Nini kusudio la Mwenye enzi Mungu kuwapa viumbe wake uzao usio kikomo?

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,882
Reaction score
5,087
Ukikata tunda la Papai ndani utakuta mamia kama sio maelfu ya mbegu, ambazo nazo zinatarajiwa kila moja kuwa Mpapai ambao nao tena utatoa mamia ya Papa yenye mamia ya mbegu ndani kwa ajili ya kuzalisha Mpapai mingine. Na ni vivyo hivyo kwa mimea mingine.

Mtu mume akisha baleghe ana uwezo wa kuwapa uja uzito mamia kama sio maelfu ya Wanawake kama atataka kufanya hivyo.

Nimetafakari sana na kujiuliza vipi kama Dunia ina uwezo wa kuhimili viumbe za uzao wake iwapo kila kitu kitaenda kama Muumba alivyokusudia?.
 
Vipi umechoka? Mbona mapema sana?
Kaza buti yajayo ni siri yake, we komaa na ya leo.
 
Vyote vinavyoweza kuzaliana, hufa baadaye
 
Quran
87:2 aliyeumba na akaweka sawa.
87:3 ambaye amekadiria na akaongoa

Hivyo kila kitu kiko katka balance yake usiogope na vina wakati maalum vyote vitasimama Kwa amri Moja ya neno naatabaki peke yake Kwa miaka mingi tu kuonyesha kwamba kila chenye chembe ya uhai kina muda maalum isipokua yeye
 
Vipi umechoka? Mbona mapema sana?
Kaza buti yajayo ni siri yake, we komaa na ya leo.
Kuna wakati huwa nafikiri labda Dunia ina mfumo wake wa kujihuisha kila baada ya muda fulani.
 
We rudi ndani kaendelee kuzaa tu usiogope.

Ya dunia hii hata yasikupe shida, kama ulivyoikuta utaiacha kama watangulizi wetu.

IShi maisha acha siasa za dunia.
 
Kuna wakati huwa nafikiri labda Dunia ina mfumo wake wa kujihuisha kila baada ya muda fulani.
Kweli inaji update kimazingira ndo maana utasikia kuna viumbe fulani vinakuwa extinct sababu mazingira hayasapoti kuwepo, au binadamu kubadilika ki genetic, mfano zamani [ cave people ] walikuwa wana taya kubwa sababu ilibidi wale nyama ambayo haijachomwa vizuri inakuwa kama mbichi ila sasa tunachemsha nyama,choma na kukaanga inaiva vizuri inakuwa laini hivyo tunakuwa na taya ndogo, pia hata maumbo zamani walikuwa wanatumia nguvu kubwa akili kidogo ila sasa akili nyingi nguvu kidogo hivyo maumbo yanapungua,, hivyo huenda dunia inaji update kutokana na muda
 
Je hili linaweza pia kutufikirisha kuhusu Binadamu walivyo jenga Pyramids?kwamba walikuwa na uwezo ambao kwa zama hizi haiwezekani bila kutumia mashine?.
 
Kuweka point yangu sawa,ukomo ninaouzungumzia hapa si wa vizazi kwa maana ya Baba,Babu,Mjukuu,Kitukuu,Kilembwe n.k la hasha.Hapa nazungumzia ukomo ndani ya Binadamu au Kiumbe mmoja.Yaani tukihesabu mbegu(shahawa)anayozalisha Mtu mume mmoja tangu baleghe mpaka anapofika miaka themanini ni mabilioni ya mbegu,na zote zinakusudiwa kutunga mimba iwapo zitakutana na yai la Mtu mke.Naye Mtu mke hupata hedhi kila mwezi inayomaanisha kuwa yai lake linapotea bure kwa kukosa kirutubishi(mbegu)ili hali yeye alikuwa tayari.Inanistaabisha sana.Hivi si ingetosha sana tu kama kila Mtu mume mmoja angepewa mbegu moja au mbili au tatu?.
 
