Nini mtazamo wako juu ya kauli ya Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso?

Mkuu huyo jamaa alikufanya nini? Ni kutofautiana tu mitazamo au kuna kitu chengine zaidi?
 
Nasikia jamaa anapitia sana Hotuba za Mwamba Jiwe Magufuli.
 
Kuna mfanano naouna Kati yake na mmoja wa Marais waliowahi kuiongoza nchi yetu. Kudos!
 
Taarifa ya rushwa unaipata kutoka kwa wakoloni,(western media), hahaha,kalaghabaho
Media gani hapo, hiyo ni website ya wanaharakati Transparency International Toka lini transparency International ni ya diaspora
 
Media gani hapo, hiyo ni website ya wanaharakati Transparency International
Toka lini transparency International ni ya diaspora
Ukishasema tu transparency halafu "International" tayari moja kwa moja tunajua ni nani yuko nyuma ya hicho chanzo.... tangu lini hizo International media outlets zikawa na jema kuhusu viongozi wazalendo wa kiafrika wanaokinzana na matakwa yao zaidi ya kueneza propaganda chafu tu dhidi yao?

Hizo huwa mnaziamini nyie tu walamba makalio ya wazungu na kuwaona wao ni Miungu watu wa hapa duniani.
 
Aliyoyasema ni yapi, maana inaonekana unayajua yote na haya niliyoandika hapa sio maneno yake.
Kuna kutofautiana katika uelewa wa yaliyosemwa. Matokeo yake ikatolewa tafsiri tofauti, hilo silo jambo la ajabu kutokea.
 
Dah!
Mkuu 'T14 Armata', umekuja na hoja ambayo sikuitegemea kabisa kuwa inaweza kuwa sehemu ya kutishia watu!
Teknolojia mbona ipo kila mahala siku hizi. Wewe unadhani hao jamaa wa magharibi bado ndio wanao miliki teknologia yote? Maswala ya magari, hujui Joe analia sana kuhusu mchina anavyoteka soko la magari ya umeme duniani? Wewe unadhani bado kuna nchi au kundi la nchi linalohodhi teknolojia tena, kwamba waitumie kama silaha ya kuwatwanga wengine? Kwani hiyo teknolojia kwani ni ya nini, si ni biashara? Wewe unadhani watakubali kupoteza biashara kizembe?
Sitaeleza hili kwa kirefu, lakini nakupa tu mfano uufikirie na kupata jibu la hoja yako hii.

Mfano wenyewe ni huu: usifikiri nchi za Magharibi ziliwapenda sana waChina wakati nchi hiyo ilipo amua kufunguka na kufanya biashara na mataifa hayo. Na usidhani hata kwa mara moja kuwa waChina waligeuka kuwa watu wazuri sana kwa mataifa hayo kiasi kwamba makampuni ya nchi hizo yakimbilie huko, tena kwa masharti magumu sana ya uwekezaji.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala ya namna hii utaelewa ninacho lenga hapa kujibu hoja yako.
Ili umaanishe Traore yuko sahihi inabidi tusikuone humu, uanze kujitenga kama anavyotaka kuitenga nchi yake. Ama ukubali wewe ni shoga ndio maana umeweza access huduma za unaoita mashoga.
haya maneno ndiyo unayomlisha wewe, kwa tafsiri unayoitaka wewe. Kukataa kukubali masharti ya nchi za Magharibi haina maana ya kujitenga na kila nchi duniani. Sijui tafsiri hii mnaitoa wapi? Nchi za Magharibi siyo DUNIA.
 
hicho kichura kwenye avatar yako kinawajibika kwa nani?
rushwa ikoje? ufisadi?

yani mnapenda kuongea ujinga as if kwe u kuna nafuu,.... wewe hapa kazi kusifia hicho kibibi kisicho na lolote
 
T14 Armata kuna time huwa anakuruouka kwa hojabza kipumbavu pumbavuuuu. Sema ndio hivyo tena kuna watu mtu unawaheshim tu kwakua kwenye uoande mwingine wana madini mazuri kama huyu jamaa. Ila kukukuruoa huwa anakurupuka muda mwingine . Nafikiri ana amhaba yaliopitiliza kwa West
 
Captain Ibrahim Troure kwa umri wake anajitahidi kuongoza nchi vizuri mpa mda hu
 
Wewe sasa umezungumza kitu chenye akili kubwa.

Binafsi huwa sipendi kabisa viongozi ropo ropo na wenye mihemko huyu jamaa ni type ya wakina Magufuli.

Anapaswa kuwa low-key na ku buy time sio hizi mbiringe mbiringe anazo enda nazo sasa.
 
Nimeamini sisi waafrika wengi wanapenda watu maarufu, wajinga wajinga, wenye mihemko katika vyeo vikubwa.

