Pre GE2025 Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha Upinzani kitakuwa na fedha za kampeni sawa na walizonazo CCM?

Pre GE2025 Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha Upinzani kitakuwa na fedha za kampeni sawa na walizonazo CCM?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
JokaKuu ishu kuu hapa sio fedha.....

Kusema hivi haina maana kuwa fedha si nyenzo muhimu katika uchaguzi...

CCM hutumia fedha nyingi kama hadaa tu lakini hawa hata kama watumie bajeti yote ya 2024/2025 hawana ushawishi wowote wa kisera na mipango kwa wananchi...

Fedha zao zote hutumika kuandaa matamasha wanayoyaita "kampeni za uchaguzi" huku ukweli ukiwa kuwa hayo huwa ni matamasha ya burudani tu kwa sababu CCM wanajua kuwa kwa ujinga wa watanzania hicho ndicho wanachokihitaji...!
=============================================

Hebu cheki hii..

Kampeni za mwaka 2015 zilikuwa za fedha nyingi sana kwa CCM lakini CHADEMA hawakuwa na fedha kufikia hata robo tu kulinganisha na za CCM lakini bado CCM hii hii ilipigwa kwenye sanduku la kura na mgombea wa CHADEMA ndugu Edward Lowassa.. HAKUTANGAZWA MSHINDI, AKATANGAZWA ALIYESHINDWA John P. Magufuli....!!

Ndivyo ilivyokuwa kule Zanzibar mpaka...

HUKO ZANZIBAR, jamaa kwa makusudi kabisa wakafuta matokeo yote ya uchaguzi baada ya kugundua kuwa Dokta Mohammed Shein (CCM) kapigwa na hayati Maalim Seif Shariff Hamad (CUF)....!!

HIYO IKAPITA. Ukaja uchaguzi wa 2019 na 2020. Kama kawa, CCM wanajua fedha sio kigezo cha kushinda uchaguzi kwa Tanzania. CCM walikuwa na fedha zote kwa kadiri ya mahitaji yao. Wakatajirika kupitia fedha hizo...

CHADEMA na Tundu Lissu hawakuwa hata na robo ya fedha za CCM. Angalia kampeni zao. Watu walikuwa wanakuja wenyewe kwa maelfu na wakampa Tundu Lissu kura kama zote.

TUNDU LISSU HAKUTANGAZWA...!!

Jamaa Magufuli na CCM yake kuona hivyo kuwa ameshalizwa kwenye sanduku la kura, wakapora uchaguzi wote. Akajitangaza kwa nguvu kuwa ndiye mshindi na sasa yuko kaburini, anatawala walio makaburini....!

Kuna Chawa anaitwa Etwege najua anachukia kweli ukimtaja Magufuli kwa mtazamo huu☝🏻☝🏻. Shauri lake. Akitaka amfuate huko aliko, lakini ukweli juu ya historia ya Magufuli wake ndivyo ilivyo na ulivyo...

Mpaka leo hakuna kura za u - Rais ambazo ziko gazzeted kuonesha Magufuli na CCM walipata ngapi kwa kila jimbo kama sheria inavyotaka kutangazwa kwa kura hizo...

Why?

The anaswer is very simple........... Ni kwa sababu walivuruga vuruga kila kitu hata wakapoteana wao kwa wao kiasi cha hesabu kugoma hata kughushika...!!

Hata zile za ubunge na udiwani zote ni utopolo tu. Hakuna aliyeshinda na leo hii kila mtu na kila Mtazanzania analipia uovu na ujinga wa CCM na Magufuli wao.....

The issue here is not about money. Hata bila fedha nyingi kama za CCM CHADEMA watafanya kampeni all over the country kama ilivyofanyika miaka yote ya nyuma....

Kwa sababu CHADEMA kila mwananchi ni wakala wake ktk kampeni. Wananchi tutafanya kampeni kuanzia kwenye familia zetu, mtaani kwetu na tutaeleweka kirahisi....

TANU ya Nyerere haikufanikiwa kupambania uhuru wa Tanganyika kwa sababu ilikuwa na fedha. They had nothing in their pockets lakini mioyo ya watu ilielewa malengo ya TANU. Mkoloni akaondoka....

