Nini madhara ya kuoa binti kutoka familia fukara?

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Hapa mtaani kuna dada mmoja anafanyakazi mjini (nadhani kariakoo) amejenga nyumba yake. Sasa huyu dada ana msichana wa kazi mzuri anaridhisha sura, umbo, na chura. Umri wake kama miaka 17 kuelekea 18 na anaanza kujitambua. Sasa kuna jamaa (kijana in his late 20s and early 30s) anajiweza yuko vizuri kiasi na kavutiwa na huyo binti kuchukua jiko.

Baada ya kuongea na huyo msichana kutaka kujua ABC kagundua mama yake aliachana na baba yake na hakuwahi kumuona hila anasikia bado yupo. Baba yake ni mvuvi huko kanda ya ziwa. Huyo bosi wake anayemfanyiakazi anadai ni ndugu wa karibu alimchukua kumsaidia kulea mwanae!

Kilichomshitua jamaa ni kuona baba yake analialia kwa mwanae amtumie chochote anachokipata huko mjini kuonyesha kwa jinsi gani choka mbaya.

Sasa akaja kuniomba ushauri kuhusu kuoa binti aliyetoka familia duni kama hiyo hata kama ni mzuri si atakuwa na yeye kajidumbukiza kwenye ufukara?
 
Ufukara si ugonjwa wa kurithi ila ni matokeo tu tabia ya familia au jamii fulani kutokujua kuwekeza vyema kwa ajili ya kesho.
Yeah watu wanachanganya kwa kufananisha ufukara na ulemavu.
Wewe ikiwa umezaliwa kwenye familia ya utajiri sio ujanja wako na yeye akiwa amezaliwa kwenye familia ya kifukara si kosa lake ni kosa la wazazi wake.
Kwa hiyo kwenye ishu ya kuoa wewe angalia huyo mwanamke ana upeo gani wa kuchanganua mambo,je anafaa kuwa mama bora wa familia?je ukimfungulua biashara ataweza kuisimamia?je ukisafiri akabaki peke yake anaweza kuendesha mji wako na kuichunga familia?
Na sio kuangalia kwao ni matajiri au mafukara.
 
Asante kwa maoni yako! Lakini kiufupi binti wa asili kama hiyo kiwango chake cha ufahamu automatically ni cha chini. Kuna pia changamoto ya kutojua mechanism ya kanuni ya maisha kutakakopelekea kuvutwa upande wa kwao na huyo binti kujaribu kuwasaidia kwa gharama za kipato cha familia ya mme wake! Mwisho wa siku nao wataburuzwa kwenye umasikini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…