Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Kuna siri kubwa sana chini ya majina tunayotumia humu JF pamoja na avatar zetu (wale wanaotumia picha zisio zao).

Kwanini uliamua kujiita A na sio B?!
Kwanini a jina feki na sio jina harisi?!

Nadhani nianze na mimi mwenyewe, sizzya007 ni jina modified kidogo, hapo zamani nilikuwa natumia sizya007 humu jf ila nilipobadili device nikawa nimesahau password ikanibidi nifungue acc mpya na kutumia sizzya007, jina hili linatokana na mizuka na mahaba mazito ambayo nilikuwa nayo kwa movie za James Bond. Toka enzi hizo za VHS, mie nilikuwa nazo movie nyingi sana za huyu mwamba! Basi rafiki na ndugu wa karibu walianza kuniita 007, nilivyofika chuo wale nilioachana nao primary ndio wakaliibua upya, ila muda huu ndio likaja na sizya007🙄

Hili ni jina ambalo nalitumia mitandao yote ya kijamii ambayo nipo, ila kwingine nimelifanyia utundu kidogo.

Sasa, natamani kujua majina ya wengi humu jf atleast origin yake ni nini hasa! Nitamzungumzia mmoja tu ambaye huyu nadhani itabodi alifafanue lake kwani limekaa kifigisufigisu, GENTAMYCINE😱😱

GENTAMYCINE, nikujaribu kulinyumbua napata ukakasi, GENTA MY CINE😳
Why should i GENTA your CINE?! And what is CINE?! Na kuGENTA ndio kufanya nini😱😱

Cc GENTAMYCINE njoo ujibu, jina liko kifigisufigisu sana hili.

Wengine ni
Faizafoxy
TheBoss
Lara1
Rubii
Bitoz
Miss chagga
Bansenburner
Mshana jr
YEOHANDA
perry
tatty
cute b
Evelynsalt
Stroke
Nyani Nyabu
Mwanakijiji
Mwanahabari huru
Mzama chumvini
Nahree

Na wengine kibaaao, ebu funguka kidogo kwanini unatumia jina hilo?!

🙄🙄

!
!
Threesixteen himself..... Nilikuwa nampenda sana mcheza mieleka mmoja aliitwa Stone Cold Steve Austine threesixteen himself.... Sasa yule comentator alikuwa anataja vizuri mno na kuongeza himself mbele. Kwa muda mrefu nimeitwa teacher threesixteen hasa mshkaji wangu mmoja hivi mwarabu. Nilipokuja huku sikupenda hilo la teacher kwani sio mwalimu tena ndio nikaona nitumie hili la threesixteen himself. Hiyo avatar ni ya king Julien wa movie moja ya Penguins of madagascar. Naipenda sana hiyo cartoon.
 
Huu uzi umenivutia cjui ni hzi story za wananchi. Nweiz mi jf nmeijulia ukubwani lakini i loved the mystery ya kwamba hamjuani majina wala sura hence the name siri hyo 123 mbwembwe. Avatar yangu ni ya mtoto napenda watoto wazuri wazuri japo nlikua mbaya utotoni hahahahah copy ya mzee
 
avatar ni mimi mwenyew, mara yakwanza kuna jina nilikua natumia, baada ya kuchange device nikasahau paswrd ikabidi nitumie hili makwiku,

chanzo cha mabwiku kuna siku nilikua na bro wangu seblen, sasa sijui alinitania nn nikachukia sasa mdogo wangu wa kike akaninong'oneza kua nimuite (mabwiku)

Nilimuita alichukia kinoma, sasa toka hapo nikapenda hilo jina japo sijuagi maana yake, nilipojaribu username nyingi zikawa zimetumika ikabidi nitumie mabwiku ili nisisahau tena.
 
Owkey ni hivi.
nilikuwa na kajamaa flan hivi enzi za ujana..kalikuwa kachuchu kangu basi akawa anafupisha jina langu la kinyumbani...akawa ananiita Tatty..ikawa hivyo. Friends mpk familia yake hasa mama yake (Mungu amrehemu) waliniita Tatty. That was 17 years ago.
Hiyo avatar...sifanani sura na hiyo pic..ila skin na nywele kiasi vinafanana.
Mara nyingi nikisoma username name yako tatty huwa najichanganya nakujikuta nasoma 'Teti' jina la mkuu wa shule mmoja ambaye naamini kama ana kitabu cha kumbukumbu ya wanafunzi wake waliomsumbua sana jina langu lazima litakuwa bolded na rangi nyekundu...hivyo jina lako unikumbusha mengi sana kuhusu maisha ya shule mkuu.
 
Hahaha....i get that a lot mzee, ila tusubiri tuone, hii ni sura ambayo only a mother can love😀
Mii ungenitafsiria maana ya 007 maana yake na kwanini mtengenezaji aliitumia hiyo kwa akina Sean Connery
Mmm ndio nitakuja na Ukwaju na avatar yangu
 
ISO is my self made nickname. Hizo ni herufi kwenye jina langu halisi.

M.CodD - Master Code Dreamer. My passion. My job description.

Avatar: The Red John Smiley from my favorite series, The Mentalist. You see it, you feel dread. Tiger Tiger.
 
Huu uzi umenivutia cjui ni hzi story za wananchi. Nweiz mi jf nmeijulia ukubwani lakini i loved the mystery ya kwamba hamjuani majina wala sura hence the name siri hyo 123 mbwembwe. Avatar yangu ni ya mtoto napenda watoto wazuri wazuri japo nlikua mbaya utotoni hahahahah copy ya mzee

Utotoni wote tulikuwa wabaya asee!!! Ila afadhali huku ukubwani kidogo alhamdu😀😀😀
 
avatar ni mimi mwenyew, mara yakwanza kuna jina nilikua natumia, baada ya kuchange device nikasahau paswrd ikabidi nitumie hili makwiku,

chanzo cha mabwiku kuna siku nilikua na bro wangu seblen, sasa sijui alinitania nn nikachukia sasa mdogo wangu wa kike akaninong'oneza kua nimuite (mabwiku)

Nilimuita alichukia kinoma, sasa toka hapo nikapenda hilo jina japo sijuagi maana yake, nilipojaribu username nyingi zikawa zimetumika ikabidi nitumie mabwiku ili nisisahau tena.

That one thing about families, huwa kunakuwa na matani yasiyo na mwisho na vimajina vya hapa na pale ambavyo nobody ever knows the origin, utotoni nilikuwa naita kimbo😱😱

Sikawai kujua kimbo lilitokana na nini mpaka leo hii😱
 
Mii ungenitafsiria maana ya 007 maana yake na kwanini mtengenezaji aliitumia hiyo kwa akina Sean Connery
Mmm ndio nitakuja na Ukwaju na avatar yangu

007 ndio alikuwa the most dangerous agent ktk british secret agency hiyo, so huyo ndo alikuwa anatumwa zile deadly missions, wako maagent wako wengi ila wengine nahisi walikuwa wazembe tu...ukweli with a bit of chumvi
 
Bitoz ni jina nililopewa skul na kitaani kutokana na uvaaji wangu......yaani kuanzia uniform hadi kitaani sikubali kufanana na mtu .....kupiga pamba vizuri ni kipaumbele changu japo mimi ni KAPUKU....

Avatar inawakilisha
* kutangaza utalii
* Tembo bishoo
*kupinga mauaji ya tembo

NIMEELEWEKA
#Team Kapuku.
 
Back
Top Bottom