NDIVYO ILIVYO LEO KWA CHADEMA. Watu wakishaelewa madhara ya kukumbatia mkoloni mweusi CCM, hakuna fedha ya kuzuia mabadiliko na uhuru wa wananchi...!

Ukifika wakati wa CCM kutoweka ktk uso wa nchi ya Tanganyika, na wakati huo tayari umeshafika, basi hakuna kiwango cha fedha kinachoweza kusaidia uwepo wao kuendelea ku - exist ....!!
 
..sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni.

..vyama vya upinzani siku zote vimekuwa vikifanya kampeni kwa kuunga-unga na kuzidiwa kwa kiwango kikubwa na CCM.

..sasa sijui mazingira hayo yanachangia kwa kiwango gani[ asilimia ngapi] kushindwa kwa vyama vya upinzani ktk mapambano yao dhidi ya CCM.

..hivyo basi nimewaza kuhusu uchaguzi wa 2025. Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha upinzani kitakuwa na kiwango sawa cha fedha walizonazo CCM? Je, mazingira hayo yatachangia kwa kiwango gani kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyazoea?
Majibu kwa hoja zako ni rahisi:

- Kwanza haiwezekani kwa chama chochote cha upinzani kuwa na pesa kiasi cha ilicho nazo CCM. Ikitokea ikawa hivyo, hicho chama hakitakuwa na tofauti yoyote na CCM. Hao watakuwa wapo tayari kutuuza kwa mwenye bei atakayo.
Kasoro pekee ni kama chama hicho kimekwenda kwa wananchi, na wananchi wakaamua kujichangsha shilingi, shilingi kila mmoja wao.
- pili, kuiondoa CCM madarakani hakuhitaji kuwa na pesa nyingi zaidi ya kiasi kinacho tosha kuwafikia wananchi huko mitaani waliko na kuwajengea uwezo wa kuikataa CCM. Elimu ya kutosha kwa wananchi, na jinsi ya kuzuia kura zao kuharibiwa.

- Zambia, Malawi, Senegal, na kwingineko kuliko tokea mabadiliko, vyama huko havikusubiri kuwa na ukwasi mkubwa kuwaangusha wakubwa wa huko.
 
Swali lako lilipaswa kukaa hivi. Hivi ikitokea tukapata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, Upinzani wanaweza kuaminiwa na kupewa nchi waiongoze? Hilo ndio lilipaswa kuwa swali.
Nimekubali uliyo sema kwenye jibu lako, ila hili nililo nyanyua hapa.
WaTanzania sasa hatuwezi kutegemea uwepo/kutokuwepo kwa "Katiba Mpya tena"kuwafungasha vilago CCM.

Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba kura tutakazo piga ni kura zitakazo hesabika na kumchagua kiongozi yeyote tunayemtaka atuongoze.
Uwezo wa kuhakikisha hilo linatokea wananchi tunao sana, kinacho kosekana ni mpangilio wa kulitimiza hilo bila ya kumwogopa mtu yeyote yule.

Je, CHADEMA wanaweza kutupanga tuifanye hii kazi vizuri?
 
Sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni.

Vyama vya Upinzani siku zote vimekuwa vikifanya kampeni kwa kuunga-unga na kuzidiwa kwa kiwango kikubwa na CCM.

Sasa sijui mazingira hayo yanachangia kwa kiwango gani[ asilimia ngapi] kushindwa kwa vyama vya upinzani ktk mapambano yao dhidi ya CCM.

Hivyo basi nimewaza kuhusu uchaguzi wa 2025. Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha upinzani kitakuwa na kiwango sawa cha fedha walizonazo CCM? Je, mazingira hayo yatachangia kwa kiwango gani kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyazoea?
Unakumbuka Lowasa alivyotia timu? Tena akiwa dhohofu. Vipi angekuwa timamu?
 
Nimekubali uliyo sema kwenye jibu lako, ila hili nililo nyanyua hapa.
WaTanzania sasa hatuwezi kutegemea uwepo/kutokuwepo kwa "Katiba Mpya tena"kuwafungasha vilago CCM.

