Nini msimamo wa TLS kwa wanachama wake kuwatetea wabakaji na walawiti ambao jamii nzima imeona unyama wao?

I tells the stoty which is wrongly perceived. Kwamb watu wa system they can get away with any criminality they do. Sisi tulikuwa Darful nani anatuambiaje?
 
Kila mtu awe mhalifu au la, ana haki ya utetezi wa kisheria. TLS haitapinga watuhumiwa kupata utetezi.
 
Mkuu mshitakiwa yeyote anayo haki ya kupata utetezi wa kisheria ( Wakili)
 
Ni haki ya kikatiba na kibinadamu kwa kila mtuhumiwa kupata utetezi na wakiki mahakamani.

Bila kujali mtuhumiwa ana makosa au hana makosa.

Hii ni kwa sababu, hata mtuhumiwa aliyefanya makosa anatakiwa achukuliwe kama hana makosa mpaka mahakama itakapompata na makosa.

Lakini pia, mtuhumiwa mwenye makosa asipewe nafasi ya kulalamika kwamba amepatikana na makosa kwa sababu hakupewa nafasi ya kutetewa na wakili.

Kuna Mmarekani mmoja alimtetea Saddam Hussein katika kesi ya Saddam na Wamarekani, akasema kuwa anajisikia raha sana kumtetea Saddam, kwa sababu hilo linaonesha kuwa mfumo wa haki wa Kimarekani unampa utetezi hata mtu muovu kabisa.

Kutetewa mahakamani ni haki ya kikatiba na kibinadamu.

Mimi nafurahi sana watuhumiwa wanapewa utetezi, wakipatikana na hatia kusiweze kuwepo malalamiko kwamba wamepatikana na hatia kwa kunyimwa mawakili wa kuwatetea.

Mwabukusi anaelewa haki hizi za kikatiba na kibinadamu, ndiyo maana haoni tatizo kulaani ubakaji, halafu mawakili walio wanachama wa TLS kutetea watuhumiwa wa ubakaji.

Kwa elimu yake na uongozi wake wa TLS, anatakiwa kuona tatizo ikiwa watuhumiwa wa ubakaji wanashitakiwa bila ya kuwa na mawakili wa kuwatetea. Hilo jambo ndilo lingekuwa scandal.

Watuhumiwa kukosa mawakili wa kuwatetea ndiyo scandal, si watuhumiwa kuwa na mawakili.
 
Ni Hali Yao kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.
 
Sheria ngumu sana joh,washitakiwa nao wanahaki zao moja wapo ndo hiyo yakuwa nawakili wakumtetea haijalishi nikesi yanamna gani
Pamoja na kumbaka binti kwa zamu hadi akaomba maji bado wahuni hawa wa haki ya kutetewa.

Huu ndio mfumo wa Dunia yetu iliyostaarabika.
 
Tuna mahakama zetu za kitaa, ndio maana kitaa tunachoma moto hatuhitaji usanii wa mawakili.
Wish hizi mahakama za kitaa zingekuwa smart sana na ku handle ishu kubwa kubwa.mfano: Watu kutekwa na kunyimwa haki ya kuishi, fulani kaingiziwa chupa, fulani sijui kafanya mkataba ya ovyo, watu kutumia madaraka vibaya etc.

Ukipata muda ukiwa na mahakimu wengine wa kitaaa waeleze na hayo tunayataka, nchi ingekuwa salama sanaaaa.
 
Sheria haina kona kona, imenyookaa.
Ni haki yao kuwa na mawakili wa utetezi.
 
hapa mie ndio napowapendea taliban, wala tusingefika huko kote. wangekuwa six feet under zamaniiii
 
Duuuu elimu ya bongo bwana hivi hata huyu naye ana Phd
 
Reactions: FWC
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…