Nini siri ya machale ya jambo litakalotokea?

Machale yanaendana na kuamini kua nikisikia jicho langu la juu kulia likicheza basi ntasafili safari ya mbali,nikitaka kwenda mahali na mguu wangu wa kushoto ukawa kama hautaki kunyooka vzr basi nikilazimisha kwenda ntapata ajali,machale ni ishara ya jambo linalokuja mbele yako liwe baya au zuri.lakini naomba Mshana Jr atie miguu hapa fasta
 
asante kwa mchango wako wa mawazo.
 
hhuyo anaitwa pepo wa uaguzi na kwenye biblia kaandikwa
 
Kwanini watu wengine huwa na machale juu ya jambo baya liwezalo kumtokea au tayari linamtokea wakati huo huo. Hata wengine utasikia akisema "Moyo wangu unauma" wakati huo huo anadai kumkumbuka mtu wa karibu kama vile mke au mme wake akihisi kumfanyia jambo baya lolote.

Mtu mwingine utasikia akisema sina amani kabisa kusafiri leo, anaahirisha kusafiri lakini baadae utasikia basi ambalo angesafiria limepata ajari mbaya hata kuua au kuumiza watu. Maswali yangu ni,

1.Je Nguvu ya machale hutoka kwa Mungu au wapi?

2.Je Watu wote wana machale au ni baadhi tu ya watu wana uwezo huo.

3.Je kuna njia ya mtu kukuza uwezo wa machale yake.

Binadamu ameumbwa na uwezo mkubwa wa kutambua mambo yaliyobeba nje ya mwili kwa njia ya kiroho lakini vilevile mwili una natural defense ambayo ina uwezo wa ku foresee hatari au kheri ijayo, kinachotuangusha wengi ni hizi harakati za maisha zinazofanya ufahamu wetu utawanyike huko na huko na kukosa nguvu ya kuweza kufanya kazi yake sawasawa
Kuna watu wenye ufahamu wenye nguvu kwamba pamoja na kutawanyika lakini bado ile nguvu ya ku foreseen inabaki palepale, meditation na elimu za utambuzi ni vichocheo muhimu sana kuendeleza machale ambayo yanatokana na sixth sense
 
Kila mtu ana huo uwezo ila inabidi uendelezwe. hapo mwanadamu hua anatumia sub-concious minds, uwezo ambao wataalam wetu hawana maneno rahisi ya kuuelezea
 
Sixth sense?kuona,kusikia,kugusa,kuonja na kunusa,hiyo sixth sense ni ipi mkuu!
 
Kila mtu ana huo uwezo ila inabidi uendelezwe. hapo mwanadamu hua anatumia sub-concious minds, uwezo ambao wataalam wetu hawana maneno rahisi ya kuuelezea

Ni hivi sub conscious mind ni ile hali ya mwili kuwa live lakini at total rest mood, kama kulala....hakuna kinachofanya kazi kwa wakati huo zaidi ya msukumo wa damu na busy mind
Hata hali ya kuzirai inaingia kwenye hali ya kuwa sub conscious mood
Kwenye mind kuna conscious mind hii ambayo unafanya kila kitu na sub conscious mind ambapo kinachofanya kazi ni mind pekee huku viungo vingine vyote vikiwa domant
 
Machale yanakuwa active sana utotoni mpaka age ya miaka 7 (kwa sie wa ukuaji wa zamani, sio kizazi cha microwave ). Baada ya hapo mazingiira na elimu huyafanya Machale yabanwe na kuondoka kwenye ufahamu. Ila kama ukipractice unaweza kuyarudisha
 
Kuna kipind hizi mambo zilikukuwa zinanitokea sana, ilikuwa kuna wakati nakikaa wazo Fulani likinijia tu bac lazma hicho nilchokiwaza kitokee au nikilala then nikaota bac lazima nilichokiota kitatokea. Sasa hz hisia zmepotea aisee
 
Daaah! Hata mimi nimejaribu hiyo mediteshen mzee,lkn inanishinda kwani tatizo langu siwezi kukaa bila kuwaza,kila dk nafungua macho,ila nahisi ni hii serkali ya mwendokasi hainipi nafasi ya kurelax! Mshana Jr. itabidi anipe darasa zaidi!
Huwazi??

Kwani meditation inahusu kukaa bila kuwaza? Au ni ku concentrate na kile unacho kiwaza ... isije kuwa mimi ndo nachanganya

Msaada tafadhali kwa wanaofahamu
 
Kwanini watu wengine huwa na machale juu ya jambo baya liwezalo kumtokea au tayari linamtokea wakati huo huo. Hata wengine utasikia akisema "Moyo wangu unauma" wakati huo huo anadai kumkumbuka mtu wa karibu kama vile mke au mme wake akihisi kumfanyia jambo baya lolote.

