Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Duh zitafika Kama zako kweli[emoji17] [emoji17] [emoji17] ila nazipenda itabidi nivumilie
Zitafika kwasababu hata zangu zilianzia chini kabisa tena walikuwa wananiambia nizitoe maana hazinipendezi ziko kama inzi
 
Ngoja niendelee kuguess tu itakuwa Edison. .......hahhahah wewe danganya tu si umeshakataaa halipo pale basi zawadi ya ushindi ishakupita....
Hahaha sawa kwa kuninyima zawadi ....
Unazidi kupotea kasikilize story 3 ya Jay Mo kama mpenzi wa muziki
 
Ha ha ha, jamaa anaelezea tukio unamsoma mtu na anakuwa kama mshikaji wako. Mimi nilimwelewa sana Salvatore Guiliano kwenye The Sicilian, nilisikitika sana jinsi kifo chake kilivyotokea, kuuawa na jamaa yake Pisciota ambaye wamekuwa naye toka utotoni, mtu ambaye alimwamini sana ndiye aliyemgeuka.

Nadhani kwenye Novel zake zote, Godfather was the best of the best, kuanzia theme mpaka characters. Mpaka sasa nikiwaza Mafia namwaza Don Corleone, pamoja na Madon wote aliowahi kuwataja kwenye novel zingine lakini navutiwa sana na Godfather, hata alivyokuja ku-take over Michael bado naona ilikuwa ndo nzuri sana.
Yeah thats true bro,the Godfather was the best maana hiyo ndio inayoaanza kutupa the story of a fictitious Mafia family na kazi zake zilizofuata ilikuwa ni kama muendelezo wa the Godfather......salute kiongozi maana inaonyesha na wewe ni crazy wa hii makitu...😎
 
Yeah thats true bro,the Godfather was the best maana hiyo ndio inayoaanza kutupa the story of a fictitious Mafia family na kazi zake zilizofuata ilikuwa ni kama muendelezo wa the Godfather......salute kiongozi maana inaonyesha na wewe ni crazy wa hii makitu...😎

Hizi Novel za jamaa nazirudiaga mara kwa mara sana. Halafu kila nikirudia kunakuwa kama vile kuna vitu sikuviona mwanzo. Godfather ni novel kubwa sana na nadhani ndiyo iliyompa mafanikio makubwa sana, nawakumbuka kina Fanucci, Clemenza, Tersio, Sony, etc.

Zile novel zinafundisha hustle na zinaelezea kinsi mifumo ya nchi inavyokuwa chini ya matajiri, nikifanya link ya jinsi kina Rostam wanavyoikimbiza nchi naona kama Godfather vile.
 
Jina hili la KATA KUCHA ninalotumia humu lilitokana na kufurahishwa na jamaa mmoja aliyekuwa akifanya biashara yake Ubungo Mataa.

Kuna siku tukiwa kwenye foleni tukisubiri kuruhusiwa huku nikiwa nimejiinamia kwenye siti kwa uchovu baada ya kukaa foleni muda mrefu, mara huyu jamaa mfanyabiashara akafika dirisha akinadi bidhaa yake "....kata kuchaaaaaa...nauza kikata kuchaaa....." kwa sauti ya mkwaruzo kidogo.

Wote tulokuwa kwenye gari tukageuka kutazama aina ya 'vikata kucha' anavyoviuza. Kuhamaki kumbe jamaa amebeba MAJAMBIA yanang'aa mno na makali haswa na ndio bishara yake. Sote ndani ya gari tulicheka sana kwa namna hivyo vikata kucha vilivyo.

Alikuwa akitumia lugha ya kuficha ukali wa maneno badala ya kunadi " nauza jambia" yeye aliita vikata kucha. Na ndio ID yangu. Maana alinisogezea "vikata kucha" vyake karibu zero distance na nilipokaa kuhamaki kumbe ni Jambia.
hahaha huyo jamaa na mm nilimsikia,,yani anavoita utadhani ana viwembe kumbe ana masime na mavisu
 
Jina...avatar vyote nadhani vina thread zake miaka ya nyuma...hizi thread
 
Back
Top Bottom