Mkuu, mbona unazunguka zunguka humo humo?
Bukina Faso ajipendekeze au awe na mihemko haitamsaidia chochote.
Jibu pekee ni Bukina Faso wenyewe kujitambua na kuadhimia kubadili hali yao inayowakabili. Hawawezi kuwa na nafuu yoyote kwa vile wanajigalagaza kwa hao wakubwa, au wanahemuka kwa yeyote.
Juu ya hao Korea Kaskazini na China sielewi unachohoji hapo. Ni wazi mawazo yako yametekwa kabisa na 'propaganda' za hao unaodhani dunia yote ni mali yao, usiponyenyekea kwao maisha yako na watu wako yanakuwa duni.
Hebu tueleze, ulishawahi kufika Korea Kaskazini na kuona hali yao ilivyo, au unayo picha tu ya kuambiwa na hao wanaoshikilia akili yako?
Korea Kaskazini, Zimbabwe, na kwingineko wamewekewa vikwazo vya kiuchumi na nani na kwa sababu zipi, unajuwa? Maana ya kuwekewa vikwazo, ni ili iweje, unajuwa?
Sasa unahimiza wabinuke juu walambe ili iweje? Kuna binaadam wasio kubali kudhalilishwa utu wao kwa bei yoyote ile. Ndiyo maana wengi wetu tulikataa utumwa, na tukakataa ukoloni na sasa tunakataa ukoloni mambo leo.