Ni kwasababu mara nyingi utajiri wameupata kwa njia za panya, yaani kihalifu
Mhalifu hawezi kukiri ni mhalifu kirahisi, si ndio?
Lakini nilichogundua ni kwamba kuna patterns flani utazisikia kwa matajiri wengi; kukwepa kodi, kutakatisha fedha, kutumia milango ya siasa nk
Mfano niliwahi kusikia mo alitumia connections zake za kisiasa kununua makampuni kwa bei ndogo kipindi cha mkapa
Au kuna hii taarifa ya rostam kutaka kutawala sekta ya madini kwa kulazimisha makampuni yamuuzie hisa nyingi
Hizo njia za kihalifu pia ni ngumu, kwahiyo kazi kazi usidhani kuna kitonga popote. Ukifanya uhalifu unarisk kunyea ndoo.
Pia nasikia kuna kiwango cha utajiri unaweza pata kwa njia halali, na kuna kiwangi ambacho huwezi kukipata bila kuwa mhuni, ila sijui ni viwango gani.
Na mpaka ufikie hiyo level ya kutakatisha hela, kutumia wanasiasa, maana yake unazungusha hela kubwa kwahiyo hapo nyuma kuna kamsoto ka kuanzia.
Sema asilimia kubwa ya matajiri huwa wametoka kwenye familia zenye uwezo...
Ukifuatilia jinsi wamarekani wanavyowachukulia billionaires nchini kwao utaelewa zaidi