Mtu mwingine utasikia akisema sina amani kabisa kusafiri leo, anaahirisha kusafiri lakini baadae utasikia basi ambalo angesafiria limepata ajari mbaya hata kuua au kuumiza watu. Maswali yangu ni,

1.Je Nguvu ya machale hutoka kwa Mungu au wapi?

2.Je Watu wote wana machale au ni baadhi tu ya watu wana uwezo huo.

3.Je kuna njia ya mtu kukuza uwezo wa machale yake.

Machale yapo ya kutoka kwa Mungu na yapo ya kutoka kwa Shetani, inategemea na Aina ya Maisha yako unayoishi. Ukibahatika ukapata ya kutoka kwa Mungu basi ujue umefanikiwa na umepata bahati na zawadi kubwa. Wapo watu wengi wanayo machale ya kutoka kwa Mungu ila si rahisi kujitangaza na huwezi kuwajua, wengi wao ni watu wanaopenda kujishusha. Na si lazima uwe kiongozi mkubwa wa dini ili uweze kupata zawadi hiyo kwa wale wapenzi wa masuala ya dini. watu wenye machale unaweza kuwajua kwa maneno na matendo yao. Mfano inaweza kutokea akatoa ushauri mkaukataa, ila anaweza asiwalazimishe lakini jambo hilo akalifanya peke yake [ukitaka kujua kuwa ana machale au la muulize akiwa peke yake madhara ya kutofuata ushauri huo] ( LAKINI si wote wanaofanya hivyo wana machale, isipokuwa ni dalili mojawapo ya watu hao).
 
Kwa waoga mno hii kitu ipo, its defensive mechanisms.

Pia sometimes ni kwa wenye elimu au kufikiri mno.

Ni jambo zuri linaufanya ubongo utumike kiasili katika kupambana na mazingira husika.
 
Mkuu asante kwa mada nzuri. Ukijifunza kidogo kuhusu Anthropology utapata majibu ya maswali yako yote. Anthropology ni elimu ihusuyo mwanadamu. Kwa kifupi mwanadamu anagawanywa ktk sehemu kuu tatu ( 3 ) za mwili , nafsi na roho. Ni ktk roho nd'o kuna kitu kinaitwa `` Intuition '' hii ni uwezo wa kufanya maamuzi bila kutumia akili. Yaani ktk intuition hakuna reasoning , mantic au logic. Ni uwezo ambao kila binadamu anao. Namna ya kuuchochea uwezo huo ambao mtoa mada umeuita '' machale '' kitaalam huitwa intuition; ni utulivu na aina za ibada kutegemea na imani ya mtu. Kwa wakristu hili ni eneo ambalo huliita maskani ya Mungu ( God's indwelling place or the home of God ) na hivyo wakristu hulichochea kwa sala na maombi hasa kwa Roho Mtakatifu. Kwa wale wanaoamini kwenye uchawi na ushirikina huwa wanadhani ni uwezo wa kichawi na nd'o maana kwa kuwa uchawi na ushirikina mara nyingine huhusisha kuchanjwa chale mwilini nd'o maana wanaita huo uwezo '' machale ." Naomba kuwasilisha .
 
Machale yapo ya kutoka kwa Mungu na yapo ya kutoka kwa Shetani, inategemea na Aina ya Maisha yako unayoishi. Ukibahatika ukapata ya kutoka kwa Mungu basi ujue umefanikiwa na umepata bahati na zawadi kubwa. Wapo watu wengi wanayo machale ya kutoka kwa Mungu ila si rahisi kujitangaza na huwezi kuwajua, wengi wao ni watu wanaopenda kujishusha. Na si lazima uwe kiongozi mkubwa wa dini ili uweze kupata zawadi hiyo kwa wale wapenzi wa masuala ya dini. watu wenye machale unaweza kuwajua kwa maneno na matendo yao. Mfano inaweza kutokea akatoa ushauri mkaukataa, ila anaweza asiwalazimishe lakini jambo hilo akalifanya peke yake [ukitaka kujua kuwa ana machale au la muulize akiwa peke yake madhara ya kutofuata ushauri huo] ( LAKINI si wote wanaofanya hivyo wana machale, isipokuwa ni dalili mojawapo ya watu hao).

Unaweza kuthibitisha hizi porojo zako
 
Back
Top Bottom