GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nchi yetu Haina dini, hilo linafahamika. Lakini karibia kila tukio la kitaifa, lazima viongozi wa dini wawepo kwa ajili ya sala.
Hiyo inamaanisha nini?
1. Watawala wanaamini sana katika maombi?
Sidhani, kwa sababu kama ndivyo, kwa nini wawaalike wa dini zenye maarufu pekee? Mara nyingi utawakuta wa CCT, TEC, BAKWATA, na FPCT. Sijawahi kusikia SDA wamealikwa
2. Wanasiasa wanawatumia viongozi wa dini kwa manufaa yao? Sina uhakika.
Kama lengo ni maombi, wangeweza kuombewa bila makamera, na wasingelazimika kuwaalika viongozi wa dini zote kubwa. Sidhani kama wanasiasa wote wanaamini katika dini, na kama wanaamini, siyo rahisi mtu awe anayaamini maombi ya dini zote!
Mtu hawezi kuwa Mpentekoste, kwa mfano, na bado akaamini kuwa maombi ya Shehe, Padri na Mchungaji kutoka CCT yatamsaidia.
3. Viongozi wa dini wanajipendekeza kwa watawala?
Nafikiri huwa wanapewa "nauli" au hela ya maji baada ya huduma. Lakini hilo linaweza likawa kichocheo cha wao kuhudhuria hayo matukio, hasa ikizingatiwa kuwa wengi wao wanapewa mishahara na waajiri wao? (dini)
Sina jibu la moja kwa moja, lakini lazima kuna sababu.
Nchi haina dini, lakini matukio mengi ya kitaifa hufunguliwa kwa maombi!