Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani?

Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani?

Mkuu heshima yako.
Mimi bado naamini jukumu la kurekebisha hayo yote ni jukumu letu sote si jukumu la serikali tu.

Pia kujituma,ubunifu kama ulivyo nena ndiyo siri ya mafanikio mtu akiamuwa kujituma bongo kama anavyojituma kubeba ma box kwa kulala saa mbili masaa 22 yuko kazini basi Hakuna sehemu yoyote atakayopata mafanikio makubwa tofauti na Tanzania.

Basi hakuna haja ya kuwa na serikali ambayo inaangalia ni mambo gani ambayo yana kero kubwa kwa wananchi na kuyafanyia kazi mambo hayo ili kupunguza kero hizo au kuzimaliza kabisa.

Hatuwezi wote kuwa wabunge au mawaziri bali tunachoweza kufanya ni kufikisha malalamiko yetu kwa wawakilishi wetu bungeni ili kero zetu zipunguzwe au kumalizwa kabisa. Hili Watanzania tunafanya miaka nenda miaka rudi bila mafanikio yoyote.

Wengine wameshasema nyumbani ni pale ambapo mkono unaenda kinywani. Siyo Watanzania wote walio nje wanabeba box, wengine wana mafanikio ya hali ya juu na kamwe hawawezi kuyapata mafanikio hayo Tanzania. Wakitaka kurudi watarudi na kama wanaona kurudi hakulipi basi ni hiari yao mradi hawavunji sheria za nchi.
 
Ligi ya kitu gani?..mtu ameanzisha thread kuhusu kinachomsibu yeye na watu wengine , wewe unaanza kutuwekea stds za kuchangia, eti ooh kama upo ughaibuni bado hujarudi bandiko halikuhusu, mleta thread amekuajiri uusemee moyo wake?.. Kati ya wewe na mimi nani anayetaka ligi sasa? Ya Ukumbi wa deen unaingiaje hapa?

Hatimaye Kibunango amepata mahali pale .Kibunango kubali mkuki uingie maana umeangukia makali sasa wacha mkuki upenye kaka heheheheh
 
Mkuu hapo ndipo tunakuja kwenye swala lile lile la connection.Hayo mawazo yako ni mazuri lakini je ni nani atakayekupa hiyo nafasi?Unazungumza kwenda na mtaji wako siyo lazima halafu una mawazo wa kulichukua shirika mfu la ATC,sasa utalifufuaje bila kuwa na mtaji?

Heshima mbele Mkuu, nimeongelea in larger picturer kuhusu mifano niliyotoa, not necessarily urudi kuendesha ATC, [ by the way kuna watu humu ndani i am sure wana better ideas kuhusu shirika hili ] nitatoa mfano wa kurudi na kuwa Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi huko Msovero ambayo haina vyoo, je ni lazima nirudi na mtaji kusaidia watoto hao wasijisaidie porini? Si ninaweza kurudi na wazo jipya kuliko kufanya kazi kwa mazoea ? Mfano kufanya mkutano na wazazi, labda kuna wazazi fundi wajenzi, kuna wazazi mafundi waashi, kuna wazazi mafundi bomba na pia labda mafundi umeme, hawa ukiwa-organise ni one week tu watoto wana vyoo, tena vya kisasa. Lakini ni aibu kuna shule ilipata msaada wa ujenzi wa choo toka kwa balozi wa Japan !!! come on now..., in 21st century ?? miaka 47 baada ya uhuru ? Ni vitu vya namna hii ndivyo ninavyoongelea.
Hapo swali nitakaoloulizwa ni kwamba je kama ni hivyo tu, mbona siyo lazima mtu atoke nje ili kujenga vyoo ? Na mimi nitajibu , sawa siyo lazima atoke nje, lakini mbona watoto wanajisaidia porini, wakiumwa na nyoka jee???
Japan iliendelea ghafla at the turn of the century kwa sababu ilipeleka sana watu nje ya nchi , especially in the western world, kujifunza na baadaye kurudi nyumbani, walichofanya ni kuweka mazingira mazuri ya watu hawa kutumia ujuzi wao waliotumwa kufuata nje KWA MANUFAA YA WOTE, [for the common good]
 
Nakuelewa mkubwa.
Unajuwa ni heri ukasote uswahilini kuliko kusota ukraine ama urusi teh teh teh teh.

