Nini nifanye niipate simu iloibiwa?

Nini nifanye niipate simu iloibiwa?

Daaah kwamba hii ndio bas haiwezekan kbs kuipata?
Futa wazo la kuipata. Mimi niliripoti polisi nikatakiwa nilipe 50,000 eti kwa ajili ya kuitrack. Miezi 3 ikapita kimya. Nilipoenda kukumbushia nikaambiwa haijapatikana na 50,000 yangu wamekula. Mpaka leo miaka 2 nilishakata tamaa!!
 
Tufundishe Tecno yangu naipenda sana aisee
Kunarafikiyngu karibia nae juz kwenye daladala jamaa nimechat nae ananijibu bila wasiwasi 😃😃😃
Hio ni app IPO play store unaiunga na Simu yako yaan huyo Mwizi hata akajifiche kwenye shimo la wapi location inasoma mbaya sasa unaweza ukaitumia Simu akiwa nayo yaan unaweza ukaipiga lock asiweze kuitumia kabisa na unaweza ukaitumia akiwa nayo na unaweza ukampiga picha bila yeye kupenda kiufupi inafanya vingi km ukiibiwa Simu Ila Ina segment zingine za kulipia ukitaka ku-upgrade
 
Futa wazo la kuipata. Mimi niliripoti polisi nikatakiwa nilipe 50,000 eti kwa ajili ya kuitrack. Miezi 3 ikapita kimya. Nilipoenda kukumbushia nikaambiwa haijapatikana na 50,000 yangu wamekula. Mpaka leo miaka 2 nilishakata tamaa!!
Sas nachouliza mim.

Sim naiona kwa location hata nikiweka direction inanionesha njia had kuifikia. Nikienda bila kupitia police huko nitakuw sawa kwel?
 
Kanunue simu mpya

Usipoteze muda endelea na shughuli zako

Imeshafunguliwa hiyo na vifaa vyote vimeuzwa kama spare
Wanaweza fungua na kutoa vifaa ila hawawezi kubadili IMEI namba ya simu, hivyo akikomaa kuisaka ataipata tu hata kama ni mwakani.

Ila kama hajui IMEI namba ya simu yake hawezi kuipata.

Usimkatishe tamaa
 
Hio ni app IPO play store unaiunga na Simu yako yaan huyo Mwizi hata akajifiche kwenye shimo la wapi location inasoma mbaya sasa unaweza ukaitumia Simu akiwa nayo yaan unaweza ukaipiga lock asiweze kuitumia kabisa na unaweza ukaitumia akiwa nayo na unaweza ukampiga picha bila yeye kupenda kiufupi inafanya vingi km ukiibiwa Simu Ila Ina segment zingine za kulipia ukitaka ku-upgrade
Daaah hyo mzur,inaitwaje hyo kaka.
 
Sas nachouliza mim.

Sim naiona kwa location hata nikiweka direction inanionesha njia had kuifikia. Nikienda bila kupitia police huko nitakuw sawa kwel?
Bila wasalama sio sawa. Huwezi jua jamaa ni mbabe kiasi gani. Asije akakudhuru
 
Wanaweza fungua na kutoa vifaa ila hawawezi kubadili IMEI namba ya simu, hivyo akikomaa kuisaka ataipata tu hata kama ni mwakani.

Ila kama hajui IMEI namba ya simu yake hawezi kuipata.

Usimkatishe tamaa
Daaah
 
Daaah hyo mzur,inaitwaje hyo kaka.
Glympse
 
Nenda vingunguti kwa mafundi simubunaweza ukaipata mana mwizi akiiba simu yenye password lazima ataipeleka kwa fundi kwwnza
 
Vyote navijua kaka had imei
Kama unaijua IMEI ya simu yako ni rahisi sana kuipata mwizi hata aweke Sim card mpya mitandao yote ya simu huwa inajua ni simu aina gani hivyo ikiwa umeripoti kwa kitengo cha cyber watamjua mwizi ni nani.
 
Kaenda polisi kaambiwa mchakato wake mrefu sana. Mpk aende sjuw tcra akapate location ambayo inagarim 50000 elfu,hlf aende kituoni atoe hela ya mafuta ndio wakaitafute,kwa mujbu wa maelezo alopewa. Sas hapo wakanichanganya kbs
Ni tz pekee ukiwa na shida ni lazima upitie shida zingine ili upate suluhu ya shida, yaani unapigwa kote kote
 
Tafuta pesa ununue nyingine, cha kulinda zaidi kwenye hizi simu za kawaida ni taarifa zako tu.

Vuta email yako, ifute kwenye ile simu, renew line yako, fungua WhatsApp acc yako, fb account na nyinginezo kabla hiyo mpuuzi hajaanza kutapeli ndgu jamaa na rafiki zako kwa kutumia accounts zako
 
Nenda polisi kitengo ya cyber security watakusaidia mkuu.
 
Back
Top Bottom