Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
 
Kama haujui ukweli unatasemaje kwamba amekudanganya....

Kama alifanya uhalifu au ufisadi unategemea atakwambia ? Kama ilikuwa boring unadhani itauzika kwa watu kama story au ni bora aweke vinjonjo ?

Unadhani ni kweli Newton aliona apple inaanguka ndio akawaza kuhusu gravity (au story ya apple made it more sensational)?

Anyway bila evidence kama wamedanganya hauna budi kusikiliza bila kushutumu...
 
Unasikiliza lakini wana vyosema haviendani na uhalisia. Not logical
 
Back
Top Bottom