Nini siri ya Bashungwa kuhamishwa Wizara kila mara?

Hahahaaa na hana mvuto haya maisha kuna watu ni dawa acha tuone zaidi yajayo
 
Wakuu salama

Innocent Bashungwa ambaye jana ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi amekuwa Waziri anayehamishwa Wizara mara nyingi sana. Nini hasa kipo nyuma ya Bashungwa kuhamishwa Wizara kila mara?

Ukiangalia tangu atotolewe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara mnamo Juni 8, 2019 hadi sasa amekuwa Waziri katika Wizara 5 (Kipindi cha miaka 4).

Kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara ndio Wizara pekee alikaa kwa zaidi ya mwaka moja.

Juni 8, 2019 - aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara (miezi 22)

Machi 31, 2021 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo (miezi 9)

Januari 8, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) (miezi 9)

Octoba 2, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (miezi 11)

Na jana Agosti 30, 2023 Rais Samia amemteuwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Nini siri ya Bashungwa kuhamishwa kwenye Wizara hizi? Hii ya sasa atamaliza mwaka?
Domo zege huyu bwana mdogo!
 
This underground gentlemen, is among the most powerful individuals within the gov as well as within the ruling party.
ni hatari kumuacha nje ya mfumo.
Nguvu yake hasa ipo kwenye nini huyu Mtu hadi iwe namna hii?
 
Unaulizia bashungwa mbona huulizi simbachawene , pindi chana mkuchika n.k
Yaani kama watu wameshindwa ni bora kuchukua wengine kuliko watu wale wale kuwazungusha kila baada muda mfupi ni kama wanafanyiwa ‘trial and error’ matokeo yake kwenye Wizara wanaanza jambo hawamalizi wanaondoka na mwingine akija anaanza yake
 
Nguvu yake hasa ipo kwenye nini huyu Mtu hadi iwe namna hii?
mwerevu hatoi siri za nguvu, uweza na ufalme wake kwa adui au hadharini.
kufanya hivyo ni kumpa nafasi adui akishughulikie vizur.

Huzificha sirini chini ya ulinzi wa Mungu ili kusudi watesi na adui zake wasipate kujua au kupanga cha kufanya dhidi yake.

The gentleman is the most powerful individual within the ruling party and the Government at large.
 
Wakuu salama

Innocent Bashungwa ambaye jana ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi amekuwa Waziri anayehamishwa Wizara mara nyingi sana. Nini hasa kipo nyuma ya Bashungwa kuhamishwa Wizara kila mara?

Ukiangalia tangu atotolewe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara mnamo Juni 8, 2019 hadi sasa amekuwa Waziri katika Wizara 5 (Kipindi cha miaka 4).

Kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara ndio Wizara pekee alikaa kwa zaidi ya mwaka moja.

Juni 8, 2019 - aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara (miezi 22)

Machi 31, 2021 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo (miezi 9)

Januari 8, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) (miezi 9)

Octoba 2, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (miezi 11)

Na jana Agosti 30, 2023 Rais Samia amemteuwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Nini siri ya Bashungwa kuhamishwa kwenye Wizara hizi? Hii ya sasa atamaliza mwaka?
Na sasa amehamishwa tena kwenda Mambo ya Ndani
 
Back
Top Bottom