Nini sababu ya gari ya petrol kutoa moshi

Nini sababu ya gari ya petrol kutoa moshi

Mkuu nimeiwasha sasa hivi iko kwenye silence na hakuna wowote hapa ila inadondosha maji kwenye exhaust.

Ok naweza kuthubutu kusema sio tatizo la ring hilo ila ignition/sparking system na haswa hapo kwenye plugs !!!!!!!

Baada ya kukaa kwenye silence kwa muda nikakanyaga accelerator, ikatoa moshi. Na huu moshi actually ni wa blue siyo mweupe.

Wakati huohuo inapotoa moshi huo inadondosha majimaji

Kitu kingine hii gari sasa hivi inakula mafuta kuliko kawaida!
 
umesema sahihi mkuu, na kwa kuongea tu kama mleta maada alivyosema kule mbele kwamba gari ikiwaka inatoa moshi mweupe na mafut ainakula sana sa hv.

nafikiri n piston ringi zimeanza kuchoka, na kati ya hizo , moja iko kaitika hali mbaya zaidi, kwa maana hiyo, mosh unatoka wa blue asubuhi ukiwasha gar ka sababu oil ambayo imebaki kwenye plug, ikichanganya na mafuta matokeo yakle n hayo.

swala la kula mafuta n kwa sababu kati ya hizo piston , (haijalishi n ngapi) moja ama mbili hazichomi kabisa, zinasababisha ukanyage zaidi accelarator ili kupata motion. ikiendelea hivyo mwisho wake utawasha gar na kuweka drive lakin haitatembea kabisa. solution ni kubadili piston ringi. before that, kapime plugs kwanza.

Kuna mengi yanaweza kusababisha.'
  1. Oil iliyowekwa katika injini sio sahihi, oili ya petrol engine ni tofauti na ya diesel engine.
  2. Spark plugs inaweza kuwa zimechoka
  3. Piston rings zinaweza kuwa zimechoka
  4. Uwiano mbovu wa hewa vs. Petrol inayoingia ktk engine
Unashauriwa kumuona fundi ili akupe uhakika zaidi
 
Mkuu General8 wazo langu ni kuweka plugs mpya kwanza halafu nione. Na je huko kudondosha maji kwenye tailpipe unakuzungumziaje?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, hiyo ni condersation tu na wala isikupe shida, n sawa tu na bati la nyumba yako kutoa umande umande asubuhi jua likiwaka, sababu ni kwamba mchana jua linawaka chuma kina expand, likipoa kina contrast, then kinatengezeza vumajimaji kama cooling system.

Mkuu General8 wazo langu ni kuweka plugs mpya kwanza halafu nione. Na je huko kudondosha maji kwenye tailpipe unakuzungumziaje?
 
Lakini pia ukumbuke baada ya kusafisha plugs na kubadilisha petrol filter actually na baadae kidogo kubadili engine oil na kuweka nyingine ( ya BP) SASA HIVI MIS NI KAMA IMEKWISHA WAKATI KABLA ILIKUWA KALI SANA KIASI KWAMBA ILIWAHI NIZIMIKIA MAHALI na ndipo nikaanza kujiuliza iwapo ni petrol chafu au plugs au piston au petrol filter au air cleaner ba kupata majibu.

Najiuliza kama tatizo ni piston rings kwanini MIS ikaisha wakati sijazibadili
 
Naomba nitofautiane na wooote mliochangia except bwana mmoja alosema maji kuchanganyika na petrol.

Hilo gari halina shida yeyote, ni gari zuri kabisa na kibongo bongo (hope hukununua mpya) bado ni kitu mnato hata usipeleke kwa fundi.

Moshi ama maji maji kutoka katika exhaust ni dalili kuwa ukiwa umepark gari the whole night engine iko intact na zile drops za combustion zimetengeneza kitu kama mvuke ambao hawezi pata kwenye gari yenye engine kuukuu.

Mimi sio mtaalamu wa magari ila ni uzoefu tu kwa yale niliyomiliki. Usipeleke kwa fundi, hongera gari bado sana hilo
 
Plug nzuri zaidi ni zipi kwa gari hii na zinabei gani hapa Dar?
 
Wengi hawayajui haya yaliyochambuliwa na wadau hapa. Ikiwa kuna mwenye nyongeza aweke hapa please
 
Kuna mengi yanaweza kusababisha.'
  1. Oil iliyowekwa katika injini sio sahihi, oili ya petrol engine ni tofauti na ya diesel engine.
  2. Spark plugs inaweza kuwa zimechoka
  3. Piston rings zinaweza kuwa zimechoka
  4. Uwiano mbovu wa hewa vs. Petrol inayoingia ktk engine
Unashauriwa kumuona fundi ili akupe uhakika zaidi

Mkuu hiyo no.1 tumeweka sahihi kabisa kwa hiyo hiyo haihusiki

No.2 inawezekana

no.3 na 4 bado sina hakika. Hivi hakuna symptoms ambazo hizo ni maalum kwa namba 3 ili mtu usijewapa mafundi wakafungua wakati hazina tatizo?
 