Mkuu hata hivyo swali la mhusika nadhani limelenga zaidi ktk mtu mwenye nafasi huko aliko ama arudi nyumbani.Na ndiyo maana ktk maelezo yangu ya awali sijasema mtu arudi nimesisitiza ya kwamba kama ulipo bila kujali upo tz ama nje una uwezo wakutengenezea nafasi watanzania wezako ni swala la busara zaidi kubakia hapo ulipo.

Nakama uko huko juu ya mawe ni bora urudi bongo,bado naamini ukiwa na masters nzuri sio ya kuingia darasani mara mbili kwa week huko uliko tz kazi bado zipo.

MkamaP
Kama nime mwelewa mtoa mada ni kwamba ni nini uzoefu baada ya kuhamasishwa na wakubwa turudi nyumbani na sasa kweli tumerudi .Je yale waliyo tueleza yapo kweli ama ni siasa zao za kujikosha tu wakija huko Ulaya ?

Mimi nasema niko Tanzania wasemayo huko si kweli kabisa ni kujikosha na hakuna equal opportunities hata mara moja .Ukiwa umesoma nje wewe ni adui yao mkubwa kabisa .Wachache nawajua wamekaa Ulaya na hata hawakusoma wala nini leo wana nafasi kubwa kwa kuwa wana wakubwa ndani ya CCM .Mie nasema CCM kwa kuwa naongea wanasema ilikuwaje.Walikuwa hapa JF wanalia kila siku na kubonda lakini baada ya kulambishwa leo namuuliza vipi bwana mbona sikuoni JF ? Anasema njaa yangu imeisha mzee wacha nitese .
 
Basi hakuna haja ya kuwa na serikali ambayo inaangalia ni mambo gani ambayo yana kero kubwa kwa wananchi na kuyafanyia kazi mambo hayo ili kupunguza kero hizo au kuzimaliza kabisa.

Hatuwezi wote kuwa wabunge au mawaziri bali tunachoweza kufanya ni kufikisha malalamiko yetu kwa wawakilishi wetu bungeni ili kero zetu zipunguzwe au kumalizwa kabisa. Hili Watanzania tunafanya miaka nenda miaka rudi bila mafanikio yoyote.

Wengine wameshasema nyumbani ni pale ambapo mkono unaenda kinywani. Siyo Watanzania wote walio nje wanabeba box, wengine wana mafanikio ya hali ya juu na kamwe hawawezi kuyapata mafanikio hayo Tanzania. Wakitaka kurudi watarudi na kama wanaona kurudi hakulipi basi ni hiari yao mradi hawavunji sheria za nchi.

Mkuu
tupo pamoja kabisa hata mimi ndiyo maono yangu kwamba kwa mtanzania mwenye mafanikio huko aliko aendelee kuwa huko ila mafanikio yake ya huko ayatumie kuwawezesha watanzania walio nyumbani kwa njisi hiyo maendeleo yatapatikana.

Ila kwa yule ambaye hana kitu huko aliko ni bora alirudi nyumbani maana huko Tanzania kuna fursa nyingi kama unavijisenti kadhaa .
 
MkamaP
Kama nime mwelewa mtoa mada ni kwamba ni nini uzoefu baada ya kuhamasishwa na wakubwa turudi nyumbani na sasa kweli tumerudi .Je yale waliyo tueleza yapo kweli ama ni siasa zao za kujikosha tu wakija huko Ulaya ?

Mimi nasema niko Tanzania wasemayo huko si kweli kabisa ni kujikosha na hakuna equal opportunities hata mara moja .Ukiwa umesoma nje wewe ni adui yao mkubwa kabisa .Wachache nawajua wamekaa Ulaya na hata hawakusoma wala nini leo wana nafasi kubwa kwa kuwa wana wakubwa ndani ya CCM .Mie nasema CCM kwa kuwa naongea wanasema ilikuwaje.Walikuwa hapa JF wanalia kila siku na kubonda lakini baada ya kulambishwa leo namuuliza vipi bwana mbona sikuoni JF ? Anasema njaa yangu imeisha mzee wacha nitese .

