Jina hili la
KATA KUCHA ninalotumia humu lilitokana na kufurahishwa na jamaa mmoja aliyekuwa akifanya biashara yake Ubungo Mataa.
Kuna siku tukiwa kwenye foleni tukisubiri kuruhusiwa huku nikiwa nimejiinamia kwenye siti kwa uchovu baada ya kukaa foleni muda mrefu, mara huyu jamaa mfanyabiashara akafika dirisha akinadi bidhaa yake "....kata kuchaaaaaa...nauza kikata kuchaaa....." kwa sauti ya mkwaruzo kidogo.
Wote tulokuwa kwenye gari tukageuka kutazama aina ya 'vikata kucha' anavyoviuza. Kuhamaki kumbe jamaa amebeba MAJAMBIA yanang'aa mno na makali haswa na ndio bishara yake. Sote ndani ya gari tulicheka sana kwa namna hivyo vikata kucha vilivyo.
Alikuwa akitumia lugha ya kuficha ukali wa maneno badala ya kunadi " nauza jambia" yeye aliita vikata kucha. Na ndio ID yangu. Maana alinisogezea "vikata kucha" vyake karibu zero distance na nilipokaa kuhamaki kumbe ni Jambia.