uvutano pekee na mtu ukatumbukia ndani ya hilo shimo ulilochimba, basi kamwe huwezi huwezi kutokeza upande wa pili wa dunia sababu, utakapojiachia kutumbukia nguvu ya uvutano itakuvuta na kadiri unapokaribia Core hiyo nguvu inazidi na hatimaye utapitiliza kwenye Core moja kwa moja kuelekea kutokea upande wa pili lakini ukikaribia kutokeza upande wa pili utavuta tena na uvutano kurudi chini na mchezo huo utaendelea hivyohivyo na hiyo hali inaitwa; Simple harmonic motion (SHM) na itasimama kutokana na "damping effect" kama jinsi bembea inaposimama baada ya kusukumwa to and fro.
 
Kwa ajili ya mjadala, kama ulivyosema, tufanye (assume) katikati ya dunia hakuna moto na pia hakuna Centre of gravitation yaani hakuna nguvu ya uvutano.

Ukitoboa dunia tundu la moja kwa moja (through hole) hiyo ni sawa uchukue Chungwa na utoboe tundu kuanzia kwenye ncha moja hadi kutokea kwenye ncha nyingi ya upande wa pili, ni kitu hicho hicho kitakuwa katika dunia kama utatoboa tundu na kama utatumbukia katika hilo tundu kwa kutanguliza miguu utatokeza upande wa pili kwa miguu kutangulia kutokeza...
Wooow
 
Chini ya dunia kuna layers nyingi na volcano ambazo zina pressure nyingi. Kuna gesi ina pressure na mafuta.

Unayoyasema yanawezekana ila ni deadly na costy.

Maana yake ni worthless to do it
 
Kwaiyo mkuu apa nitakua nadumbukia nakurudi inakua endless progress
 
Chini ya dunia kuna layers nyingi na volcano ambazo zina pressure nyingi. Kuna gesi ina pressure na mafuta.

Unayoyasema yanawezekana ila ni deadly na costy.

Maana yake ni worthless to do it
Walijaribu russia kitambo ila wakakimbia baada ya vyombo vyao kumumunyuka ndo maana nikasema ukiondoa uwezo wa izo layer mh.
 
Hilo haliwezekani, ilikuwa rahisi zaidi kuichunguza Atmosphere na layers zake kuliko sehemu ya ndani ya dunia.

Kuanzia kwenye mesosphere all the way to barysphere(core) imebase kwenye Assumptions

Hata GIS can not give exact n correct records at 100% to be trusted.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo mkuu apa nitakua nadumbukia nakurudi inakua endless progress

Kulingana na sheria ya kwanza ya mwendo ya Newton Isaac (the Newton 1st law of motion), kama hakutakuwepo na ukinzani wa nguvu yoyote ya nje mfano hewa au kitu chochote basi safari ya nenda- rudi (SHM) kama bembea itaendelea tu hadi Mungu atakapo simamisha systems za dunia (kwa wale tunaoamini nguvu za Mungu), kuendelea huko ni sawa na mfano wa sayari kuendelea kulizunguka jua.

Katika mfano halisi (in real practical) jambo la kuendelea kutembea nenda- rudi (to and fro) "nadhani" halitawezekana kutokana na ukinzani wa hewa itakayo kuwemo ndani ya hilo shimo na utofauti wa densities/mass za materials zinazojenga dunia na hivyo kufanya kuwe na utofauti wa nguvu za uvutano "along the bore", kifupi ni kwamba mwendo wa nenda- rudi hauwezi kudumu katika hali halisi ya hayo mazingira niliyoyataja.

Sasa kama hali hiyo ya kutoendelea kwa mwendo wa nenda-rudi nini kitatokea kwa mtu au kitu kilichotumbukizwa humo shimoni?--- kulingana na sheria za kifizikia mtu au kitu hicho kitabaki katika Core ya dunia hakiwezi kutoka katika upande wowote wa hilo shimo.

Jambo jingine la kutafakari kiuhalisia ni hili; katika core hiyo ni sehemu yenye pressure kubwa sana kutoka katika kila upande wa uso wa dunia na hivyo tundu lolote likipitia hapo kuna nafasi kubwa ya tundu hilo ku "Collapse" katika sehemu hiyo.
 
Hilo haliwezekani, ilikuwa rahisi zaidi kuichunguza Atmosphere na layers zake kuliko sehemu ya ndani ya dunia.

Kuanzia kwenye mesosphere all the way to barysphere(core) imebase kwenye Assumptions

Hata GIS can not give exact n correct records at 100% to be trusted.

Sent using Jamii Forums mobile app
But akuna kisicho shindikana duniani balikimoja tu kumpa mtu uhai ili ndo gumu but trust me ata miaka 5000 iliyopita watu waliamini akuna kitu kinaeza chunguza anga la mbali lets make it simple i kitu ni physically how can it be impossible?? Unazani ndai joto nikali kuliko litengenezwalo na jua?
Sijaku argue nataka tu tuwaze wote kua it possible.....if we ill be serious
 
Wakati unaelekea kutokea upande wa pili, utazimia mara kadhaa, na hatimae kufa...

Utajikuta sehemu tofauti kabisa...

Cc: mahondaw
 
Hii ni theory na myths tu, coz hizo layer naona waliandika tu. Coz hakuna aliyewahi kwenda huko chini physical na kuziona hizo layer
 
Back
Top Bottom