Mkuu wangu
hilo ni kweli unaloongea na hata hivyo wanasiasa wengi uongo ndiyo miongozo yao ,lakini hatuwezi kukatishwa tamaa na kuliacha Taifa linadidimia lazima sisi kama wananchi tufanye hima tulikomboe taifa letu.

Mfano kuna watanzania wapo wana nafasi nzuri na fedha za kutosha tu nafikiri tukijiorganize tukachanga ama kutafuta wafadhili na tukanunua majenerata pale Ruvu ya kusukuma maji DAR serikali wataona aibu wanaweza wasi react hapohapo lakini itawapain.

Mfano watanzania walio na fursa wanaweza tafuta mdhamini ama tukachanga na kujenga pale mwanza chuo kikuu cha kisasa kitakachotoa ushindani kwa udsm.
kwa hiyo kwa kujitolea hivyo moyo wa kizalendo, taratibu hata serikali inasumakishwa huo moyo wa kizalendo na ndani ya miaka michache kabisa tanzania yenye neema inapatikana.

Dawa ya Mkorofi si kugombana naye maana hapo atakuwa mkorofi zaidi na utampa nafasi ya kugudua ukorofi ulio advance badala yake ni kumuunyesha matendo mema naye taratibu atajikuta anafanya mema.

Mfano mtu akikutukana ukamwambia asante atafadhaika sana roho na kujiona mjinga tofauti na wewe ukijibu kwa kutukanana.

Hivyo hawo jamaa wanaokuwa adui kwa wasomi wenzao ni ka ugnoransi tu ambako kanasumbua ili ukaondoe ni lazima ukae naye umuonyeshe ulivyo mwelevu sasa na wewe ukiamuwa kumuonyesha ka uignoransi ka kutorudi nyumbani basi utampa huyu nafasi ya kutafuta kiugnoransi kangine kalikokwenda shule.

Kheri ya mwaka mpya.
 
Heshima mbele Mkuu, nimeongelea in larger picturer kuhusu mifano niliyotoa, not necessarily urudi kuendesha ATC, [ by the way kuna watu humu ndani i am sure wana better ideas kuhusu shirika hili ] nitatoa mfano wa kurudi na kuwa Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi huko Msovero ambayo haina vyoo, je ni lazima nirudi na mtaji kusaidia watoto hao wasijisaidie porini? Si ninaweza kurudi na wazo jipya kuliko kufanya kazi kwa mazoea ? Mfano kufanya mkutano na wazazi, labda kuna wazazi fundi wajenzi, kuna wazazi mafundi waashi, kuna wazazi mafundi bomba na pia labda mafundi umeme, hawa ukiwa-organise ni one week tu watoto wana vyoo, tena vya kisasa. Lakini ni aibu kuna shule ilipata msaada wa ujenzi wa choo toka kwa balozi wa Japan !!! come on now..., in 21st century ?? miaka 47 baada ya uhuru ? Ni vitu vya namna hii ndivyo ninavyoongelea.
Hapo swali nitakaoloulizwa ni kwamba je kama ni hivyo tu, mbona siyo lazima mtu atoke nje ili kujenga vyoo ? Na mimi nitajibu , sawa siyo lazima atoke nje, lakini mbona watoto wanajisaidia porini, wakiumwa na nyoka jee???
Japan iliendelea ghafla at the turn of the century kwa sababu ilipeleka sana watu nje ya nchi , especially in the western world, kujifunza na baadaye kurudi nyumbani, walichofanya ni kuweka mazingira mazuri ya watu hawa kutumia ujuzi wao waliotumwa kufuata nje KWA MANUFAA YA WOTE, [for the common good]

Labda mimi sikuelewi mkuu.Yaani una maana let say unatoka zako kiwanja na Masters yako safi ya engineering eti kisa kwa vile huna mukulu kwenye system basi uende ukajipachike kwenye ualimu halafu upewe ualimu mkuu kisha uanze kutumia utundu wako na uzoefu wako wa nje kufanya mikutano na wazazi na kuwa organise mjenge vyoo?Ndiyo uzalendo huo mkuu wa kwenda kulipwa laki mbili tena kwa mbinde?
Kama ndiyo hivyo mkuu bora nigangamale na box huku nikiwa push jamaa home na kwavile nina nondo tayari basi siku bepari anaweza kunipachika kwenye kibarua cha ujuzi wangu kuliko kwenda kuichezea IT yangu kuwahimizia wanakijiji wajenge vyoo!
 
