Nini sababu ya gari ya petrol kutoa moshi

Nini sababu ya gari ya petrol kutoa moshi

Soki

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
1,303
Reaction score
279
Wataalamu tafadhali pitieni hapa. Ni zipi zinazoweza kuwa sababu za gari ya petrol kuanza kutoa moshi kwenye ekzosti?

Moshi wenyewe unatoka kidogo tu na siyo mfululizo bali wakati fulani tu kama asubuhi gari inapowashwa.

Maarifa tafadhali!
 
kuna mambo hayajakaa sawa MKUU.Mara NYINGI gari ya petrol kutoa misho husababishwa na mchanganyiko wa mafuta na hewa kutokuwa sahihi.
au oil kuingia kwenye compastion chamber na kuunguzwa pamoja hewa na mafuta.

na kuna sensor nyingine ambazo zikifa au kuwa mbovu husababisha tatizo hilo kama airflow/airmass. vacuum sensor oxygen sensor spark plug zikichoka n.k

kwa ufafanuzi zaidi ungesema ni gari aina gani na lina engine aina gani.ndio ingetoa wepesi.

tusije tukawa tunatoa ushauri wa gari ya injection kumbe yako ni ya cabureter
 
Kuna mengi yanaweza kusababisha.'
  1. Oil iliyowekwa katika injini sio sahihi, oili ya petrol engine ni tofauti na ya diesel engine.
  2. Spark plugs inaweza kuwa zimechoka
  3. Piston rings zinaweza kuwa zimechoka
  4. Uwiano mbovu wa hewa vs. Petrol inayoingia ktk engine
Unashauriwa kumuona fundi ili akupe uhakika zaidi
 
Kama ni asubuhi tu inaweza kuwa valve seals zimechoka huwa zinakakamaa .
 
Ndugu nilikuwa na usingizi ndio maana nikachanganya mambo manake hii thread ililetwa usiku mnoo!!

Lakini kwani ilikuwa ni lazima uchangie mkuu? Umenichekesha sana! Da!
 
Kwani kama ni piston rings itakuwa inatoaje moshi wake; utakuwa mfululizo au ?
 
Kama ni asubuhi tu inaweza kuwa valve seals zimechoka huwa zinakakamaa .

Mkuu mara nyingi ni asubuhi tu. Na ikishaindoka huwezi wala kuona Moshi wowote. Labda wakati mwingine ikipaki mda. Na huo wa asubuhi kuna siku ilikuwa inatoa mwingi sana nikikanyaga accelerator lakini baada ya muda mfupi unaisha.

Lakini siku nyingine asubuhi ukiwasha haitoi moshi.
 
kuna mambo hayajakaa sawa MKUU.Mara NYINGI gari ya petrol kutoa misho husababishwa na mchanganyiko wa mafuta na hewa kutokuwa sahihi.
au oil kuingia kwenye compastion chamber na kuunguzwa pamoja hewa na mafuta.

na kuna sensor nyingine ambazo zikifa au kuwa mbovu husababisha tatizo hilo kama airflow/airmass. vacuum sensor oxygen sensor spark plug zikichoka n.k

kwa ufafanuzi zaidi ungesema ni gari aina gani na lina engine aina gani.ndio ingetoa wepesi.

tusije tukawa tunatoa ushauri wa gari ya injection kumbe yako ni ya cabureter

Ni injection mkuu....... Suzuki
 
Labda nikanuse leo mkuu!!
 
Moshi una rangi gani !!!???
Kuna smell gani hapo kwa exhaust, unajua harufu ya moshi mbichi!!???

Mkuu swali lako ni la msingi kabisa. Ngoja nikawashe gari asubuhi hii nije na maelezo. ILA KAKA HUO MOSHI MBICHI SIJUI UNANUKAJE MKUU. Kuhusu rangi siyo mweusi bali ni kama mweupe na sometimes wa blue. Ngoja niwashe gari
 
Moshi una rangi gani !!!???
Kuna smell gani hapo kwa exhaust, unajua harufu ya moshi mbichi!!???

Mkuu nimeiwasha sasa hivi iko kwenye silence na hakuna wowote hapa ila inadondosha maji kwenye exhaust.
 
Maelezo mengine ni kuwa wakati ilipokuwa inatoa moshi mwingi ilikuwa pia na misi kali sana.

Nikasugua plug kwa fundi kwani zilikuwa na weusi. Pia nimebadilisha engine oil.

Sasa sijui itakuwa ni petrol chafu au ni plugs au ni piston rings.

Baada ya service hiyo misi imepungua sana almost imeisha na moshi nao umepungua sana almost umeisha ila naona bado kwa mbali upo moshi wa blue nimakanyaga sana mafuta, ila kwa mbali sana na unaweza usiuone usipokuwa makini.
 
Mkuu Idimi ni kweli ni muhimu kuwaona mafundi ila niliona nianzie hapa kwa kuamini kuwa wako mafundi wazuri au wengine wenye uzoefu wa hili kabla ya kuwaendea mafundi garage!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Idimi ni kweli ni muhimu kuwaona mafundi ila niliona nianzie hapa kwa kuamini kuwa wako mafundi wazuri au wengine wenye uzoefu wa hili kabla ya kuwaendea mafundi garage!
Sawia kabisa.
Umefanya la msingi kupita hapa kwanza kabla hujaenda kunako mafundi.
 
Back
Top Bottom