Hapa unafanya juhudi za kujisahaulisha tu, kwamba watu hawakulazimika kushika silaha na kumwaga damu kutafuta uhuru wao toka kwa watu hao hao ambao wao ndio wamekubuhu katika hayo unayotaka Traore ayafanye, ya unafiki.
Unatoa mifano ya Urusi na Korea kaskazini. Kwa akili yako unadhani hivyo vikwazo walivyo wawekea nchi hizo na nyinginezo, kama Iran, zimekomesha maisha ya wananchi wa nchi hizo kuishi, unataka wakajitweze kwa hao wakubwa!
Katika jamii yoyote, watu wa aina yako hawakosekani. Hata enzi za utumwa watu wa misimamo kama huu wako walikuwepo, na kama wao ndio wangesikilizwa, siyo ajabu utumwa hadi leo hii ungekuwa unaendelea.
China hajitwezi kwa nchi hizo kama unavyo fikiri wewe.
Traore hajasema hatashirikiana na mataifa mengine; bali katika akili yako unadhani kushirikiana na mataifa hayo ndiyo njia pekee ya nchi kupata mafanikio.
Lakini hata katika nchi hizo za Magharibi, siyo kila nchi inafuata mwongozo wa mkubwa wao, kwa hiyo ushirikiano na nchi hizo utakuwepo.