Ni jukumu letu kuhakikisha kwamba kura tutakazo piga ni kura zitakazo hesabika na kumchagua kiongozi yeyote tunayemtaka atuongoze.
Uwezo wa kuhakikisha hilo linatokea wananchi tunao sana, kinacho kosekana ni mpangilio wa kulitimiza hilo bila ya kumwogopa mtu yeyote yule.

Je, CHADEMA wanaweza kutupanga tuifanye hii kazi vizuri?
Ni ngumu kuliko unavyo jatibu kufikiri. Shida inakuja hata kama mmeshinda na hesabu za vituo mnazo. Mkurugenzi anamtangaza mgombea wa ccm kashinda. Tena anamtangaza usikj wa manane. Hapo hapo polisi ambao wanakuwa tayari wameandaliwa wanafyatua mabomj ya machozi na bakora za kutosha. Watu wanasambaratika. Ndio imeisha hiuo.

Mnaanza kufungua kesi za kupinga matokeo. Kesi inaendeshwa kwa miaka mi3.
 
Nyerere aliwahi kusema hivi.

"Upinzani wa kweli utatoka Ndani ya CCM"

Swali lako kwa maana nyingine unauliza CCM inaweza kufirisika? Jibu ni hapana as long as long hakuna nguvu ya kijeshi au armed resistance.

Mfumo uliopo unaipa CCM nguvu ya kumiliki chochote Tanzania hata hivyo vyama vya Upinzani inaweza kuvinunua
 
Kampeni ile ya Lowasa na JPM nadhani Ukawa walikuwa na Nguvu sawa na Ccm ila Serikali ikaingilia kati
 
Nyerere aliwahi kusema hivi.

"Upinzani wa kweli utatoka Ndani ya CCM"

Swali lako kwa maana nyingine unauliza CCM inaweza kufirisika? Jibu ni hapana as long as long hakuna nguvu ya kijeshi au armed resistance.

Mfumo uliopo unaipa CCM nguvu ya kumiliki chochote Tanzania hata hivyo vyama vya Upinzani inaweza kuvinunua

..Wapinzani wakiweza kusimamisha wagombea kila sehemu.

..Wapinzani wakifanya mikutano ya kampeni mingi kupita Ccm.

..Wapinzani wakiweza kuweka mawakala kila kituo nchi nzima na kuwalipa.

..Wapinzani wakiweza kugawa t-shirt na kofia nyingi kuliko Ccm.

..Je, matokeo yatakuwa tofauti na tulivyozoea?
 
Issue sio CCM au Upinzani issue ni mfumo Ndio unawapa Watu walioko ndani ya CCM kuwa na nguvu.

Mfano Muangalie mtu nobody kama Samia alivokuwa na Nguvu baada ya kuwa CCM.

Mifumo yote ya Dola inaipa nguvu CCM.

Watu wenyewe, Jeshi na Kamati kuu ya CCM Ndio inaweza kubadili Hali yetu ya Kisiasa na lazima kuwe na coordination ya Hali ya juu ya hivo vitu vitatu, refer to Zimbabwe
 
Ni ngumu kuliko unavyo jatibu kufikiri. Shida inakuja hata kama mmeshinda na hesabu za vituo mnazo. Mkurugenzi anamtangaza mgombea wa ccm kashinda. Tena anamtangaza usikj wa manane. Hapo hapo polisi ambao wanakuwa tayari wameandaliwa wanafyatua mabomj ya machozi na bakora za kutosha. Watu wanasambaratika. Ndio imeisha hiuo.

Mnaanza kufungua kesi za kupinga matokeo. Kesi inaendeshwa kwa miaka mi3.
Mkuu 'Ziroseventytwo', nikupe pongezi nyingi kwa jibu lako hili.
Na kwa dhati ya moyo wangu wote, nakuomba tulijadili hili kwa undani wake kamili, kwa sababu najuwa inawezekana kabisa kukomesha haya unayozungumzia wewe hapa.

Sasa tufanyeje, tuweke mada inayojitegemea kujadili njia zinazoweza kutumiwa na wananchi kuzima uharibifu wa kura zao wakati wa uchaguzi, au tuendeleze mjadala huo hapahapa?

