Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Hahahaha Id name ni majina yangu yote hapo ila nimecheza na herufi tu plus bond yangu,Avatar hii nimependa tu maneno na dressing style,ila kuna ile avatar yangu ndo naipenda sana ileeee ya Aishrywa anakunywa wineee ile ndo ina story behind,wewe mtoto wa Juzi Juzi huijui hiyo Avatar.
Hahhaaaa kumbe alikuwa bado hajazaliwa ila ile avatar irudishe
 
Iramba ni Wilaya Moja Wapo Kati ya Wilaya Sita za Mkoa Wa Singida!
Nimejiita Iramba Ili Kukidhi Haja Yangu ya Kuitangaza Wilaya Yangu Pendwa ya Iramba...
Na Pia Kupata Jukwaa la Kueleza Changamoto za Wilaya yangu Maana Mbunge Wetu Mwigulu Kaloea Dar
Poa Go West or East,Home is the Best!
 
Annie Josh (Anna Joshua) siyo majina yangu but ni majina imaginary ya watoto wangu wawili ntakaojaliwa na M/Mungu...Nina Imani atanipa
Nayapenda maana wenye majina hayo wana sifa ya upole na utu Wema mostly wacha Mungu.

Behind my avatar ... I used to trust human beings much! Sikujua binadamu aweza kuwa na tabia Za kinyama au kumtendea binadamu mwingine yasiyofaa! I came to realize human beings are not to be trusted Kwa niliyoyaona Kwa dada yangu! Alitendwa na mumewe yasiyohadithika licha ya kuwa dada yangu aliweka rehani mambo Yake muhimu kwaajili ya Upendo Kwa mumewe...lkn alichotendwa hatokaa asahau!
Pia nami Nimepitia kadhaa yanayonifanya nione sina haja ya kumwamini sana binadamu...naishi naye KIAKILI tuu! But that notion haizuii kuona mema yaliyomo kwenye ubaya mchache wa Mtu
Daah hongera na pole...Joshua ni mtu wa vita ck zote za maisha yako,,,so ujue mwanao atakuwa mtu wa mapito mazito japo atatoboa. ANNA ni aina ya wanawake wenye mapitoazito sana japo nao ni wacha Mungu na wengine ni makahaba 1/2. Ni uchaguzi mzuri japo...
 
I'd yangu haihusiani na chochote kuhusu maisha yangu na mienendo yangu! ila story tu ya kawaida!!
 
Nitairudishaaa......dahhh tushirikishe na wewe Eddy na hiyo Avatar Nini story nyuma yake.
Avatar na jina linawakilisha upenzi wangu kwa katuni niliamua kutumia jina Hilo sababu katuni hiyo inabeba jina langu pia. Ila I'm sad [emoji17] [emoji17] sababu nililikosea badala ya ed edd and eddy nikaliandika hivyo.

Zile figisufigisu za ku-edit jina mwenyewe kushindwa nikawaweka ed edd and eddy kwenye avatar kuwawakilisha my craziest boy's
 
Daah wew kiboko umeisimamia uzi wako hadi inavutia...hongera sn

Mkuu i dont even believe what is happening before me asee!!
Its a phenomenal, yaani ni balaa😱😱
 
Kuna siri kubwa sana chini ya majina tunayotumia humu JF pamoja na avatar zetu (wale wanaotumia picha zisio zao).

Kwanini uliamua kujiita A na sio B?!
Kwanini a jina feki na sio jina harisi?!

Nadhani nianze na mimi mwenyewe, sizzya007 ni jina modified kidogo, hapo zamani nilikuwa natumia sizya007 humu jf ila nilipobadili device nikawa nimesahau password ikanibidi nifungue acc mpya na kutumia sizzya007, jina hili linatokana na mizuka na mahaba mazito ambayo nilikuwa nayo kwa movie za James Bond. Toka enzi hizo za VHS, mie nilikuwa nazo movie nyingi sana za huyu mwamba! Basi rafiki na ndugu wa karibu walianza kuniita 007, nilivyofika chuo wale nilioachana nao primary ndio wakaliibua upya, ila muda huu ndio likaja na sizya007🙄

Hili ni jina ambalo nalitumia mitandao yote ya kijamii ambayo nipo, ila kwingine nimelifanyia utundu kidogo.

Sasa, natamani kujua majina ya wengi humu jf atleast origin yake ni nini hasa! Nitamzungumzia mmoja tu ambaye huyu nadhani itabodi alifafanue lake kwani limekaa kifigisufigisu, GENTAMYCINE😱😱

GENTAMYCINE, nikujaribu kulinyumbua napata ukakasi, GENTA MY CINE😳
Why should i GENTA your CINE?! And what is CINE?! Na kuGENTA ndio kufanya nini😱😱

Cc GENTAMYCINE njoo ujibu, jina liko kifigisufigisu sana hili.

Wengine ni
Faizafoxy
TheBoss
Lara1
Rubii
Bitoz
Miss chagga
Bansenburner
Mshana jr
YEOHANDA
perry
tatty
cute b
Evelynsalt
Stroke
Nyani Nyabu
Mwanakijiji
Mwanahabari huru
Mzama chumvini
Nahree

Na wengine kibaaao, ebu funguka kidogo kwanini unatumia jina hilo?!

🙄🙄
mkuu picha uonanayo hapo ni yangu mwenyewe nilipiga bene beach kule Entebe Uganda...... na jina hapo ni sir name yangu ya Msumeno.... kwa kinyamwezi tunaitwa bha mgana msumeno... yaani koo au familia ya msumeno full stop mimi sio mwizi mpaka nifiche sura yangu
 
mkuu picha uonanayo hapo ni yangu mwenyewe nilipiga bene beach kule Entebe Uganda...... na jina hapo ni sir name yangu ya Msumeno.... kwa kinyamwezi tunaitwa bha mgana msumeno... yaani koo au familia ya msumeno full stop mimi sio mwizi mpaka nifiche sura yangu

Ja milimo?! Mie ni wa nzega kijiji cha busondo.....pale ambapo vitunguu hulimwa sana, nice to meet u distant kin😀
 
Back
Top Bottom