Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Mafanikio ni siri. ukishindwa kutunza siri, sahau kuhusu utajiri na mafanikio.
 
Mtu anaweza kuongeza chumvi lakini mimi nimeshuhudia Fundi Baiskeli hatimae akafungua Duka la Spea za Baiskeli baadae akawa analeta Baiskeli na sasa kahamia kwenye Pikipiki na ni Multi Milionea.
Hii Ina make sense Haina ubishi
Sio zile za nilianza na kuuza karanga ss Nina kampuni ya mabasi 🤣
 
Utajiri ni siri ya mtu binafsi , washamba ni wale wanaoenda kwenye semina za kufundishwa utajir.
 
Utajiri ni siri ya mtu binafsi , washamba ni wale wanaoenda kwenye semina za kufundishwa utajir.
Hapa wanapigwa wengi sana, wanalipia semina na vitabu wana nunua eti wapate
maarifa na siri ya kupata utajiri.
 
Nakumbuka nilianza kufunga karanga za elfu moja. Sasa namiliki vi eite 5.
Mara ooh mimi nilikuwa na zungusha mchicha na matembele kwenye nyumba za watu na beseni kichwani, biashara imekuwa sasa napeleka nje ya nchi kwa ndege nimeweza kujenga ghorofa mjini kati.
 
Utajiri sio jambo rahisi hakuna mtu hapambani ukweli naouona Kuna njia mbili za kufanikiwa Moja unapambana mungu anaweka tiki huu ni utajiri mzuri ambao hauna maagano wa pili ni WA shetani ambao unaupata kiraisi sana na kwa maagano na huu mwisho wake unakuwa sio mzuri sasa wewe ndio wa kuchagua uende upande upi
Mwisho mzuri ni upi na mwisho mbaya ni upi mkuu?
 
Sio wao tu hata wewe kesho ukiwa mmoja wao hutasema kila kitu kwa sababu utajiri ni matokeo ya tabia ya mtu katika kumudu mambo makuu matatu
Mosi, Imani katika utendaji
Pili, Siri katika utendaji
Tatu, Nidhamu katika utendaji
 
Matajiri hasa hawa wa kibongo wengi wana msongo wa mawazo coz utajiri wao mwingi ni wa kutumia juju.
 
Sasa unataka ukweli upi mtu kama superfeo alianza kuhustle alivyomaliza darasa la saba wakati wengine waliendelea na shule miaka kumi mbele mpaka chuo biashara huwa inasumbua ukiwa na mtaji mdogo Kuna kuanguka sana wengi huwa wanakata tamaa hapa ila wanaokaza mwisho ukijipata halafu ukaweka njaa zaidi Mzee utajiri upo
Huyo super feo wako unamjua vizuri?🤔. au unataka tukwambie,....?
 
Ni kweli unayoyasema ila behind the scene na ku-make fortune si viatu wala maduka yao!! SSB anatajwa sana kwenye poaching ,Musukuma udhulumati wa madini ,kishimba anatajwa sana kurun bizness za Vigogo wa serikali kwa kupitia jina lake kwakuwa ni muaminifu hapo hapo na yeye akajiongeza.

Kuna jamaa mmoja maeneo flani alikuwa ana duka tu kubwa la nguo anatoka kanda ya kaskazini ,alikuwa pia ana duka genge ,anauza mkaa ,maji na vitu vingi vingi ,lilijaza balaa akajenga nyumba mbili enzi hizo tulikuwa tunaita "SEFU KONTENA" ,jioni alikuwa anasema anafanya kazi ulinzi kumbe behind the scene alikuwa "MANDONGA MTU KAZI SHOW SHOW aka MZEE WA MJEGEJE" ilikuja kubainika baada ya kushikwa kwa ujambazi....Kwahiyo kuna baadhi ya watu wanafanya biashara front kucover ufirauni wao wa nyuma.
hiyo ni kawaida na ndo siri zenyewe,....tuna mfano mzuri, mdogo wake ROSTAM AZIZ kukutwa na hazina ya meno ya tembo na silaha nzito,....watu wanaona gas na hisa kumbe nyuma ni jangiri mkubwa,....huku kwetu miaka ya nyuma matajiri wengi walidhamini makundi ya ujambazi,...watu wanabomoa maduka ya jumla yale makubwa au magodown , kisha wanapeleka mzigo kwa tajiri ananunua kwa bei ndogo mno,...huku yeye akiwalinda dhidi ya sheria na kuwapa silaha,...kwasasa ,...ni dili za dollar na dhahabu kwenye black market,....wasomali,,(wasafiri harmu) ,...utakatishaji wa fedha za kifisadi,....ndo vinashika kasi sana,...
 
hiyo ni kawaida na ndo siri zenyewe,....tuna mfano mzuri, mdogo wake ROSTAM AZIZ kukutwa na hazina ya meno ya tembo na silaha nzito,....watu wanaona gas na hisa kumbe nyuma ni jangiri mkubwa,....huku kwetu miaka ya nyuma matajiri wengi walidhamini makundi ya ujambazi,...watu wanabomoa maduka ya jumla yale makubwa au magodown , kisha wanapeleka mzigo kwa tajiri ananunua kwa bei ndogo mno,...huku yeye akiwalinda dhidi ya sheria na kuwapa silaha,...kwasasa ,...ni dili za dollar na dhahabu kwenye black market,....wasomali,,(wasafiri harmu) ,...utakatishaji wa fedha za kifisadi,....ndo vinashika kasi sana,...

Yes ,siri ya utajiri anajua mwenye tajiri ,wengi hizi biashara tunazoziona front ni zuga tu ,ni kama kina Shamim zeze na mumewe ,kina niffer wanatundanganya walianza na mitaji ya elfu 10 na elfu 40 ni nonsense...Waweke wazi tu kwamba niliwezeshwa fungu na mtu fulani siyo mbaya appreciation zinakubalika.
 
Back
Top Bottom