Mimi niliamua kufungua akaunti jf kwa jina hili na avatar hii kwa sababu
Kaka yangu alikuwa na simu fulani hivi NOKIA 1280
Kwenye Ile simu mbele ya kioo alikuwa ameandika T 1986 BUL
Siku moja nilimuuliza kuwa anamaanisha nini kuandika hivyo kwenye simu yake
Akanijibu kuwa T ni TANZANIA na 1986 ni mwaka wake wa kuzaliwa na BUL ni kifupisho cha jina langu
Sasa bhasi na Mimi T namaanisha ni TANZANIA na 1990 ni mwaka wangu wa kuzaliwa na ELY ni kifupi cha jina langu
Kuhusu Avatar hiyo ni Mimi mwenyewe yaani sura yangu kabisa iliyotukuka isiyokuwa na mashiko.