Nini madhara ya kuoa binti kutoka familia fukara?

Nini madhara ya kuoa binti kutoka familia fukara?

Ko wanawake wanaotoka familia ya kifukara hawatakiwi kuolewa au? Hii sasa kaliiii woiiiiiih
 
Ko wanawake wanaotoka familia ya kifukara hawatakiwi kuolewa au? Hii sasa kaliiii woiiiiiih
Mbona wanaolewa saana na wanaume wa size zao kiuchumi? Tena hao wanolewa kuliko wale wanaojimudu kiuchumi! Tiamajitiamaji hawana mambo mengi! Unapiga sound asubuhi jioni katia timu geto na kabegi! Mtaenda kujitambulisha baada ya kupata watoto kadhaa! Wakikinukishana wanatimuana kila mtu 50 zake!
 
Ni kweli haya mambo ni kama yanaambukiza hivi, mtu aliyetoka kwenye familia duni huwa kuna vitu vilivyopelekea uduni kama na yeye kavimeza ni ngumu sana kuliachia maana huamini maisha ni bahati na sio kupangiwa, Nidhamu na uwajibikaji, na pia aliyetoka familia iliyopigwa ikawekq mambo vizuri pia huwa na maambukizi ya kujua kwamba mali inatafuta na kutunzwa ili izae,

Kikubwa angalia kana ni mtu anaweza badilika, vinginevyo utazama na kuwa tegemeo la familia yake.
 
Hapa mtaani kuna dada mmoja anafanyakazi mjini (nadhani kariakoo) amejenga nyumba yake. Sasa huyu dada ana msichana wa kazi mzuri anaridhisha sura, umbo, na chura. Umri wake kama miaka 17 kuelekea 18 na anaanza kujitambua. Sasa kuna jamaa (kijana in his late 20s and early 30s) anajiweza yuko vizuri kiasi na kavutiwa na huyo binti kuchukua jiko.

Baada ya kuongea na huyo msichana kutaka kujua ABC kagundua mama yake aliachana na baba yake na hakuwahi kumuona hila anasikia bado yupo. Baba yake ni mvuvi huko kanda ya ziwa. Huyo bosi wake anayemfanyiakazi anadai ni ndugu wa karibu alimchukua kumsaidia kulea mwanae!

Kilichomshitua jamaa ni kuona baba yake analialia kwa mwanae amtumie chochote anachokipata huko mjini kuonyesha kwa jinsi gani choka mbaya.

Sasa akaja kuniomba ushauri kuhusu kuoa binti aliyetoka familia duni kama hiyo hata kama ni mzuri si atakuwa na yeye kajidumbukiza kwenye ufukara?
Nilitaka nipite kimya ila acha nikoment kama ifuatavyo:
Japo sio ndoa zote ila asilimia kubwa ya kuoa binti wa familia maskini tena yule aliyelelewa na mzazi mmoja mama pekee tarajia yafuatayo.
1. Kabebeshwa mzigo wa kila kitu ukweni kuanzia kusomesha wadogo wa mkeo, kuombwa misaada kila siku mbaya zaidi mwanamke anaweza kuforce ajenge nyumba kwao kabla hata hamjajenga kwenu.
2. Kuchapiwa kwa urahisi( mwanamke aliyetoka familia maskini sana huwa haridhiki kwa urahisi akishazoea ndoa ataanza kuchapwa nje ili kujiongezea kipato atume nyumbani kwao tena wengine kupewa ushauri na mama zao kwamba awe anakuibia hata pesa anatuma kwao
3. Kurogwa na kulishwa limbwata( asilimia kubwa ya familia za hivyo ndio wanaongoza kwenda kwa waganga ili kutafuta limbwata mwanaume awe zoba awachukie wazazi na ndugu zake awe anamsikiliza mkewe tu.
4. Lawama zisizoisha (familia maskini zinaongoza kwa lawama yaani hata kama unawapa mahitaji kila siku ikitokea kuna kitu umeshindwa kufanya utasemwa maneno machafu sana na hata mkeo atakununia bila sababu kisa umeshindwa kutuma hela ya marejesho kwa mama yake
5. Kuachwa ghafla siku pesa zikiisha( mara nyingi maskini hawana shukrani na hawakumbuki fadhila Siku umepata tatizo kama ajali, kesi, au kuugua kwa muda mrefu pesa ikaisha hawezi kuvumilia kuishi na wewe atakimbia atafute mwenye pesa.
6. Kama binti alilelewa na mama pekee basi tarajia akikuzoea atakuwa anakupanda kichwani na atataka awe na sauti nyumbani kuliko wewe maana amekua akimwona mama ndiye kiongozi wa familia tena wengine ukikuta mamake ana akili za ajabu hata binti lazima awe hivyo maana mshauri wa kwanza wa binti ni mamake mzazi sasa kama mama mwenyewe ni single hana experience ya ndoa unategemea atamshauri nini binti yake ikitokea changamoto ya ndoa? Zaidi atamshauri waende kwa mganga akuinamishe uwe jinga.
-Kwa kifupi kuoa mwanamke wa familia maskini sana ni kujibebesha mzigo wa matukio mazito huko mbeleni
Ila unaweza kuoa mwanamke maskini iwapo amezaliwa na kulelewa na wazazi wote wawili halafu nyumbani kwao baba ndiye mwenye sauti halafu wawe ni wazazi ambao wanajishughulisha hata kama ni kilimo cha kawaida( hii itamfanya hata binti atakapoolewa awe na nidhamu kwa mumewe na pia ajue kwamba maisha yakiyumba mnaweza hata kulima au kufanya kazi ngumu ili kupata pesa.
Huo ni mtazamo wangu
 
Kila mwanamke ana fungu lake!
Kuoa ni fumbo.
Kuoa ni bahati mbaya na nzuri.
Kuoa ni kuingiza mkono kwenye kapu lenye mdomo mdogo hujui utakuta nini ndani.
Hakuna kanuni ya kuoa vizuri ila kuna viashiria vya kuoa vizuri.
Kuoa ni nyota yako wewe na yule unaemuoa.
Kuoa ni kitendawili, tega utegue.
 
Back
Top Bottom