Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Watu wanashindwa kutofautisha kati ya utajiri na kuyapatia maisha!

Kila mtu huyapatia maisha kipindi fulani Cha maisha yake!kubaki kwenye kilele hicho na kuendelea zaidi Hadi utajiri ndio kazi ilipo hapo!!

Kwanza ku maintain bila kushuka halafu kupanda kilele kufikia utajiri hapo ndipo majaaliwa ya Mungu au kulazimisha kwa kafara ya maisha Yako has uchawi na uganga!

Wengi TU tunajipata lakini baada ya kujipata unapigwa scard na shetani Hadi unaweza anguka anguko kuu!

Wengi tumewaona!

Mungu wenu hataki muwe matajiri hadi mpitie kwa shetani?
 
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Wengi huwa wanaongea ukweli ila shida ni kwamba njia ambazo mwenzio amezitumia kupata utajiri sizo ambazo wewe unaweza kuzitumia ili upate utajiri huo.

Matajiri Wengi wanaonekana ni waongo kwasababu vitu wanavyoongea ni vile vile ambavyo vimezoeleka sana kusikika kwenye maskio ya watu ila ndio uhalisia wa mambo.

Tajiri atakwambia usikate tamaa, kwasababu yeye ako na msululu wa biashara ambazo amezijaribu ila hazikumtoa hadi alipokutana na biashara hiyo ikiyompa utajiri.

Tajiri atakwambia heshimu watu kwasababu yeye wakati yupo kwenye hiko kipindi cha kujaribu na kufeli pengine aliwahi kukutana na mtu katika mazingira yasiyo ya kutarajia akamshika mkono.

Tajiri atakwambia ni bahati tu kwakua amejaribu biashara kibao na alitumia nguvu kibao ila biashara ambayo aliianza tu kimasihala ndio ambayo imekuja kumtoa.

Kwahiyo hakuna siri yoyote kwenye utajiri ila siri ipo kwenye hatima ya mtu, ndio maana ni nadra sana kukuta Elon Mask na ukoo wake wapo kwenye orodha ya matajiri wa dunia.

Na hakuna Tajiri yeyote anaeongea uongo wanasema ukweli mtupu ila shida ni kwamba walio wengi huwa wanazungumzia sana struggle za nyuma kuliko pale walipopatia utajiri kwasababu wao wenyewe hawajui namna sahihi ya kupaelezea "miracle".

So tuendelee kupush and kujaribu huku na huku hadi tutakapopata njia sahihi ya yake yaliyo upande wa hatima zetu kwa maana huko ndiko kuliko na bahati.
 
Neno utajiri Kwa muono wa Mungu ni pana sana,sio kwa fikra zetu finyu,eti Mali za kidunia pekee!utajiri una tafsiri pana Sana kwake!
Kwahiyo Mungu wenu hataki muwe matajiri duniani hadi mbinguni? Yani kawaumba ili mteseke tu duniani? Wewe kwa akili za kibinadamu unaweza kubali mwanao ateseka wakati una uwezo wa kumsaidia? Story zenu don't make any sense. Zinamchafua zaidi Mungu wenu kuliko kumsifia.
 
Shetani ni sawa na mtu ambaye alikuta kiwanja hakuna mtu akaamua kujimilikisha lakini mmiliki yupo na hati kaamua kutulia tu pesa na dhahabu ni mali ya Bwana

Hujajibu swali, Mungu wenu hataki muwe matajiri? Yani purposely anataka watu wake mteseke? Inabidi dishi licheze kuamini hizi story.
 
Utajiri sio jambo rahisi hakuna mtu hapambani ukweli naouona Kuna njia mbili za kufanikiwa Moja unapambana mungu anaweka tiki huu ni utajiri mzuri ambao hauna maagano wa pili ni WA shetani ambao unaupata kiraisi sana na kwa maagano na huu mwisho wake unakuwa sio mzuri sasa wewe ndio wa kuchagua uende upande upi
Hakuna Mungu wala Shetani anayegawa utajiri.

Hakuna mtu aliyetajirishwa na Mungu.

Hakuna mtu aliyetajirishwa na Shetani.
 
