Nini msimamo wa TLS kwa wanachama wake kuwatetea wabakaji na walawiti ambao jamii nzima imeona unyama wao?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Mimi siyo mwanasheria, lakini nimeona msimamo wa TLS kulaani tukio la unyama uliofanywa na wabakaji na walawiti na TLS imetowa wito kuhakikisha haki inatendeka.

Sasa napata tabu kidogo kusikia kuna mawakili wanne wanaowatetea hawa washenzi wasiostahili huruma hata chembe.

Mimi ningekuwa wakili hata niwe na njaa kiasi gani siwezi kukubali clients wa aina hii.

Hivyo basi JF ni kubwa natowa wito tupate majina ya mawakili wote wanaowatetea hawa washenzi ili jamii iwajuwe wanaounga mkono ujahili.
 
Mimi siyo mwanasheria, lakini nimeona msimamo wa TLS kulaani tukio la kulaani unyama uliofanywa na wabakaji na walawiti na TKZ imetowa wito kuhakikisha haki inatendeka...
Kulaani tukio la kulaani? Hebu weka vizuri hapo Dr.
 
Mimi siyo mwanasheria, lakini nimeona msimamo wa TLS kulaani tukio la kulaani unyama uliofanywa na wabakaji na walawiti na TKZ imetowa wito kuhakikisha haki inatendeka.

Sasa napata tabu kidogo kusikia kuna mawakili wanne wanaowatetea hawa washenzi wasiostahili huruma hata chembe.

Mimi ningekuwa wakili hata niwe na njaa kiasi gani siwezi kukubali clients wa aina hii.

Hivyo basi JF ni kubwa natowa wito tupate majina ya mawakili wote wanaowatetea hawa washenzi ili jamii iwajuwe wanaounga mkono ujahili.
Mshtakiwa nae ana haki zake.
 
Hata waahitakiwa wa mauwaji hupewa wakili tena bure na serikali, wawatetee. Sheria zina mambo mengi sana. Pengine mmojawapo kafananishwa na sio mhusika wa tukio?
 
Kwanza kumbuka vitu hivi mkuu

1.Presumption of innocence,Kila mtuhumiwa anakuwa presumed hana hatia mpaka itakapokuwa kuwa proved otherwise, na hii ni very important principle thus why imekuwa enshrined mpaka kwenye Katiba yetu.

Pi ukumbuke kwenye Sheria za jinai hakuna kitu muhimu kama due process of law,huwezi kuzuka tu huko kusema huyu mtu afungwe,lazima ufuate taratibu na standard of proof ni beyond reasonable doubt thus why kwa sisi wenye mahaba na haki jinai wakati mwingine unatokea mtuhumiwa amefanya kweli kosa lakini labda mwendesha mashtaka Kuna kitu kajisahau unakazia hapo hapo kwenye technicality na mtu anaachiwa.

Mfano Kuna kesi nyingi tu mwezi huu Mahakama ya Rufani imewamwaga watuhumiwa just tu kwa sababu certificate of consent ya DPP haikuwa proper

2 .Kwenye ethics za mawakili Kuna kitu wanaita "Rule against discrimination" ambayo Wanasheria wanapenda kuiita kwa kizungu "Cab Rank Rule" hutakiwi kumnyima huduma mteja as long as ishu aliyoileta ipo katika eneo lako la practice,ko ukikataa kesi yake Ina maana ume mdiscriminate mtuhumiwa.

Lakini pia tusisahau kuwa Kila mtu ana haki ya kuwa represented kama haki hiyo ilivyotolewa na KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai

Hivyo mawakili wapo sahihi kabisa kuwawakilisha wateja wao (Usiwaite wabakaji mpaka mahakama tukufu itakaposema hivyo)
 
Haha Matola punguza, nao wana haki ya kuwa na wakili.

Nadhani huu ni mfano rahisi kwa hawa kunguni wengine wajue kuwa hata yule “malaya mwenzetu” ana haki zake kama binadamu.
 
Kwanza kumbuka vitu hivi mkuu

1.Presumption of innocence,Kila mtuhumiwa anakuwa presumed hana hatia mpaka itakapokuwa kuwa proved otherwise, na hii ni very important principle thus why imekuwa enshrined mpaka kwenye Katiba yetu.

Pi ukumbuke kwenye Sheria za jinai hakuna kitu muhimu kama due process of law,huwezi kuzuka tu huko kusema huyu mtu afungwe,lazima ufuate taratibu na standard of proof ni beyond reasonable doubt thus why kwa sisi wenye mahaba na haki jinai wakati mwingine unatokea mtuhumiwa amefanya kweli kosa lakini labda mwendesha mashtaka Kuna kitu kajisahau unakazia hapo hapo kwenye technicality na mtu anaachiwa.

Mfano Kuna kesi nyingi tu mwezi huu Mahakama ya Rufani imewamwaga watuhumiwa just tu kwa sababu certificate of consent ya DPP haikuwa proper

2 .Kwenye ethics za mawakili Kuna kitu wanaita "Rule against discrimination" ambayo Wanasheria wanapenda kuiita kwa kizungu "Cab Rank Rule" hutakiwi kumnyima huduma mteja as long as ishu aliyoileta ipo katika eneo lako la practice,ko ukikataa kesi yake Ina maana ume mdiscriminate mtuhumiwa.

Lakini pia tusisahau kuwa Kila mtu ana haki ya kuwa represented kama haki hiyo ilivyotolewa na KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai

Hivyo mawakili wapo sahihi kabisa kuwawakilisha wateja wao (Usiwaite wabakaji mpaka mahakama tukufu itakaposema hivyo)
Umeimaliza msomi
 
Back
Top Bottom