Mimi ningependa pawe na mada inayo jitegemea yenyewe kuhusu hili.

Naomba na wachangiaji wengine watoe maoni kuhusu hili.

Nipe mrejesho haraka tuianze kazi hii.

Mkuu 'JokaKuu' nimemwona akiambaa ambaa sehemu, hebu toa ushauri tufanye nini hapa.
 
Issue sio CCM au Upinzani issue ni mfumo Ndio unawapa Watu walioko ndani ya CCM kuwa na nguvu.

Mfano Muangalie mtu nobody kama Samia alivokuwa na Nguvu baada ya kuwa CCM.

Mifumo yote ya Dola inaipa nguvu CCM.

Watu wenyewe, Jeshi na Kamati kuu ya CCM Ndio inaweza kubadili Hali yetu ya Kisiasa na lazima kuwe na coordination ya Hali ya juu ya hivo vitu vitatu, refer to Zimbabwe
Mkuu 'Stormryder' mchango wako mzuri, lakini sikubaliani nao. Hakuna mfumo unaoweza kushinda adhma ya wananchi popote pale.
Hizi ni' excuses' zisizokuwa na nguvu hata kidogo.
Hiyo mifumo inafanya kazi kwa sababu inawasoma wananchi. Wananchi waliopania kukataa hiyo mifumo, hata ifanye nini haiwezekani kuharibu kura zao.
 
Mkuu 'Ziroseventytwo', nikupe pongezi nyingi kwa jibu lako hili.
Na kwa dhati ya moyo wangu wote, nakuomba tulijadili hili kwa undani wake kamili, kwa sababu najuwa inawezekana kabisa kukomesha haya unayozungumzia wewe hapa.

Sasa tufanyeje, tuweke mada inayojitegemea kujadili njia zinazoweza kutumiwa na wananchi kuzima uharibifu wa kura zao wakati wa uchaguzi, au tuendeleze mjadala huo hapahapa?

Mimi ningependa pawe na mada inayo jitegemea yenyewe kuhusu hili.

Naomba na wachangiaji wengine watoe maoni kuhusu hili.

Nipe mrejesho haraka tuianze kazi hii.

Mkuu 'JokaKuu' nimemwona akiambaa ambaa sehemu, hebu toa ushauri tufanye nini hapa.

1. wakala wa upinzani ktk kila kituo, na alipwe.

2. Mfumo independent wa wapinzani kukusanya, na kujumlisha, matokeo.

3. waangalizi huru wa uchaguzi, kwa mfano taasisi za kidini, NGOs, ktk kila kituo.

Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa UWAZI ktk kuhesabu kura, na kutangaza matokeo.
 
Sijui kama wachambuzi wa siasa na chaguzi zetu wameangazia vya kutosha suala la FEDHA na RASILIMALI wanazokuwa nazo CCM wakati wa kampeni.

Vyama vya Upinzani siku zote vimekuwa vikifanya kampeni kwa kuunga-unga na kuzidiwa kwa kiwango kikubwa na CCM.

Sasa sijui mazingira hayo yanachangia kwa kiwango gani[ asilimia ngapi] kushindwa kwa vyama vya upinzani ktk mapambano yao dhidi ya CCM.

Hivyo basi nimewaza kuhusu uchaguzi wa 2025. Nini kitatokea ikiwa chama kimojawapo cha upinzani kitakuwa na kiwango sawa cha fedha walizonazo CCM? Je, mazingira hayo yatachangia kwa kiwango gani kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyazoea?
Watakaoleta mapinduzi ndani ya Tz siyo CCM wala CDM au ATC, siku ya mapinduzi ikifika hatokuwepo mwenye hela, mwenye jeshi au sera gani sijui. Siku tukifika na wenye nchi wakisema imetosha, basi ....., usiulize itakuwa lini.
 
