JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Uchaguzi ikiwemo Kugombea Nafasi mbalimbali na Kupiga Kura ni hatua muhimu za Kidemokrasia na huchangia kuleta Mabadiliko ya Mifumo ya Utawala
Je, huwa unashiriki katika Michakato hiyo? Kama haushiriki ni kwasababu gani?
Kwa maoni zaidi, shiriki katika Mjadala utakaofanyika kupitia XSpaces ya JamiiForums siku ya Alhamis Julau 4, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku
Kushiriki Mjadala jamii.app/VijanaNaUchaguzi
=====
06:04pm: Mjadala umeanza na umefunguliwa na Jamiiforums ambae anaanza kuzielezea Jamiicheck na Fichua Uovu na anamkaribisha Hussein Melele, mkurugenzi wa Mulika Tanzania kuendesha mjadala.
Baada ya kuilezea taasisi anayoiongoza, Melele anamkaribisha Ismail Biro kutoka Tanzania Bora Initiative.
Ismail Biro: Ripoti ya sensa 2022 inaonesha takribani 75% kati ya umri ya 35 na kushuka, wadau wakubwa katika uchaguzi wamekuwa ni vijana.
Mwaka 2020 aslimia 50.72 ya waliopiga kura walikuwa ni vijana. Idadi ya waliojitokeza kugombea tuliona kundi la vijana lililojitokeza kutangaza nia lakini sio wengi waliofanikiwa.
Chini ya 30% ya wabunge bungeni ni vijana walio chini ya miaka 40.
Changamoto kubwa inayokwamisha Vijana kushiriki katika Siasa ni Uhamasishaji
Michakato ya Uhamasishaji inafanyika wakati au kipindi cha Uchaguzi tuu na kuwafanya Vijana kutokuwa na mwamko wa kushiriki
Pengine Jitihada za Uhamasishaji kabla na wakati wa Uchaguzi zingekuwa zinafanyika wakati wote mambo yangekuwa tofauti.
Kingine ni suala la Ukosefu wa Ajira. Kuna tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na waathirika wakubwa ni Vijana
Zaidi ya 60% ya Vijana hawana ajira
Hii inawafanya wakate tamaa, wanaona hata wakishiriki Siasa haina maana
Abdul Nondo: Napongeza mjadala, katika uchaguzi wa mwaka 2000 unaonesha ushiriki nkubwa wa vijana, 84% waliweza kushiriki kupiga kura.
Uchaguzi wa Mwaka 2020 waliandikishwa watu takriban Milioni 29 na nusu yao walikuwa ni Vijana. Wengi ambao hawapendi kupiga kura ni vijana.
Mifumo ya kiuchaguzi ipoje
Mifumo yetu ya Siasa ndio inayokwamisha Vijana kutojihusisha na Siasa
Mtu anakwenda kupiga kura anaona mtu wake hashindi, anazuiwa kupiga kura, anaona vurugu au Wakala anaondolewa
Mtu huyo anahesabu kura yake, kwamba haiwezi kuleta mabadiliko.
Tunachohitaji ni Sheria imara, Katiba imara ili kuongeza ushiriki wa Vijana kwenye Siasa na waweze kuwachagua Viongozi wanaowataka
Tunaenda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, watu bado wanawaza "tunaenda kwenye uchaguzi na mgombea wangu hashindi"
Tuangalie mifumo yetu, katiba yetu, ni namna gani tunaweza kurekebisha haya
Ukosefu wa ajira unazuia Vijana kushiriki Siasa kwasababu wana disatifications, hawaridhishwi na vitu vingi.
Pia hawana kazi, wako busy na maisha yao kujipambania. Wanaona Siasa sio sehemu ya maisha yao.
Eugene Kabendera(Chauma): Naibu Katibu Mkuu Bara-CHAUMA: Chaguzi za Tanzania zimetawaliwa na Pesa. Pesa inatumika sana kipindi cha Uchaguzi
Na vijana wengi hawana pesa. Chaguzi za Vyuoni na kwengine ambapo hazihusishi pesa Vijana wanashiriki na wanachaguana
Lakini hizi nyingine zinazoamua nani anakuwa nani na zinazohusisha pesa vijana hawashiriki, wanabaki kuwa Machawa kwasababu hawana pesa.
Pia Vijana wamekubali kupangwa Kuna nafasi huko watu wanaambiana mwachie mwachie huyu.
Kwa nini kupangana? Watu waachwe wachague mtu anayemtaka. Kama kiongozi anakubalika si anapigiwa kura?
Shamira Mshangama(Mwanamke na Uongozi): Elimu ya Uraia inahitajika sana na pia inapaswa kuakisi uhalisia. Uhitaji wa Elimu hii ni Mkubwa lakini utoaji bado ni mdogo
Taasisi nyingi zinajitosa kutoa elimu hii Dar au maeneo ya Mijini. Kuna vitu ambavyo vinakwamisha utoaji wa Elimu ya Uraia nchini hasa utoaji wa vibali
Unakuta Taasisi fulani inauwezo wa kutoa elimu lakini wanashindwa kwa kukosa vibali. Pia resources, wafadhili bado ni wachache na Vijana ni wengi sana.