Sidhani kama ni hivyo ila nafikiri ni hivi, tupo kwenye ulimwengu wa chances!.. Namaanisha ni kama uwe na sehemu yakulenga moja na uwe na mshale mmoja hapo chance yakupata ni ndogo!, so nature ikaamua iwe na mishale mingi ili ikiirusha basi katika ile mishale basi mmoja wapo utapatia point!.

mbegu za papai ni nyingi lakini katika hizo nyingi mpaka itakayokuja kukua na kukomaa unakuta hazifiki hata kumi!.. Mazingira yametawaliwa na hatari nyingi tena hivyo hata chances za kusurvive huwa ni chache pia!.
Jambo hili lipo hata kwa binadamu just angalia unaambiwa binadamu wakiume mmoja anauwezo wakutoa billion za sperms!, lakini angalia muda ambao binadamu mpaka sasa yupo kwenye hii dunia ndio kwanza tupo 8 billion!, wakati kwa hiyo idadi tu ni mipigo kadhaa ya mtu mmoja!..😅
Hivyo kama kwa kila mwanaume anaweza kutoa Billions of sperms hivyo sasahivi tulitakiwa tuwe hata zillions of people!.

Hili jambo linanifanya hata nifikirie kuwa huenda hata maisha kupatikana kwenye sayari fulani hutokea by chances!, na ndio maana mpaka sasa tumegundua sayari nyingi lakini bado imekuwa ni ngumu kupata sayari yenye uhai zaidi ya hii yakwetu!.
Usikute maisha kuwepo kwenye sayari fulani hutokea kama vile me na ke wanavyofanya tendo!, ama namna fulani ambayo inahusiana na hilo!..

Fikra zangu hazijaamua kuishia hapo tu vilevile zimenipeleka huenda hata plan ya kuwa na kiumbe aitwae binadamu ni katika namna yakuisaidia nature kusambaza huo uhai ktk ulimwengu!, maana katika viumbe vyote kwenye hii dunia ni binadamu pekee ndio anaewaza kuhama hii sayari nakwenda kuanzisha maisha sayari nyengine!, na ni huyohuyo kiumbe ndie anaewaza ku modify hata mbegu ama uhai ktk namna mbalimbali!, so it seems like tunafanya kazi fulani kwa kudhani tunajifanyia sisi kumbe ni maelekezo ila hatujui!.
Kitu chochote ambacho kitavamia kiumbe chochote hapa duniani basi binadamu tutawajibika kupigana na hicho kitu!, hata kama hicho kitu hakitudhuru sisi ila sisi kama waangalizi na walinzi tunawajibika kupambana!.
Sijui kama mlishawahi kuwaza hichi kitu...?!
kwa kiasi kikubwa sisi binadamu ni waangalizi na watatuzi wa kitu chochote ambacho kitaingia hapa duniani!.

It's just matter of time binadamu anaenda kuweza kuhama hapa duniani nakuanzisha makazi sayari nyengine na huko ataweza kupanda mimea nakuanzisha kila kitu kama ecosystem ilivyo hapa duniani!.
 
Kweli kabisa Michio Kaku anasema tumebakisha miaka kama 50-100 kufika type 1 civilization tukifika hapo itakuwa step kubwa sana
 
Kweli inaji update kimazingira ndo maana utasikia kuna viumbe fulani vinakuwa extinct sababu mazingira hayasapoti kuwepo, au binadamu kubadilika ki genetic, mfano zamani [ cave people ] walikuwa wana taya kubwa sababu ilibidi wale nyama ambayo haijachomwa vizuri inakuwa kama mbichi ila sasa tunachemsha nyama,choma na kukaanga inaiva vizuri inakuwa laini hivyo tunakuwa na taya ndogo, pia hata maumbo zamani walikuwa wanatumia nguvu kubwa akili kidogo ila sasa akili nyingi nguvu kidogo hivyo maumbo yanapungua,, hivyo huenda dunia inaji update kutokana na muda
Naomba kuuliza kidogo,. Kama Mazingira ndiyo determinant ya Kiumbe kipi kiwepo na kipi kisiwepo,. Kwanini Mazingira hayaleti viumbe vipya yaani Mimea,matunda, wanyama na kadhalika?

