Nini maana ya neno kuokoka?

Nini maana ya neno kuokoka?

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
286
Reaction score
597
Maana ya Kwanza
Kuhokoka nikukombolewa kutoka kwenye hatari

Matendo ya Mitume 27:41-44
[41]Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi.
.
[42]Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia.

[43]Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu;
:
[44]nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama.

Matendo ya Mitume 28:1
[1]Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita.

Kwa hiyo MTU aliyeokoka ni MTU ambaye amekombolewa au kunyakuliwa kutoka kwenye Moto WA milele

Mathayo 25:41,46
[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
:
[46]Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Maana ya pili
Kuokoka maana yake ni Kuzaliwa katika Roho, kama vile mwanadamu anavyozaliwa katika mwili kadharika wokovu ni Kuzaliwa katika Roho

Yohana 3:3-6
[3]Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

[4]Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

[5]Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

[6]Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Maana ya Tatu
Kuokoka ni kuhamishwa kutoka chini ya ufalme wa Giza ( ufalme wa shetani na malaika zake) na kuingizwa katika ufalme wa nuru ( ufalme wa Mungu aliyehai katika Kristo Yesu)

Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
 
Pia kuokoka ni kunusurika na hatari ambayo ilikuwa ikupate, waliokoka wamenusurika kwenda kwenye moto wa milele.
 
Katika Ukristo hakuna kuokoka , kwani Bwana Yesu alishasema

1695870500682.jpeg
 
Ni nini maana ya kuokoka?

Kwanza kabisa naomba niieleweke, hilo swali silijuwi jibu lake wala sifanyi utani wala sifanyi kejeleli.

Mimi ni Muislam naongozwa na Qur'an kwa hiyo siwezi kumfanyia mtu kejeli kwa imani yake wala sipendi kufanyiwa kejeli kwenye imani yangu. Qur'an inanifundisha;

Qur'an 3:64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu. 64

Tujadili ni nini maana ya kuokoka kwa staha na amani kwa sababu pengine tunaongelea kitu kimoja lakini kwa ndimi (lexicon) tofauti ndiyo maana tunashindwa kuelewana.
 
Asanteh kwa swali zuri. Kuokoka ni hali yakuepuka janga lililowaumiza au kuwaangamiza wengine... Mfano Ajali kwa wale waliotoka wazima ilhali kuna wengine wamepoteza maisha. Tunasema wale wameokoka katika ajali ile. Kwa mfano huo unaweza ukapata na mingine mingi.

Ila sijajua kwanini umehuaisha imani za kidini katika neno litumikalo katika imani zote na maana yake tukiijua?
 
KUOKOKA NI KUMPOKEA NA KUMFANYA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WAKO

MaranAtha-Bwana Wetu Yesu Kristo Anakuja View attachment 2806936
Mimi ni mkristo... Nimejitahidi sana kutafuta mstari unaonipa uhakika wakuwa nikifanya hivyo nimeokoka ila nimeukosa... Yote inayoelezea wokovu ipo katika wakati ujao. Je, Ni Mstari gani au andiko gani linalotuthibitishia.. nikifanya hivi au vilw nitakua nimeokoka na sio nitakuja kuokoka?

Namaanisha... Kwanini tuseme tumeokoka wakati maandiko yanatuambia Tutaokoka.?

Halafu tusipende kulazimisha udini katika mada zilizo wazi. Swali ni nini maana ya Kuokoka. wewe imekuja na habari za Wokovu... kitu ambacho nakuona umenasa kwenye mtego wa mtoa mada.
 
Biblia inasema Warumi 10: 9-10

Kwasababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka. kwa maana kwa moyo mtu huamini na hata kupata haki na kwa kinywa mtu hukiri hata kupata Wokovu.

Kuokoka ni kuzaliwa upya, ikiwa na maana kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako...

Hapa lazima uombe Sala ya Toba...

Ili utakaswe kwa damu ya YESU uondolewe dhambi zote zako na za ukoo wako...

Hapa unakuwa umempokea Yesu tayari na kuwa ndio msaidizi wako kwa Kila jambo...

