Nini maana ya ndoto hii?

Nini maana ya ndoto hii?

Nimeota nipo sehemu nisioijua ni kama mji hivi, umechangamka kiasi nikajikuta na mtu nisiemjua, tukaenda kwenye mwembe uliokua umemwaga maembe mengi lakini hayana muokotaji.

Basi tukaanza kuyaokota lakini mengi yalikua mabichi nikasema niokote mabichi ndio makubwa na la kuiva lilikua dogo nililiokota hivohivo, kwa pembeni kulikua na nyasi nikahisi uwepo wa nyoka mweusi mdogo, nikarusha jiwe sikujua kama lilimpata au la, nikajikuta kwenye mfuko nina embe moja tu lililoiva dogo.

Nikawa najiuliza inawezekanaje wakati nimeokota mengi sana na yule mtu alinipotea tu sikumuona, nikajikuta nipo mjini kwenye huo mji, kilichonifanya nijue hapa ni mjini ni wingi wa magari ajabu kila gari ninayotaka kuipanda imejaa na haisimami, mwisho ikaja gar haikua na watu wengi nikaingia lakini lile gari likakwama kuondoka.

Nikashtuka, inaweza kuwa kuna kitu gani kinaendelea? naomba kutafsiriwa kwa anejua.
Sio mtaalamu sana ila hapo gari kukwama hapo inatakiwa uombe baraka zako kuna vitu vinakwamisha inabidi ukatae hzo roho zakukwamishwa
 
Kinacho kukwamish ni hayo uliosema maemb mengi mabichi (hayaliki ni machachu) yan watu wasio na faida au ambao hawakusaidii ni wengi, una ukoo wako lkn mambo mengi upo mwenyewe, Muombe Allah upate watu wenye faida ili ufanikishe jambo lko peke ako hutaweza tafuta timu nzuriii
hio timu nzuri anyway point kuu ni kuzidisha ibada kila kitu kitakaa sawa umenipa tafakuri sana leo nimeshinda siko sawa nafikiri mnooo
 
Msikilize mtaalam Sasa,nyoka kwenye ndoto yyte huwasilisha uzinzi, na mizagamuo isiyo rasmi,maembe tuseme ni Wanaume na aina ya Wanaume,kifupi kuchagua chagua kutakufanya uchelewe kupata mtu sahihi,na Hilo litakucheleweshea Ndoa ambayo unaitamani.Upoo?
 
Msikilize mtaalam Sasa,nyoka kwenye ndoto yyte huwasilisha uzinzi, na mizagamuo isiyo rasmi,maembe tuseme ni Wanaume na aina ya Wanaume,kifupi kuchagua chagua kutakufanya uchelewe kupata mtu sahihi,na Hilo litakucheleweshea Ndoa ambayo unaitamani.Upoo?
nimeolewa mtaalam vipi kuhush hilo na ramli yako feki
 
Kuna mwanaume alikuhadaa au ata kuhadaa kufanya jambo ambalo Kwa picha ya nje litaonekana Lina manufaa lakini baadae halitokuwa na manufaa. Kwa kifupi mtu huyo atakupotezea sana muda.😭😭😭😭

Atasababisha hata wengine uwanyime nafasi na wao pia kipindi ambacho huyo mtu atakuwa ameondoka awatokupa nafasi...!​
 
Back
Top Bottom