Mama Mwana
JF-Expert Member
- Jun 6, 2023
- 2,435
- 7,784
Nimeota nipo sehemu nisioijua ni kama mji hivi, umechangamka kiasi nikajikuta na mtu nisiemjua, tukaenda kwenye mwembe uliokua umemwaga maembe mengi lakini hayana muokotaji.
Basi tukaanza kuyaokota lakini mengi yalikua mabichi nikasema niokote mabichi ndio makubwa na la kuiva lilikua dogo nililiokota hivohivo, kwa pembeni kulikua na nyasi nikahisi uwepo wa nyoka mweusi mdogo, nikarusha jiwe sikujua kama lilimpata au la, nikajikuta kwenye mfuko nina embe moja tu lililoiva dogo.
Nikawa najiuliza inawezekanaje wakati nimeokota mengi sana na yule mtu alinipotea tu sikumuona, nikajikuta nipo mjini kwenye huo mji, kilichonifanya nijue hapa ni mjini ni wingi wa magari ajabu kila gari ninayotaka kuipanda imejaa na haisimami, mwisho ikaja gar haikua na watu wengi nikaingia lakini lile gari likakwama kuondoka.
Nikashtuka, inaweza kuwa kuna kitu gani kinaendelea? naomba kutafsiriwa kwa anejua.