BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mkuu heshima yako.
Mimi bado naamini jukumu la kurekebisha hayo yote ni jukumu letu sote si jukumu la serikali tu.
Pia kujituma,ubunifu kama ulivyo nena ndiyo siri ya mafanikio mtu akiamuwa kujituma bongo kama anavyojituma kubeba ma box kwa kulala saa mbili masaa 22 yuko kazini basi Hakuna sehemu yoyote atakayopata mafanikio makubwa tofauti na Tanzania.
Basi hakuna haja ya kuwa na serikali ambayo inaangalia ni mambo gani ambayo yana kero kubwa kwa wananchi na kuyafanyia kazi mambo hayo ili kupunguza kero hizo au kuzimaliza kabisa.
Hatuwezi wote kuwa wabunge au mawaziri bali tunachoweza kufanya ni kufikisha malalamiko yetu kwa wawakilishi wetu bungeni ili kero zetu zipunguzwe au kumalizwa kabisa. Hili Watanzania tunafanya miaka nenda miaka rudi bila mafanikio yoyote.
Wengine wameshasema nyumbani ni pale ambapo mkono unaenda kinywani. Siyo Watanzania wote walio nje wanabeba box, wengine wana mafanikio ya hali ya juu na kamwe hawawezi kuyapata mafanikio hayo Tanzania. Wakitaka kurudi watarudi na kama wanaona kurudi hakulipi basi ni hiari yao mradi hawavunji sheria za nchi.