Utajiri huamki na kuwa tajiri bali unaanza taratibu
Mtu kafanikiwa baada ya miaka 20 unamuuliza amepata wapi utajiri
Ila siku anaanza kuuza dagaa ulikuwa unamcheka

Mnataka mtu auze ugoro miaka 40 kila leo unampita hapo
Baba anza leo ila unakuwa na bahati yako pia
Unaweza ukawa tajiri na ukaporomoka na unaweza pia ukawa tajiri ukiwa mzee kama kina Kentucky wa fried chicken 🍗 kawa millionaire kwa umri wa miaka 65
 
Utajiri mkubwa kwa Mungu ni kutenda mema utajiri wa mali ni nyongeza tu sio lazima ila kwa mtu yoyote akiomba kwa bidii utajiri Mungu ana anakupa
Huyo Mungu Alishindwa na Anashindwa kuwapa hata chakula Maelfu ya watoto, wanawake na wazee wanaokufa kwa njaa wakilia na kumuomba awasaidie,

Halafu ndio unasema huyo Mungu anagawa utajiri?

Utajiri gani?
FB_IMG_1722976782305.jpg
 
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Tanzania hakuna ni wafanya biasha wa kuhasabika walio fan ikiwa kihalali bila kushirikiana na watu wa serikalini kuiba kodi na rasiri mali za umma. Wewe nchi ambayo hata ukiweka hela bank ,badala ya bank kulipa liba kwenye hela wanazo kama nazo bank. Wao ndio wanarundikia mwenye account fees na charges za kiwizi. Eti Ledger charge, VAT charge kwenye saving accounts?
 
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.
Siyo uongo, kwa yeyote ambaye hajarithi utajiri, ni lazima aanze maisha ya kutokuwa na kitu, maana hakuna pesa za utajiri ambazo utaokota tu njiani.

Ova
 
Wasalam wakuu,

Imekuwa ni jambo la kawaida matajiri wakihojiwa kuhusu utajiri wao utasikia anasema nilianza na baiskeli sasa
namiliki kampuni kubwa ya mabasi. Mwingine atasema nilianza mama ntilie leo namiliki hoteli kadhaa mjini, mwingine anasema nilianza kushona viatu ila sasa na miliki kiwanda cha viatu, mara nilianza na mtaji wa 20,0000 sasa nina billion 5.

Wanaeleza mambo kana kwamba ni mepesi sana na baadhi ya vijana wasio fikirisha akili yao vizuri wana chukua kama ilivyo wana hamasika wana enda kupambana bila mafanikio, matokeo yake wanakata tamaa zaidi. Jamani kama alivyo wahi sema Mh raisi mstaafu Jakaya Kikwete kwamba akili za kuambiwa changanya na za kwako hii ni muhimu sana.

Nyie mna mtizamo gani ndugu wanabodi.

IMG-20230428-WA0032.jpg
The secret remains the secret.
 
Ni kwasababu mara nyingi utajiri wameupata kwa njia za panya, yaani kihalifu

Mhalifu hawezi kukiri ni mhalifu kirahisi, si ndio?

Lakini nilichogundua ni kwamba kuna patterns flani utazisikia kwa matajiri wengi; kukwepa kodi, kutakatisha fedha, kutumia milango ya siasa nk
Mfano niliwahi kusikia mo alitumia connections zake za kisiasa kununua makampuni kwa bei ndogo kipindi cha mkapa
Au kuna hii taarifa ya rostam kutaka kutawala sekta ya madini kwa kulazimisha makampuni yamuuzie hisa nyingi

Hizo njia za kihalifu pia ni ngumu, kwahiyo kazi kazi usidhani kuna kitonga popote. Ukifanya uhalifu unarisk kunyea ndoo.

Pia nasikia kuna kiwango cha utajiri unaweza pata kwa njia halali, na kuna kiwangi ambacho huwezi kukipata bila kuwa mhuni, ila sijui ni viwango gani.

Na mpaka ufikie hiyo level ya kutakatisha hela, kutumia wanasiasa, maana yake unazungusha hela kubwa kwahiyo hapo nyuma kuna kamsoto ka kuanzia.

Sema asilimia kubwa ya matajiri huwa wametoka kwenye familia zenye uwezo...

Ukifuatilia jinsi wamarekani wanavyowachukulia billionaires nchini kwao utaelewa zaidi
 
Back
Top Bottom