Kwanza kumbuka vitu hivi mkuu
1.Presumption of innocence,Kila mtuhumiwa anakuwa presumed hana hatia mpaka itakapokuwa kuwa proved otherwise, na hii ni very important principle thus why imekuwa enshrined mpaka kwenye Katiba yetu.
Pi ukumbuke kwenye Sheria za jinai hakuna kitu muhimu kama due process of law,huwezi kuzuka tu huko kusema huyu mtu afungwe,lazima ufuate taratibu na standard of proof ni beyond reasonable doubt thus why kwa sisi wenye mahaba na haki jinai wakati mwingine unatokea mtuhumiwa amefanya kweli kosa lakini labda mwendesha mashtaka Kuna kitu kajisahau unakazia hapo hapo kwenye technicality na mtu anaachiwa.
Mfano Kuna kesi nyingi tu mwezi huu Mahakama ya Rufani imewamwaga watuhumiwa just tu kwa sababu certificate of consent ya DPP haikuwa proper
2 .Kwenye ethics za mawakili Kuna kitu wanaita "Rule against discrimination" ambayo Wanasheria wanapenda kuiita kwa kizungu "Cab Rank Rule" hutakiwi kumnyima huduma mteja as long as ishu aliyoileta ipo katika eneo lako la practice,ko ukikataa kesi yake Ina maana ume mdiscriminate mtuhumiwa.
Lakini pia tusisahau kuwa Kila mtu ana haki ya kuwa represented kama haki hiyo ilivyotolewa na KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai
Hivyo mawakili wapo sahihi kabisa kuwawakilisha wateja wao (Usiwaite wabakaji mpaka mahakama tukufu itakaposema hivyo)