Mukulu Mtarajiwa,

Ni kweli muzee, ktk situation hizi za kuingizana mkenge wa 'uzalendo' ni bora uendelee kukamata box. Ningekuwa mimi nimekamata chance ya kubeba boks, sirejei ng'o. Sintorejea kwa sababu najua what is at stake. Kila mtu hapa anajua anatokea ktk familia ya namna gani. Wengine hali ni mbaya mno, kwa hiyo hizi ngonjera za 'uzalendo' mtatusamehe sana wakulu.
 
Mara nyingi sana tunasikia viongozi wetu wakiwa wanazungumza na Watanzania nje ya nchi, Botswana, Afrika Kusini, Canada, UK na kwingineko wanashauri sana vijana warudi nyumbani kusaidia juhudi za kujenga Taifa.
Lakini mimi binafsi nimesikia tofauti kidogo kutoka kwa ndugu na jamaa waliofuata ushauri huu. Kwamba fursa hiyo ya kujenga taifa baada ya kurudi hawaipati !!!! Ndugu mmoja alisoma mambo ya computer nje na kufanya kazi hiyo kwa miaka 7 nje. [ ni mtaalamu wa kutisha wa IT } Akaamua kurudi nyumbani kusukuma gurudumu la maendeleo kama wakubwa walivyosihi, lakini baada ya muda alirudi tena na kusema ameshindwa kufanya kazi nyumbani na kwamba atarudi baada ya kustaafu !!
Mwingine alisoma mambo ya masoko, akapata kazi shirika la umma, lakini bosi wake alimnyanyapaa sana. Jamaa akitoa mawazo mapya bosi anasema anataka kumnyang'anya kazi au anafanya kazi kwa sifa. Sasa yeye hana uwezo wa kurudi nje alikokuwa. Inabidi awe hapohapo huku manung'uniko hayaishi. Na kutusihi sisi " jamani msirudi".
Jamaa mwingine akaniambia kama siku hizi nina lafudhi ya Ki-Kenya basi nirudi nyumbani !!!Maana hao ndio wana kazi zote nzuri.
Tupatie experience yako baada ya kurudi.

Kwame,

Mimi sijarudi ila nina kauzoefu kidogo na wanachosema hawa waheshimiwa wakiwa nje na ukweli kule nyumbani. Njia ninayotumia mimi ni kwamba tanguliza mguu mmoja kwanza ili kama kuna madhara basi yasikudhuru mwili mzima.

Ukitaka kurudi nyumbani isiwe kwa kufuata wanachosema wanasiasa. Wanachosema kiwe challenge ya kukufanya uchunguze zaidi na kuangalia unawezaje kufaidika na opportunities zilizoko nyumbani.

Wanasiasa karibu wote wanadanganya, wanalipwa kwa kusema uongo huo. Wanasiasa hao hao ukifika bongo huwezi hata kupata nafasi ya dakika tano kuongea naye. Wakiwa Tanzania ni bidhaa adimu.

Kwa watu waliobobea kwenye nyanja zao, muhimu iwe kuwa na uwezo wa kujiajiri na kuendesha shughuli zako. Ukienda serikalini kwa lengo la kuleta mabadiliko, utakorofishana na watu wengi sana. Ushauri wangu ni kwamba hata ukiamua kwenda serikalini, ficha makucha yako kwanza mpaka umesimama imara. Kwa mtu mwenye ujuzi na change management ni kwamba lazima usome uwanja wa mapambano ukoje, kama huna chance ya kushinda ni bora usianzishe change.