Ushiriki wa Vijana hasa Wanawake katika Siasa bado ni hafifu sana Nchini
Na sababu kubwa ni Ukatili wa Kijinsia, pia Rushwa ya ngono. Hivyo katika Mijadala hii ni muhimu kujadili namna ya kuwasaidia hawa Wanawake.
Ruqaiya Nassir: Naibu Katibu Ngome ya Vijana Taifa, ACT Wazalendo: Tunahitaji Sheria nzuri zinazofanya kazi ili kuongeza Ushiriki wa Wanawake katika Siasa
Tumekuwa tunaongelea Sheria ya 50/50 lakini tumeahindwa kuhakikisha inafanya kazi.
Elisante Ngoma: Mfumo wetu wa Kisiasa na Kiuchumi tangu Uhuru umetulia kwamba ni ngumu Vijana kushiriki katika Siasa
Kuna wanaojiandikisha na hawapigi kura. Vijana wengi wanaona kushiriki masuala ya kisiasa haiwahusu
Tofauti na Majirani zetu kama Kenya na wengine wanaojua Siasa ni sehemu ya maisha yao
Mfumo wa Kijamaa ulifanya kuhoji kuonekane ni kukosa adabu. Hata huko kwenye Vyama unaona Vijana wakija na wazo lao wanapingwa
Hii inawafanya Vijana wasiwe active katika Siasa
Clinton: Vijana wengi wanateseka na Mgogoro wa Kiuchumi. Hivyo mawazo yao ya kibunifu yakofika mezani yanazuiwa na wakubwa, na yamekuwa yakozuiwa kwa kukosa nguvu ya kiuchumi
Pia Sera za Uchumi za Nchi haziwahusishi vijana. Vijana huko kwenye Vyama wanabebwa, sio kwasababu ya kuwa innocative
Kenan Kihongosi: Ambalo nimeona katika mjadala, sisi kama vijana, moja hatujiamini hasa katika malengo ya kisiasa. Pili vijana wengi hatushirikiani, hatupendani. Kwa experience, unakuta kuna kijana ana ndoto ya kugombea au kiongozi, wanaopinga huyo kijana ni vijana wenzake.
Vijana wote lazima wawe na mshikamano bila kujali itikadi, mimi nampenda mfano Abdul Nondo, Ngoma, Pambalu.
Tatu, zinapotokea nafasi za uongozi twende tukagombee bila kuangalia mifuko yetu.
Aisha Madogo: Mitandao ya kijamii in ‘impact’, pia Vyama vya Siasa ana Wadau wengine wote wanaohusika na Siasa wanatakiwa kutumia ‘platforms’ za Mitandaoni kufikisha ujumbe na elimu kwa Vijana.
Kuwapata Vijana ana kwa ana wakati mwingine ni ngumu kutokana na mazingira na hali ya Uchumi wetu, mfano Bodaboda hawezi kuacha shughuli zake aende kwenye mkutano
Hivyo, tunaweza kubadili Siasa zetu na kuzifanya Kidigitali, hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wao.
Mwaka 2015 nilikamatwa wakati nasikiliza Mgombea, nilikaa ndani kwa siku nne hadi Tano, hapo namaanisha kuna mazingira ya kutishana kutoka kwa Vyombo vya Usalama
Unadhani mtu anapokutan na tukio kama hilo unadani kesho yake atakuwa na moto wa kuendelea kushiriki kwenye Siasa?
Vijana wanapokutana na vitisho wanarudi nyuma, ijulikane pia hali hiyo itarudisha nyumaa Vijana wa vyama vyote bila kujali ni CCM au Upinzani, suala la vitisho halifai na ni moja ya chanzo cha kurudisha nyuma ushiriki wa Vijana kwenye Siasa.
John Pambalu (Mwenyekiti BAVICHA): Kijana mwenye umri wa Miaka 18 anaruhusiwa kupiga Kura lakini haruhusiwi kugombea, hili ni tatizo la Kikatiba na linachangia kuwarudisha nyuma Vijana, kwanini Mtu awe na uwezo wa kuchagua Kiongozi wake lakini hawezi kuchaguliwa, hilo ni tatizo.
Suala la Umri wa kugombea Urais kwamba hadi ufikishe Miaka 42 ndio unaruhusiwa kugombea nalo linaweza kuwa kikwazo, Nchi nyingine za wenzetu wamerekebisha hilo na kuruhusu umri wa kugombea uanzie Miaka 35
Unapofikisha Miaka 35 na kuonesha nia ya kugombea inamaanisha upo tayari na umejiandaa, nashauri umri urekebishe katika vipengele vya kugombea Urais.
Suala lingine ambalo haliandikwi au kuzungumza sana ni kuulizwa suala la kama ‘umeoa’ wakati unapoonesha nia ya kuwania uongozi wa Kisiasa
Mara nyingi maswali ya aina hiyo yametawala zaidi Vijijini kwa kuwa nimekutana nayo, ni maswali au vizingiti ambavyo vinakera na vinawalazimisha Vijana wakae pembeni.