Japkas
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 3,011
- 4,617
Kuepusha kuchomana na magunia ya mkaa it's better kukaa pembeni. Wanaume wengi sasa hivi wakiona kuna dalili ya kupotezana uhai wanaondoka na kwenda kupanga. Hii hali ipo sana sasa hivi. Huenda mwanamke kuna jambo amefanya la hatari au alikuwa katika mission na jamaa kajua hajataka malumbano kamuachia mji akae na watoto na kuhudumia kila kitu.Wakuu,
Huyu jamaa ni jirani yangu haswa, yaani tunashare upande mmoja WA ukuta wa fensi,shughuli nyingi za kifamilia Huwa anashiriki vizuri Sana, migogoro pia anakuja kusuluhisa na kunishauri pia.
Japo Kwa ndoa yake niliamini Ni ndoa iliyokamilika haswa maana tangu miaka yote tuishi hapa sijawahi kusikia kagombana na mkewe Hata siku moja, hivyo Huwa nawaheshimu sn.
Kuna siku mkewe alileta malalamiko kwangu kua mmewe kahama nyumbani kwake ghafla,
Anasema siku ya mwisho kuonekana NYUMBANI, aliaga Kama kawaida anaenda kazini kwake asbh na MAPEMA na ndo hakurudi mazima mpaka Leo hii.
Anadai hakubeba chochote kile nyumbani, Kila kitu Kiko Kama kilivyo kua, hawajagombana na wala hajaambiwa kipi kamkosea.
Anadai Mume wake tangu ahame matumizi ya Kila siku anatoa vzur Ila haifiki kabisa nyumbani. anapewa boda ndo apeleke.
Anasema mumewe akipigiwa simu anapokea anadai atarudi TU Ila kavumilia Sana anaona haioni dalili yoyote ya mumewe kurudi nyumbani.
Anasema alishapeleleza Sana hadi kujua anapoishi, kaenda Sana pale (Hadi mida ya usiku sn) labda Kuna mwanamke anaishi nae pale Ila kathibitisha mumewe anaishi peke yake TU na haijawai kuleta mwanamke yeyote pale Hata siku moja.
Anasema keshapeleka kesi Kwa wazazi pande zote mbili, mumewe anadai hamna tatzo, Kuna mambo anayaweka sawa, yakikaa sawa atarudi nyumbani,wala Hana tatzo nae.
Kavumilia Sana Ila haoni dalili yoyote mumewe kurudi. Anadai keshapeleka kesi kanisani, mumewe alishaitwa Sana kagoma kwenda na Kuna siku kapigiwa kamtukana Hadi askofu.
Anasema ilivyofika miezi 3 haoni dalili yoyote akajaribu kwenda ustawi WA jamii kumfungulia kesi ya kutelekeza familia (labda atapata hofu ya serikali), mumewe alivotoka uko ndo kamchukia kabisa na kamblock kwenye mawasiliano yake yote na pesa za matumizi ya familia Kwa Sasa anachukulia ustawi WA jamii.
Jamaa nimejaribu kumdadisi tatzo Nini,hataki kabisa kufunguka, anadai hana tatzo lolote na mkewe, Kuna mambo yake kadhaa anayaweka sawa, punde tu atarejea home nisijali.
Kila mara nimejaribu kumkubushia mkewe anavoteseka kuukosa uwepo wake nyumbani, jamaa Wala haoneshi kujali, miezi 6 sasa inakatika, jamaa hana mahusiano yoyote nje, kuoa mke mwingine Wala Hana mpango wowote WA kurejea nyumbani kwake.
Watoto wao wote sahv wamerejea mashuleni, mkewe juzi kati kaumwa sn mpk kalazwa, jamaa kataarifiwa Ila katuma pesa TU Hata hajakanyaga hospital Wala kumpiga simu kumjulia hali.
Aliporuhusiwa ikabd ahamie kwangu mpk atakapokaa sawa maana watoto wao wote wamesharud mashuleni, jamaa nilimtaarifu Hilo ili atoe ruksa mkewe augulie kwangu, kasema sawa Haina shida. Ni Mwezi Sasa mkewe anashinda,kula na kulala nyumbani kwangu. Jamaa Hana Hata wasiwasi.
Juzi kati kanunua kiwanja nje ya mji, kaniita nimsainie Kama shahidi na kashaanza msingi anasema hapa ndo anajenga makazi yake mapya.
Namuuliza hii inamaanisha Nini khs hatma ya familia yake, anasema haihusiani kbs na familia yake, na Wala nisije thubutu kumwambia chochote mkewe khs hili suala TUTAGOMBANA. Nkamwambia sawa Haina shida.
Hebu wakuu,
Huenda mi sio nzur kwny mambo kusuluhisha migogoro ya ndoa za watu.
Najua humu mna mawazo mazur sn na wataalam tele WA ishu hizi za ndoa.
Hebu nipeni mawazo mawili matatu niweze kuinusuru hii ndoa ya Hawa jirani zangu.
Mkewe tangu jamaa ahame, saivi Kawa Kama kuchanganyikiwa , simuelewi elewi kabisa. Hata anachoumwa Hata hakieleweki, nahisi ni stress za ndoa zake.
Pia, KUISHI NA MKE WA MTU NYUMBANI KWANGU, KIUKWELI binafsi nijistukia kua kimaadili HAIKAI VIZURI kabisa.
Nawasilisha wakuu🙏
Usilazimishe kumpeleka jamaa kwenye moto. Mpe muda