Lingine ambalo wanasiasa huwa hawasemi lakini ni ukweli, huenda unaweza kuisaidia Tanzania zaidi huko uliko kuliko ukiamua kwenda kuwa mla rushwa Tanzania au mpiga stori kwenye vijiwe. Sina maana watendaji wote ni wala rushwa ila kama unataka kuleta mabadiliko ukiwa ndani ya system lazima ujiandae kwa mapambano ikiwa ni pamoja na kuumia. Kama huna uwezo huo, basi huenda ni bora huko uliko kuliko kule nyumbani.

Mwisho, nyumbani ni nyumbani, mwenda kwao sio mtoro, kwa shida au kwa raha, wote huwa tunarejea tulikotoka. Panga vizuri kabla ya kurudi, utapokewa kwa shangwe na ndugu na marafiki wakati dola zako hazijaisha, zikissha wataanza kujikata mmoja mmoja. Njia ya kuwajua ni kufilisika ukifika airport ili wote wakukimbie baada ya muda fuata visenti vyako na kuvitumia kwa mambo ya maana.
 
Mukulu Mtarajiwa,

Ni kweli muzee, ktk situation hizi za kuingizana mkenge wa 'uzalendo' ni bora uendelee kukamata box. Ningekuwa mimi nimekamata chance ya kubeba boks, sirejei ng'o. Sintorejea kwa sababu najua what is at stake. Kila mtu hapa anajua anatokea ktk familia ya namna gani. Wengine hali ni mbaya mno, kwa hiyo hizi ngonjera za 'uzalendo' mtatusamehe sana wakulu.

Uzalendo mkuu
Uzalendo ni kitu cha mhimu na cha kwanza ktk ujengaji wa taifa.Mkuu uzalendo hauonyeshi kwa kurudi nyumbani tu bali huko uliko kama una nafasi na vijisenti tuvitumie hivyo kusaidia ndugu zetu walioko tanzania kielimu na ku create kazi kama inawezekana watu watakapoelimika na wakapata maisha bora kidogo UFISADI utakufa wenyewe.

Kwa hiyo kama hapo ulipo una nafasi bakia hapohapo lakini ukumbuke kule nyumbani na kama hapo huna kitu kwanini uendelee kuteseka na baridi na kukimbazana na polisi?
 
Acha maneno wewe! Kama huna walau $50,000, kibanda/vibanda vyenye akili, na godfather au washkaji wa kukushika mkono kukuelekeza njia mjini basi usirushe mguu bongo!!! Hiyo "walau 50,000" itakusaidia if and only if una akili ya biashara...vinginevyo uwe fisadi au mmoja ya watoto wao, ama sivyo utajuta kuzaliwa na nyoro itakutoka!!.

Watu wengi "washkaji" ninao wajua mimi waliorudi bongo, kwanza, wengi wao ni 'vilaza' kiasi kwamba wameshindwa ku-compete hapa hivyo wanarudi home ambako kwa mawazo yao wanaweza kupata mambo mazuri juu ya elimu yao ya ughahibuni. Pili, jamaa wengi ni wazushi, aidha ni mashabiki wa ufisadi (wanapenda kona kona, dhulmati na wezi) au wana ndugu zao ambao ni mafisadi na wanakuwa wameshapewa michongo.

Usifuate mkumbo wa kurudi bongo kichwa kichwa.........utaumbuka!!

No comment
 
Hii hoja ndio haswa sababu iliyonisukuma kusema kuwa mtu kama upo ughaibuni na upo serious na career yako, unakamata hata kama ni bingo mbuzi..haitakaa vizuri ukirudi bongo. Utaratibu wa ajira bongo ni kujuana na kazi zinazolipa kufuatana na ukali wa maisha ni za kuhesabika..wengi wanaishi kwa madeni tu...
mwenye macho na some na mwenye masikio na asikie......mkitaka kufa mapema njooni
 