Namaanisha kwanini inaonekana kuna possibility tu ya mazingira kupelekea kupotea kwa viumbe na si mazingira kupelekea uwepo wa viumbe wengine wapya kabisa?
 
It's just matter of time binadamu anaenda kuweza kuhama hapa duniani nakuanzisha makazi sayari nyengine na huko ataweza kupanda mimea nakuanzisha kila kitu kama ecosystem ilivyo hapa duniani!.
Kwamba Binadamu akapande mimea na kuanzisha ecosystem kwenye sayari nyingine? kinadharia inawezekana,... ila cha kujiuliza kwanini Mimea na ecosystem kwa ujumla isijizukie tu kwenye hizo sayari nyingine kama zilivyojizukia hapa Duniani, mpaka itegemee Binadamu wafanye hivyo na wakati huo Binadamu pia ni part ya hiyo Ecosystem?
 
Naomba kuuliza kidogo,. Kama Mazingira ndiyo determinant ya Kiumbe kipi kiwepo na kipi kisiwepo,. Kwanini Mazingira hayaleti viumbe vipya yaani Mimea,matunda, wanyama na kadhalika?

Namaanisha kwanini inaonekana kuna possibility tu ya mazingira kupelekea kupotea kwa viumbe na si mazingira kupelekea uwepo wa viumbe wengine wapya kabisa?
Ulimwengu hautengenezi matter tena hivyo ni vigumu kutengeneza vitu vipya kabisa labda ifanyike mutation
 
Sasa mkuu huamini kwenye round earth hata nikikuelezea utacheka tu na maelezo utayaweka pembeni
Hahh usitoke nje ya mada uzi wa round/flat earth upo unasubiri watu wathibitishe tu,.. kwenye hoja yako hii nilitaka nijue toka kwako umejuaje kama ulimwengu ndiyo ulitengeneza matter na Je hiyo hoja yako inamaanisha Ulimwengu ulikuwepo before bila ya uwepo wa matter yoyote,.. sasa kwa mantiki hiyo ulimwengu wenyewe ni nini?
 
umejuaje kama ulimwengu ndiyo ulitengeneza matter
kutokana na theory ya big bang, ilivyotokea ukatengeneza matter na antimatter
Ulimwengu ulikuwepo before bila ya uwepo wa matter yoyote,..
Kabla ya big bang ilikuwepo kitu kinaitwa inflation ambapo space ilikuwa ni cold ikiwa na energy tu, kabla ya inflation haijulikano bado ila inawezekana kulikuwa na big bang nyingine kwenye universe nyingine
sasa kwa mantiki hiyo ulimwengu wenyewe ni nini?
Ulimwengu ni kitu [sina jina lingine ] ambacho kimebeba space time,matter na energy na kila kitu solar sytem galaxy . Hivyo ndivyo inavyojulikana kwa sasa
 
kutokana na theory ya big bang, ilivyotokea ukatengeneza matter na antimatter

Kabla ya big bang ilikuwepo kitu kinaitwa inflation ambapo space ilikuwa ni cold ikiwa na energy tu, kabla ya inflation haijulikano bado ila inawezekana kulikuwa na big bang nyingine kwenye universe nyingine

Ulimwengu ni kitu [sina jina lingine ] ambacho kimebeba space time,matter na energy na kila kitu solar sytem galaxy . Hivyo ndivyo inavyojulikana kwa sasa
So, ulimwengu ulikuwepo before au after bing bang? lakini pia hapo hujaonyesha kwamba ulimwengu ndiyo umetengeneza matter bali umeonyesha kwamba bing bang ndiyo imetengeneza matter.

Hoja yako ime base kwenye nadharia tu,. naona nikiendelea kuuuliza hutokua na majibu maana kadri unavyoelezea unazalisha maswali mengi mno,.. ngoja niishie hapa.
 
Back
Top Bottom