Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Yes ,siri ya utajiri anajua mwenye tajiri ,wengi hizi biashara tunazoziona front ni zuga tu ,ni kama kina Shamim zeze na mumewe ,kina niffer wanatundanganya walianza na mitaji ya elfu 10 na elfu 40 ni nonsense...Waweke wazi tu kwamba niliwezeshwa fungu na mtu fulani siyo mbaya appreciation zinakubalika.
Madogo wako bize kuwa amini motivation speakers 😞😞🥲
 
hiyo ni kawaida na ndo siri zenyewe,....tuna mfano mzuri, mdogo wake ROSTAM AZIZ kukutwa na hazina ya meno ya tembo na silaha nzito,....watu wanaona gas na hisa kumbe nyuma ni jangiri mkubwa,....huku kwetu miaka ya nyuma matajiri wengi walidhamini makundi ya ujambazi,...watu wanabomoa maduka ya jumla yale makubwa au magodown , kisha wanapeleka mzigo kwa tajiri ananunua kwa bei ndogo mno,...huku yeye akiwalinda dhidi ya sheria na kuwapa silaha,...kwasasa ,...ni dili za dollar na dhahabu kwenye black market,....wasomali,,(wasafiri harmu) ,...utakatishaji wa fedha za kifisadi,....ndo vinashika kasi sana,...
Mfano wa Said Lugumi kaonesha magari yake ya gharama kweli tena kwenye

Packing ya kisasa, alafu anasema kupitia kushona viatu hapa Dar ni mwanzo
wa yeye kufanikiwa.
 
Madogo wako bize kuwa amini motivation speakers 😞😞🥲
Wana waamini sana na kuwafuatilia hasa madogo wa chuo kikuu ndio

huwaambii kitu kuhusu hao motivation speaker ila baada ya kuja mtaani
ndio wanaelewa uhalisia wa maisha ulivyo.
 
Kazi kweli kweli ? Ndio wadanganye watu au ndio wanawapa motivation vijana wapambane?
Umeshaambiwa ni siri, pia kwenye utajiri mnatakiwa kuwa wachache. Hivyo ili kuzidi kuwapunguza ni lazima kuwadanganya ili kutunza na kuilinda siri.
Ukiona mtu anawakusanya watu ili kuwapa mbinu za kuwa matajiri au kukamata pesa, basi ujue huyo ni Kibwetele na watakaokusanyika kumsikiliza ndiyo waumini wake anaopanga kuwateketeza na kuua kabisa ndoto na mipango yao
 
Back
Top Bottom