Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuh uWakuu heshima kwenu.
Habari za jioni, poleni na majukumu (kwa wale wenye majukukumu).
Naomba kufahamishwa KISHERIA kama kichwa cha uzi kimavyojieleza.
Mi hivi, baada ya mgogoro wa ghafla sana (only 2 months now) na vurugu zilizofuata hapo, hatimae mke wangu ame file kesi mahakama ya mwanzo jii ya dai la talaka.
Nimepogiwa simu siku kadhaa zimepita sasa kitaarifiwa pia kitakiwa kuchukua wito "samansi" wa mahakama juu ya kesi husika na kweli nikachukua.
Charges ambazo nimekuta zimeainishwa ni kama 4 hivi ikiwemo
- talaka
- mgawanyo wa mali
- matunzo ya watoto
- kuishi na watoto
Sasa katika maisha yetu tulifanikiwa kijenga nyumba , kuwa na kiwanja pia usafiri ndio angalau kwa uchache vitu vya kueleweka.
Wazo langu mimi ni kwamba, sitaki habar za kugombania kitu na huyu mama ambaye mpaka sasa alishachukua watoto na kwenda kupanga mtaani.
Na mi pia nikaamua kuhamisha harakati zangu mkoani kulingana na nature ya shughul zangu.
Hivyo sina mpango wa kugombania mali wala chochote katika vyote tulivyo navyo.
Moja ya vipengele nimesoma kwenye hii samansi ya mahakama inasema "endapo mdaiwa /mlalamikiwa (mimi yani ) hatafika mahakamani , shauri litasomwa na kusikilizwa upande mmoja bila mimi kuwepo.
Sasa naomba kufahamu, kisheria kama nitaamua KUTOONEKANA mahakamani siku hiyo, je ,nitakua nimetemda UHALIFU ambao unaweza kunigharimu??
Naomba kusaidowa ufafanuzi.
Ahsanten
Hii hadithi inasisimua balaa. Kama najiona mimi tu japo story zetu ni tofauti kidogo sanaUmenikumbusha mbali sana, nilizaa na mwanamke, nikaamua kuishi naye bila kufunga ndoa, (sukutaka kufunga ndoa haraka haraka) nilimtambulisha kwetu na Kwao nilienda kujitambulisha nikaishia hapo.
Miaka kadhaa baadaye nikagundua Ana-date x wake, nikathibitisha pasiposhaka kwamba ameliwa siku tatu mfululizo! (Aliniaga anakwenda kusalimia Msiba wa shangazi yake, kumbe anaenda kuliwa na jamaa yake wa zamani)
Nilimuuliza baada ya kujiridhisha na ushenzi aliofanya, akawa mbogo hataki kuulizwa chochote, nikaamua kufanya maamuzi magumu, nikamwambia NITALEA MTOTO na wewe uendelee na mahusiano yako, akanijibu sheets za maana! Nikalazimika kujizuia kumpiga ili nisiingie kwenye kesi isiyo na ulazima!
Nilipomuacha cha kwanza akakimbilia mahakamani, alipoulizwa anataka nini akasema anataka tugawane mali ili akaendelee na maisha yake, nilipoitwa nilienda, nikawaambia sijawahi kumuoa huyo mwanamke zaidi ya Kazaa naye, hivyo nitawajibika kmtunza mtoto tu.
Alipotakiwa kuthibitisha mimi kuwa mume wake akasema tumeishi pamoja zaidi ya miaka 2, nikwaambia sijawahi kuishi naye kwa hata miezi Sita Kwani nilikuwa nafanya kazi mahali tofauti na palipokuwa na makazi!
Baada ya purukushani nyingi na matusi juu, hatimaye nikapewa jukumu la kutunza mtoto!
Kwa kuwa Ali kuwa jeuri, mtoto alikuwa na miaka 9 nikaiomba mahakama inipe idhini ya kuishi na mtoto, nikakubaliwa!
Ameridi mwaka Jana December, kuniomba msamaha na kutaka turudiane, nikamwambia asithubutu kuniletea ushenzi, nisijeondoka na shingo yake! Anajiliza liza mpaka leo kutaka turudiane!
😂Usipofika, mahakama itatoa uamuzi kama vile ulikuwepo, ukakaa kimya,au ukakubari kila kitu,