1. wakala wa upinzani ktk kila kituo, na alipwe.
Haitoshi, kama ni swala la kulipwa tu. CCM wanyo mahela chungu nzima ya kuwanunua wote hao. Ni lazima hao "wakala" wawe na kitu cha ziada. Hili ndilo CHADEMA wangekuwa wanalifanyia kazi kwa makini sana wakati huu.
2. Mfumo independent wa wapinzani kukusanya, na kujumlisha, matokeo
Walisha jaribu hili likavurugwa. Huko Kenya Raila alijaribu mara kadhaa likavurugwa. Wakiamua kuliendeleza wawe tayari kulijengea uimara lisivurugwe.
Kisheria, sijui kama linakubalika.
3. waangalizi huru wa uchaguzi, kwa mfano taasisi za kidini, NGOs, ktk kila kituo.
Hapa tulipo fikia kabla ya uchaguzi kuanza, utaratibu huu utaingizwa vipi kwenye mipango ya chaguzi hizi? Ni wazo zuri; lakini CCM wapo tayari kulikubali? Watafanya kila mbinu kulihujumu. Kisheria halipo mahali popote katika taratibu za uchaguzi.
Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa UWAZI ktk kuhesabu kura, na kutangaza matokeo.
kama hili ndilo tatizo, na ninakubali ni tatizo. Wakati ni sasa tukune vichwa vyetu kuchangia njia za kuliondoa hili. Na njia ninayo iona mhimiri wake ni wananchi wenyewe waliopania kuzuia uharibifu huo.

TATIZO: "KUKOSEKANA KWA UWAZI KTK KUHESABU KURA,..." NA KUTANGAZA MATOKEO (kutangaza matokeo ni rahisi kudhibiti)
 
1. wakala wa upinzani ktk kila kituo, na alipwe.

2. Mfumo independent wa wapinzani kukusanya, na kujumlisha, matokeo.

3. waangalizi huru wa uchaguzi, kwa mfano taasisi za kidini, NGOs, ktk kila kituo.

Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa UWAZI ktk kuhesabu kura, na kutangaza matokeo.
unaikumbuka Arab spring, ikumbuke Philino enzi ya Corazon Aquino na mumewe, etc etc
 
Tuko mbioni kuizidi ccm hela za Kampeni
makamu mwenyekiti wa chama chenu cha wachaga anachangisha upatu kununua gari pesa ya uchaguzi mtoe wapi? M/kiti wa maisha mboye pesa aliyohongwa kishaimalizia kwenye konyagi
 
Haitoshi, kama ni swala la kulipwa tu. CCM wanyo mahela chungu nzima ya kuwanunua wote hao. Ni lazima hao "wakala" wawe na kitu cha ziada. Hili ndilo CHADEMA wangekuwa wanalifanyia kazi kwa makini sana wakati huu.
Walisha jaribu hili likavurugwa. Huko Kenya Raila alijaribu mara kadhaa likavurugwa. Wakiamua kuliendeleza wawe tayari kulijengea uimara lisivurugwe.
Kisheria, sijui kama linakubalika.
Hapa tulipo fikia kabla ya uchaguzi kuanza, utaratibu huu utaingizwa vipi kwenye mipango ya chaguzi hizi? Ni wazo zuri; lakini CCM wapo tayari kulikubali? Watafanya kila mbinu kulihujumu. Kisheria halipo mahali popote katika taratibu za uchaguzi.
kama hili ndilo tatizo, na ninakubali ni tatizo. Wakati ni sasa tukune vichwa vyetu kuchangia njia za kuliondoa hili. Na njia ninayo iona mhimiri wake ni wananchi wenyewe waliopania kuzuia uharibifu huo.

TATIZO: "KUKOSEKANA KWA UWAZI KTK KUHESABU KURA,..." NA KUTANGAZA MATOKEO (kutangaza matokeo ni rahisi kudhibiti)

..hapo nime-cover the basics.

..wapinzani wawe na wakala lila kituo, na wamlipe.

..kama Ccm watamhonga uwezekano ni wakala wa upinzani kuwa na maokoto kuliko wakala wa Ccm.

..wakala wa upinzani aliyelipwa na akaongezewa cha juu na Ccm, kwangu mimi ana afadhali kuliko wakala ambaye wapinzani hawajamlipa kabisa.
 
Back
Top Bottom