Kuna tofauti ya kuokoka na kuishi wokovu...

NB: Kuokoka sio rahisi ni lazima ujikane mwenyewe alafu umfuate Yesu...
 
Ww hujauliza kwa nia ya kujifunza ni unafiki tu unakusumbua ww ya wakristo yana kuhusu nn maana hata wakikueleza kwa ulivo mdini wanatwanga maji kwenye kinu.KUOKOKA NI KUACHA UISLAM NA KUJA KWA MUNGU WA KWELI.
Napingana na wewe.. kwanini umenasa kwenye mtego.. ina maana huo wokovu wako haukusaidii maono. na kama umeliona hilo kwanini usiliepuke?

Kuokoka hakuna Dini... ni hali tuipitiayolatikamazingira ya maiaha yetu ya kilasiku.. labda kama angeuliza maana ya Wokovu hapo ndio ungetoa hili povu.
 
Asanteh kwa swali zuri... Kuokoka ni hali yakuepuka janga lililowaumiza au kuwaangamiza wengine... Mfano Ajali.. kwa wale waliotoka wazima ilhali kuna wengine wamepoteza maisha.. Tunasema wale wameokoka katika ajali ile. Kwa mfano huo unaweza ukapata na mingine mingi..

Ila sijajua kwanini umehuaisha imani za kidini katika neno litumikalo katika imani zote na maana yake tukiijua?
Nimeuliza kiimani, kwa sababu huwasikia wengi hususan wasio waislam wakisema "nimeokoka, ameokoka, wameokoka" likihusika na imani zao.

Ndiyo nauliza ni nini maana ya kuokoka?
 
Biblia inasema Warumi 10: 9-10

Kuokoka ni kumkiri Yesu kwa kinywa chako...Kuokoka ni kuzaliwa upya, ikiwa na maana kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako...

Hapa lazima uombe Sala ya Toba...

Ili utakaswe kwa damu ya YESU uondolewe dhambi zote zako na za ukoo wako...

Hapa unakuwa umempokea Yesu tayari na kuwa ndio msaidizi wako kwa Kila jambo...

Kuna tofauti ya kuokoka na kuishi wokovu...

NB: Kuokoka sio rahisi ni lazima ujikane mwenyewe alafu umfuate Yesu...
Tunapata uhakika wa Tumeokoka kutoka katika andiko gani?
 
Biblia inasema Warumi 10: 9-10

Kwasababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka. kwa maana kwa moyo mtu huamini na hata kupata haki na kwa kinywa mtu hukiri hata kupata Wokovu.

Kuokoka ni kuzaliwa upya, ikiwa na maana kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako...

Hapa lazima uombe Sala ya Toba...

Ili utakaswe kwa damu ya YESU uondolewe dhambi zote zako na za ukoo wako...

Hapa unakuwa umempokea Yesu tayari na kuwa ndio msaidizi wako kwa Kila jambo...

Kuna tofauti ya kuokoka na kuishi wokovu...

NB: Kuokoka sio rahisi ni lazima ujikane mwenyewe alafu umfuate Yesu...
 
Kuokoka ni tendo la Imani, ni dhamira ya moyoni mwako...
 
Nimeuliza kiimani, kwa sababu huwasikia wengi hususan wasio waislam wakisema "nimeokoka, ameokoka, wameokoka" likihusika na imani zao.

Ndiyo nauliza ni nini maana ya kuokoka?
Walokole ndio huokoka
 
Kiuhalisia hakuna alieokoka hapa duniani Kwa Sasa, huo ni msemo tu umeibuliwa ili kuleta maana Kwa watu wanaoacha na kuchukia dhambi.

Ila mpaka atakapokufa akiwa mtenda mema ndio hapo atakuwa ameokoka

Au

Atakevumilia mateso yote wakati wa siku za mwisho na asisaliti imani yake juu ya Mungu, mpaka kurudi mara ya pili Kwa Yesu Kristo endapo akiwa hai, huyo atakuwa ameokoka.

Reference Yesu yeye mwenyewe alisema
"""" Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka """ Matthew 24:13
 
Back
Top Bottom