Wanabodi,

Mimi nimerudi Bongo mara kadhaa na kujaribu kuangalia hali halisi kabla sijafikia maamuzi ya kurudi moja kwa moja lakini kusema kweli Bongo INATISHA...
Sasa nitazungumzia tu experience yangu na pengine kuongezea machache ambayo pia nimeyaona..
Ni makosa makubwa kuondoka Ulaya ukitegemea ajira na pengine nitawashauri wasomi wetu kitu kimoja kwamba unaposoma shule hiyo lengo lako liwe kuwa Mwajiri yaani kwa kiswahili safi TAJIRI...nikiwa na maana nje ya neno RICH isipokuwa mwenye KUTOA AJIRA..
Somo hili ndilo litangulie akilini mwako kwa sababu kama nilivyosema huko mwanzo muhimu sana kutazama WATU na MAZINGIRA kabla hujafikia maamuzi muhimu..Hivyo kwa sababu Tanzania bado ni dunia ya tatu, elimu ya watu wengi ni duchu na ewekeshaji ktk sekta ya ajira ni ndogo sana kiasi kwamba unemployment ni zaidi ya asilimia 50, Taasisi za kutoa huduma na biashara bado ni chache sawa na wilaya moja ya nchi za Ulaya.. bajeti ya nchi nzima ni sawa na bajeti na kitongoji cha mji wa Ulaya wakati Population yetu inashindana sawa na nchi za Ulaya...Tofauti zote hizi za watu na mazingira ndizo zinazoifanya Tanzania kuwa tofauti.
Isipokuwa kitu kimoja tupo pamoja ni kwamba, elimu siku zote ni muhimu sana na huchukua nafasi kubwa ya ufanisi ktk innovation, of which is the key to success..

Sasa unapokwenda Bongo na elimu yako ukifikiria unaweza kubadilisha mwenendo wa taratibu za huduma na biashara nchini kama Ulaya wakuu zangu utadunda na utaonekana unachekesha..Na kibaya zaidi utashindwa hivyo elimu yako itakuwa bure kwa sababu hukuzingatia watu na mazingira mapya ya Tanzania ambyo kinadharia ulitaka kuibadilisha iwe kama Ulaya.

Kwa hiyo kitu cha kwanza unachotakiwa kuingia nacho Tanzania ni idea ya kui nvest na hiyo elimu yako ndio the right key (tool) leading to innovation..wala usitegemee mtaji toka kwa tajiri fulani pale bongo..Utadunda sana sana utaibiwa idea yako na itafanyiwa marekebisho kibongo bongo (watu na Mazingira) kwa sababu Imani kubwa ya biashara na mafaniko Bongo inategemea na muda wa returns za kile unachojaribu ku invest... Hakuna tajiri (rich) ambaye anataka kusubiri matunda ya Uwekeshaji wake miezi sita au mwaka mzima.. Biashara ya nyumbani ni papo kwa hapo yaani idea yako lazima iwe na short term returns, mtaji uliowekeshwa utarudi within few months.

Kikwazo kingine ni Ukiritimba..kwa yule anayetafuta ajira au ku invest ni lazima awe na Mtandao, kama alivyosema FMES kwamba viongozi wetu ni reflection yetu ndivyo maisha ya kila siku navyoendesha..Tusitake sana kuzungumzia Mtandano ndani ya chama tawala CCM, lakini ukweli ni kwamba mtandao upo kila sehemu, siwezi kuamini kwamba vyama vya Upinzani havina makundi ya Mtandao ndani yake nitakuwa najidanganya kwani kama kungekuwa hakuna mtandao basi vyama pinzani vingeweza kuungana. Hakuna sababu ya kutooungana zaidi ya watu kuwa ktk makundi tofauti ya vijiwe...
Pia ukitembelea vitongoji mijini kila eneo lina kijiwe chake na wanachama wa kijiwe hicho..na laa ajabu ni kwamba vijiwe hivi vimejenga hata chuki baina yao out of nothing maadam tu kijiwe cha Kinondoni hakiwezi kula sahani moja na kijiwe cha Magomeni, Temeke, Kariakoo, Sinza na kadhalika..kisha within vitongoji hivyo kuna sub groups ambazo pia haziwezi kupatana hata kama lengo la vijewe hivi ni kuzungumzia matatizo sawa na kundi jingine...
Athari za Ukiritimba zimeingia hadi sehemu za uwekeshaji, hivyo ukiwa na idea, elimu na nondo zote za uwekeshaji toka nje isikupe guarantee kwamba utafanikiwa kwani imani kubwa ya ujenzi wa nchi yetu Tanzania leo hii ni kwamba - FEDHA ndio msingi wa Maendeleo..
Tatu, ni muhimu sana kwa vijana wetu mnaporudi nyumbani kufahamu kwamba Tanzania kama nchi na watu wake inatazama vitu kwa darubini tofauti kabisa..Kwa mfano ukifikira kuwa Kazi ndio kipimo cha Utu wao wanaweza kuamini kwamba - Utu ndio kipimo cha kazi..jambo ambalo linaweza kuwa na results tofauti kabisa..