Baada ya kukaa kwenye silence kwa muda nikakanyaga accelerator, ikatoa moshi. Na huu moshi actually ni wa blue siyo mweupe.

Wakati huohuo inapotoa moshi huo inadondosha majimaji

Kitu kingine hii gari sasa hivi inakula mafuta kuliko kawaida!

Kaka mimi ntafia hapo tu kwenye uchomaji au uchanganyaji wa hewa na mafuta ili kupata mlipuko ndio penye shida!!!
 
Lakini pia ukumbuke baada ya kusafisha plugs na kubadilisha petrol filter actually na baadae kidogo kubadili engine oil na kuweka nyingine ( ya BP) SASA HIVI MIS NI KAMA IMEKWISHA WAKATI KABLA ILIKUWA KALI SANA KIASI KWAMBA ILIWAHI NIZIMIKIA MAHALI na ndipo nikaanza kujiuliza iwapo ni petrol chafu au plugs au piston au petrol filter au air cleaner ba kupata majibu.

Najiuliza kama tatizo ni piston rings kwanini MIS ikaisha wakati sijazibadili

Hilo sio tatizo la piston kaka piston moshi mweupe na haukati sababu oil inapenya! !!!
Lakini pia gari ndogo ya petroli mpaka kuua ringi sio kitu cha mara kwa mara!!!
Pia compression ingeshuka na ingekosa ile nguvu/pulling uliyozoea
 
Mkuu OLESAIDIMU nimenunua spark plugs mpya ngoja kesho fundi azifunge!!
 
Last edited by a moderator:
Kaka mimi ntafia hapo tu kwenye uchomaji au uchanganyaji wa hewa na mafuta ili kupata mlipuko ndio penye shida!!!

Nami nimelenga kuhakikisha kwamba hapo pako sawa kwanza!
 
Wakuu nimeweka plugs mpya jana leo asb nimeiwasha hamna moshi. Hivyo tatizo lilikuwa spark plugs bila shaka.

Nitaangalia leo nzima ku confirm
 
Kweli wewe unaijua gari. Matatizo mengi hapo juu niliyafahamu baada ya kununua gari kimeo... Nilitengeneza kila kitu hapo juu mwishowe gari ikakaa sawa.
 
Wengi hawayajui haya yaliyochambuliwa na wadau hapa. Ikiwa kuna mwenye nyongeza aweke hapa please

Mkuu Soki, hiyo ndio taaluma yangu. Fuata ulichoambiwa na bwana Jerry Msigwa, sana sana ntakushauri ubadilishe plug tu, narudia, badilisha plug tu usije ukadanganywa na mafundi kuwa gari yako mbovu, si kweli.Matatizo yanayotokea kwenye gari yako yanasababishwa na spark plug kuwa zimeisha nguvu. Kwa kawaida spark plug hutakiwa kubadilishwa kila baada ya km Elfu 15 na 20 toka ilipowekwa, hii ni kwa gari za kijapan sijui za mataifa mengine.Na pia nahisi uliweka petrol ambayo sio safi ndio maana unaona matatizo yamekuwa mengi. Lkn kwa mtiririko wa maelezo yako naungana na Mkuu Jerry Kuwa gari yako,"Mundai nai" (haina tatizo) la kukuumiza kichwa.
 
kuna mambo hayajakaa sawa MKUU.Mara NYINGI gari ya petrol kutoa misho husababishwa na mchanganyiko wa mafuta na hewa kutokuwa sahihi.
au oil kuingia kwenye compastion chamber na kuunguzwa pamoja hewa na mafuta.

na kuna sensor nyingine ambazo zikifa au kuwa mbovu husababisha tatizo hilo kama airflow/airmass. vacuum sensor oxygen sensor spark plug zikichoka n.k

kwa ufafanuzi zaidi ungesema ni gari aina gani na lina engine aina gani.ndio ingetoa wepesi.

tusije tukawa tunatoa ushauri wa gari ya injection kumbe yako ni ya cabureter
Langu ni Cresta gx 100 vvti engine, automatic.
 
Combustion due to incomplete burn of petrol
 
Naomba nitofautiane na wooote mliochangia except bwana mmoja alosema maji kuchanganyika na petrol.

Hilo gari halina shida yeyote, ni gari zuri kabisa na kibongo bongo (hope hukununua mpya) bado ni kitu mnato hata usipeleke kwa fundi.

Moshi ama maji maji kutoka katika exhaust ni dalili kuwa ukiwa umepark gari the whole night engine iko intact na zile drops za combustion zimetengeneza kitu kama mvuke ambao hawezi pata kwenye gari yenye engine kuukuu.

Mimi sio mtaalamu wa magari ila ni uzoefu tu kwa yale niliyomiliki. Usipeleke kwa fundi, hongera gari bado sana hilo
hahahaha, umenikosha sana ndugu yangu ingawa ni sms ya siku nyingi ila imejibu swali langu la leo.
 
Back
Top Bottom