Pre GE2025 Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha Upinzani kitakuwa na fedha za kampeni sawa na walizonazo CCM?

Pre GE2025 Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha Upinzani kitakuwa na fedha za kampeni sawa na walizonazo CCM?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni.

Vyama vya Upinzani siku zote vimekuwa vikifanya kampeni kwa kuunga-unga na kuzidiwa kwa kiwango kikubwa na CCM.

Sasa sijui mazingira hayo yanachangia kwa kiwango gani[ asilimia ngapi] kushindwa kwa vyama vya upinzani ktk mapambano yao dhidi ya CCM.

Hivyo basi nimewaza kuhusu uchaguzi wa 2025. Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha upinzani kitakuwa na kiwango sawa cha fedha walizonazo CCM? Je, mazingira hayo yatachangia kwa kiwango gani kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyazoea?
 
..hivyo basi nimewaza kuhusu uchaguzi wa 2025. Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha upinzani kitakuwa na kiwango sawa cha fedha walizonazo CCM? Je, mazingira hayo yatachangia kwa kiwango gani kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyazoea?
Haiwezekani kabisa. How?
 
Haiwezekani kabisa. How?

..kwanini haiwezekani?

..kampeni za uchaguzi ni fedha.

..kama wapinzani wanataka kushindana na CCM ni lazima wakabiliane nao ktk kila angel ikiwemo hamasa, na oganaizesheni ya kampeni.
 
Zaidi ya hapo kinatakiwa kuwa na watu serikalini. Hao ndio wanaoiwezesha CCM kusalia madarakani.
 
..sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni...
Ccm hatushindi kwanguvu yapesa .ccm tunashinda kwanguvu ya wanachama wengi na wapenzi wake
 
..sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni...
chanzo cha hizo fedha ni nini? au zimetoka wapi kwa nani? au ni ruzuku?

au ni mkopo wa kuuza nchi wamechukua kutoka kwa fulani wa huko ng'ambo?🐒

kwani sheria ya gharama za uchaguzi inasemage kuhusu ukomo wa matumizi ya ukwasi kwa vyama vya siasa nyakati za uchaguzi?🐒

au ni kuandaa disqualifications za mapema kushiriki uchaguzi?
 
chanzo cha hizo fedha ni nini? au zimetoka wapi kwa nani? au ni ruzuku?

au ni mkopo wa kuuza nchi wamechukua kutoka kwa fulani wa huko ng'amb...

..labda tungeangalia vyanzo vya Ccm halafu tuone ni ktk chanzo kipi wapinzani wanaweza ku-match.

..naona kama Ccm inatumia mapesa mengi sana kukandamiza vyama vya upinzani na hilo ni eneo ambalo linapaswa kuangaziwa.
 
Ccm hatushindi kwanguvu yapesa .ccm tunashinda kwanguvu ya wanachama wengi na wapenzi wake

..kwa macho ya kawaida kampeni za Ccm hufunika kabisa kampeni za wapinzani kwasababu ya FEDHA.

..sasa kama fedha zisingekuwa na umuhimu basi Ccm wasingetumia fedha kwa kiwango tulichozoea kukiona wakati wa kampeni.

..lakini hata ukiangalia kampeni za nchi nyingine hakuna chama kinachofunika vyama washindani kifedha na ukubwa wa kampeni kama Ccm.
 
..labda tungeangalia vyanzo vya Ccm halafu tuone ni ktk chanzo kipi wapinzani wanaweza ku-match.

..naona kama Ccm inatumia mapesa mengi sana kukandamiza vyama vya upinzani na hilo ni eneo ambalo linapaswa kuangaziwa.
wapinzani hawana chanzo kingine chochote cha pesa ispokua ruzuku kidunchu 🐒

kwahiyo ni rahisi mno kuwabaini na kuwahoji pesa wamepata wap, coz ruzuku yenyewe ya upinzan haitoshi kufanya mikutano zaidi ya mikoa mi2 tu.

nadhani ukiachilia mbali vyavyo vingine ikiwa ni pamoja na vitega uchumi vyake, ruzuku yake tu inaweza kutumika kufanya kampeni Africa Mashariki na pesa bado zisiishe 🐒

na hiyo ni kwasababu CCM iko serious, inadhamira na malengo ya kufanya kampeni, kushinda uchaguzi, kushika dollar, kuunda serikali na kuongoza nchi na wananchi 🐒

Lakini pia inafahamika bayana kwamba Elections a very is expensive process.

sasa wewe huna pesa na unaenda kushiriki uchaguzi, kweli?🐒
 
Zaidi ya hapo kinatakiwa kuwa na watu serikalini. Hao ndio wanaoiwezesha CCM kusalia madarakani.

..nakubaliana na wewe kwamba Ccm ina mbinu nyingi ikiwemo msaada wa watu walioko serikalini.

..mada yangu imejikita kwenye FEDHA wakati wa kampeni.

..Utakubaliana na mimi kwamba Ccm wana advantage kubwa sana ya kifedha kulinganisha na wapinzani.

..Je, mazingira hayo yanaathiri MATOKEO kwa kiwango gani?
 
wapinzani hawana chanzo kingine chochote cha pesa ispokua ruzuku kidunchu 🐒

kwahiyo ni rahisi mno kuwabaini na kuwahoji pesa wamepata wap, coz ruzuku yenyewe ya upinzan haitoshi kufanya mikutano zaidi ya mikoa mi2 tu...
Ndio hapo sasa nasema wapinzani lazima watafute namna ya kupata fedha za kampeni ili ku-match ukwasi walionao Ccm.
 
..Ndio hapo sasa nasema wapinzani lazima watafute namna ya kupata fedha za kampeni ili ku-match ukwasi walionao Ccm.
hatari ya kutokua na vyanzo vya kutosha vya pesa kwa chama cha siasa, kwa mfano mpaka sasa hivi vingekua tayari vimeingiza fedha, mathalani kutoka kwa marafiki au mabwenyenye ya magharibi au America kinyemela, huenda pasingekua na shida 🐒

Lakin pia hata hao mabwenyenye marafiki na wafanya biashara wanaangalia mtu mwenyewe wa kumchangia kupitia chama 🐒

kasumba ya vyama vyetu,
ni kwamba siku 90 kabla ya uchaguzi ndio unajua nani ni mgombea urasi wa chama fulani, wakati inchi imeimarisha ulinzi kila kono kila nyanja,

hukuna chama kitaingiza hata sent moja kutoka ng'ambo na kwahiyo mgombea wake hataweza kua na nyenzo kumfikisha katika baadhi ya maeneo nchini,

mwisho wa siku alieshinda ana asilimia 90 , wapinzani ukijumlisha wote wana 8% na kura zilizoharibika ni 2%🐒
 
..sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni....
We jamaa upo ulimwengu gani? CCM inaishi kwa kutegemea katiba hii mbovu, pia kwa kutegemea Tume hii inayoitwa tume huru ya uchaguzi na jeshi la polisi period.

Hakuna kada yoyote angeweza kumshinda mh Freeman Mbowe kule hai. Hata angegombea Marehemu Magufuli.
UWanja ukiwa fair bila kujali gharama ccm ni weupe kama karatasi.

Swali lako lilipaswa kukaa hivi. Hivi ikitokea tukapata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, Upinzani wanaweza kuaminiwa na kupewa nchi waiongoze? Hilo ndio lilipaswa kuwa swali.

Kwanza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu atapata tabu sana kwenye kampeni. Hauziki.
 
Back
Top Bottom