Nne, Ni lazima ufahamu kwamba Tanzania sawa na nchi zote maskini - Cheo sio dhamana isipokuwa ni Title inayomwezesha mtu kuwa Mungu Mtu ktk sekta aliyokabidhiwa madaraka..kuondolewa madarakani mara nyingi hutafsirika kama mapinduzi ambayo yametokana na chuki na wivu.. hakuna kiongozi hata mmoja anakubali accountability kwa sababu moja - Accountability sio Utamaduni wetu...
Wananchi au kwa lugha nyepesi wateja ndio wanatakiwa kuwa accountable, ni wao wenye shida na maskini hivyo ni jukumu lao kufanya kazi, kuomba, kusubiri na kunyenyekea na kadhalika.. Accountability ni hoja inayotazama mteja ama mwananchi sio kiongozi kwani kwa desturi zetu kiongozi ni Nyapala ambaye husimamia watumwa kufanya kazi kwa ufanisi akilipwa pango kubwa la ile title ya Unyapala. Ni urithi tulioachiwa na mkoloni hivyo leo hii Nyapala atapimwa ufanyaji kazi wake kwa utu anaotumia yeye yaani yule Nyapala poa kabisa!

Kwa hiyo tusishangae kuona Mwanakijiji anapotaka kuongea na waziri mkuu kuhusiana na hali mbaya ya wanafunzi Russia anakujibu - Anakula piga simu baadaye..na hiyo baadaye Mwanakijiji asimpate tena waziri zaidi ya kutamiwa makachero wamtafute huyu Mwanakijiji ni nani!..
Tano na mwisho - ni Ufisadi, huu sina hata la kuongea zaidi ya kusema elimu yako itakuwa na manufaa tu kama inaweza kutumika ktk Ufisadi.. Hiyo ndio elimu inayotakiwa Tanzania, elimu ya kobomoa na sio ya kujenga.

Kwa mtaji huo ndugu zangu kulingana na WATU na MAZINGIRA nimejifunza mengi ambayo inabidi kuyafanyia darasa jipya..Lakini wakati huo huo JK ameweza kufungua baadhi ya ajira nchini pamoja na kwamba ameshindwa kuondoa Ukiritimba, kusimamisha Accountability na kuhakikisha Ufisadi hauna nafasi...
Kwa mara ya kwanza nimeona traffic ya vijana inarudi nyumbani. Wakati wa Mwinyi na hasa Mkapa, tulishudia vijana wengi sana wakiondoka nchini kwenda tafuta Elimu nje..Aidha ilikuwa shida kupata elimu nchini au kwa sababu Mkapa alirudisha hadhi ya elimu ktk kipimo cha ajira...
Kutokana na vijana kurudi nyumbani kwa kasi kubwa inanipa moyo kwamba madirisha yamefunguka kama sio milango kuwa wazi..meaning Opportunities zipo!..
 
.....huyo ni story mingi tu za kuhadithiwa vijiweni!

Uzalendo kitu mhimu,kama una nafasi hapo ulipo kurudi hakutokusaidia unless unaenda kuajiri kama wadau walivyobainisha.

Na sisi lazima tuwe na malengo ya mda mfupi na mda mrefu cha kujiuliza sawa saizi na beba mabox tena kwa kutumia triki ya kwamba ni mwanafunzi kwa kujiandikisha ktk shule fulani je hii triki itaendelea mpaka lini? na je nguvu hizi za kubeba mzigo zitaendelea hadi lini?
 