Kwenye kuongoza nchi unapaswa uwe mjanja sana na mtu makini huyu bwana kwa mfano ukamtoa Burkina Faso kwa nafasi aliyonayo ukampeleka China na ukamtoa Xi Jinping ukamuweka yeye ndani ya mwezi China inaenda mlama.

Kwenye kuongoza unahitaji watu wali calm, wasio na mihemko, wasio na macho mafupi yanayo tazama leo na kesho tu bali macho yatakayo tazama taifa lilikuwa wapi, lipo wapi( katika hali gani hapa siasa za ndani na za nje ) na linapaswa kuwa wapi miaka ijayo( hapa ndipo penye ugumu mkubwa)

Huyu bwana mdogo anapaswa ajifunze kwa mabwana zake warusi sasa( katika kupambana na mifumo iliyo kita mizizi tena Urusi ni taifa kubwa lenye uchumi mkubwa na rasimali nyingi linapitia hali gani ? halafu achanganye na akili zake na za washauri wake je, Burkina Faso inaweza pambana ? Au ina hitaji ushirikiano na mataifa yote ya pande zote )

asiishie tu hapo ajifunze na kwa Kim wa NK je kujifungia kama panya kumeiimarisha NK au ndio kutwa kuwa lilia China wawape misaada

Kingine cha mwisho ajifunze kwa wachina namna wanavyo pambana na mifumo ya kimagharibi huku wakati huo huo akinufaika na mifumo hiyo hiyo ya kimagharibi( nacho maanisha kumshinda adui kwa mchezo wake huo huo anao cheza unakuwa smart kuliko yeye )

Huyu bwana mdogo anapaswa kuwa smart sana tu tena sana ningekuwa mtu wake wa karibu ningemshauri apeleke wataalam Singapore wakajifunze iliwezekana vipi Singapore wakati wa Cold war na sasa kuweza kuwa neutral kwa powers mbili.

Lee aliweza vipi kuifanya Singapore kutoegemea upande mmoja bali kujali maslahi yake na kushirikiana na pande zote licha ya kutokuwa rasimali nyingi kama walizonazo Burkina Faso.

Singapore mpaka leo siasa zao za ndani na za kimataifa ni bora sana kwa sababu wao ni smart.
 
Hapa unafanya juhudi za kujisahaulisha tu, kwamba watu hawakulazimika kushika silaha na kumwaga damu kutafuta uhuru wao toka kwa watu hao hao ambao wao ndio wamekubuhu katika hayo unayotaka Traore ayafanye, ya unafiki.

Unatoa mifano ya Urusi na Korea kaskazini. Kwa akili yako unadhani hivyo vikwazo walivyo wawekea nchi hizo na nyinginezo, kama Iran, zimekomesha maisha ya wananchi wa nchi hizo kuishi, unataka wakajitweze kwa hao wakubwa!

Katika jamii yoyote, watu wa aina yako hawakosekani. Hata enzi za utumwa watu wa misimamo kama huu wako walikuwepo, na kama wao ndio wangesikilizwa, siyo ajabu utumwa hadi leo hii ungekuwa unaendelea.
China hajitwezi kwa nchi hizo kama unavyo fikiri wewe.
Traore hajasema hatashirikiana na mataifa mengine; bali katika akili yako unadhani kushirikiana na mataifa hayo ndiyo njia pekee ya nchi kupata mafanikio.
Lakini hata katika nchi hizo za Magharibi, siyo kila nchi inafuata mwongozo wa mkubwa wao, kwa hiyo ushirikiano na nchi hizo utakuwepo.
 
Safi akifanikiwa kujenga system nzuri ya uongozi atakuwa amepiga bao kweli kweli.
Shida kazi kunwa aloifanya itakuja kuharibiwa na mpuuzi mmoja, ndo maana viongozi wengi wa kimapinduzi hutaman kutawala milele. Ningekuwa Traore sitokuja kuachia madaraka mpaka kifo
 
Upo sawa.

Tunatofautiana uwezo wa akili, wenda wewe una akili nyingi kunizidi hivyo una nafasi ya kuona mambo kiupana kunizidi.

Lakini tambua mihemko haijawahi saidia kuongoza sasa jiulize kati ya China na North Korea nani ana nafasi bora.

Burkina Faso ni ndogo na masikini sana inahitaji watu watakao tuliza mihemko na kujenga nchi kupambana na mifumo iliyokita mizizi sio kazi ya mihemko bali akili.
 
Captain Ibrahim Traore, President of Burkina Faso, reduced all Ministers and politicians salaries by 20 percent.

This guy is a real Pan-afticanist
 
Nevertheless, he refused to accept a President's salary and maintain his salary as a military captain. His salary as a soldier and not a president.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…