Duh! Wewe umekazania tu watu wanabeba box!!!! Watu shule zimepanda bwana na wengine mke na mume wanavuta kwa mwaka mpaka $200,000 sasa watu kama hawa kwa nini warudi Tanzania!? Kuijenga Tanzania siyo lazima uwe ndani ya Tanzania unaweza kufanya hivyo popote pale ulipo duniani. Na wengine wengi hawaishi kwa kubabaisha kama unavyodhani kwa kujiandikisha kwamba ni wanafunzi wengine wameshachukua hata uraia wa nchi wanazoishi. Acha kuwa ni fikra potofu kuhusu Watanzania wanaoishi nchi za nje.
 
Mkandara,

..kwa kiwango kikubwa nakubaliana na maoni yako.

..challenges ziko kila mahali. hata kwenye nchi za watu usipoangalia unaweza kuibiwa ideas zako.

..ila lazima tusisitize kwamba ukiwa ulaya na marekani 50,000 USD is nothing. ukiwa Bongo kiasi hicho cha fedha kinaweza kukufikisha mbali sana.

..off course mahali popote[Tanzania,Ulaya,Marekani] lazima ujiweke karibu with the "right people."

NB:

..wengi wetu tunarudi Bongo na elfu-hamsini zetu tukitegemea fedha hizo hizo kwa chakula,makaazi, na mtaji wa biashara.

..tena biashara nyingi za wabongo zinafilisika kutokana na reality hiyo. lazima uweze kuizungusha hela, na kuipa biashara muda ichanue na kukupa faida.
 
Duh! Wewe umekazania tu watu wanabeba box!!!! Watu shule zimepanda bwana na wengine mke na mume wanavuta kwa mwaka mpaka $200,000 sasa watu kama hawa kwa nini warudi Tanzania!? Kuijenga Tanzania siyo lazima uwe ndani ya Tanzania unaweza kufanya hivyo popote pale ulipo duniani. Na wengine wengi hawaishi kwa kubabaisha kama unavyodhani kwa kujiandikisha kwamba ni wanafunzi wengine wameshachukua hata uraia wa nchi wanazoishi. Acha kuwa ni fikra potofu kuhusu Watanzania wanaoishi nchi za nje.

Lakini Mkuu
mbona hutaki kunielewa mimi sikuelewi nimesema watu wenye nafasi nikiwa na maana yahao waliokwenda shule hawana sababu ya kurudi nyumbani na tunachowaomba watupe sisi fursa huku nyumbani.

Nawale wezangu na mimi wabeba mabox tuangalia namna ya kurudi nyumbani .Mkuu labda sieleweki ama labda tayari umeshaniweka ktk kundi fulani ,mbona narudia sana hayo maneno kipi kisichoeleweka??
 
mwenye macho na some na mwenye masikio na asikie......mkitaka kufa mapema njooni

Ha ha ha..

Muzee nipo bongo, natafuta kazi ya maboxi popote pale nimechoka maisha ya passport size bana..Maisha gani kila siku afadhali ya jana?
 
Lakini Mkuu
mbona hutaki kunielewa mimi sikuelewi nimesema watu wenye nafasi nikiwa na maana yahao waliokwenda shule hawana sababu ya kurudi nyumbani na tunachowaomba watupe sisi fursa huku nyumbani.

Nawale wezangu na mimi wabeba mabox tuangalia namna ya kurudi nyumbani .Mkuu labda sieleweki ama labda tayari umeshaniweka ktk kundi fulani ,mbona narudia sana hayo maneno kipi kisichoeleweka??
Fafanua jinsi unavyotafsiri neno hilo.
 
...nafikiri wabeba box wenye bidii wana maisha mazuri na wana msaada mkubwa kwenye familia(back home),acha vijana wajitahidi na maisha yao,wewe kama unataka kurudi rudi tuu na sijui kama kweli wanahitajika nyumbani kuliko $$ zao wanazotuma kila siku kusaidia familia zao!
 
Back
Top Bottom