Nini tafsiri ya mabinti kuzaa wakiwa bado wapo kwa wazazi?

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,981
Reaction score
4,170
Hili halikuwepo miaka ya 90s kurudi nyuma, sisemi kwamba haikuwa ikitokea, la hasha! bali hata kama ilikuwa inatokea basi ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na ilivyo sasa.

Katika maeneo ninayokuwa hasa kwa watu mbalimbali ninawafahamu, jambo hili linaonekana kukuwa zaidi ya mara dufu na inavyoonekana hali ikazidi huko mbele ya safari.

Mabinti wengi wanaozaa wakiwa bado hata hawajaposwa wamekuwa wakiwaacha watoto wao wakilelewa na babu&bibi huku wakiendelea masuala yao ikiwemo kuendeleza uhusiano na wanaume ambao unapelekea kuongeza idadi ya watoto kwa wazazi bila kujua ugumu wa kulea watoto.

Wanaume wamekuwa wakiwazalisha mabinti bila kuwaoa wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kulea badala yake mwanamke ndio anaachiwa jukumu la uangalizi wa mtoto ambaye naye anakabidhi majukumu kwa wazazi wake! kimsingi wazazi hawawezi kuwakataa watoto wa watoto wao.

Suala linaonekana kuwa mzigo hata kama mtoto atapewa mahitaji mengine kama kulishwa na kuvishwa kwa gharama za nje ya wazazi wa binti lakini suala la kuwaangalia watoto ni zito na linachosha maana linaonekana kuwasumbua wazee tu ambao jukumu lao la kuangalia watoto lilishapita tangu siku nyingi nyuma.
 
wazaz nao wanpenda sana wajukuu,hasa wazaz wa kike, binti umri ukienda hajaolewa wala hajazaa anaonekana tasa
 
Tafsiri yake ni kwamba wanarubuniwa na wanaume kuwa watawaoa,baadae wanaume wakiona wana mimba huwa wanawakana,na tatizo wanaume wa siku hizi wanaendekeza starehe hivyo wanakwepa majukumu ya kuoa na Kuwa na familia na hapo ndo tatizo linapoanzia

Siku hizi wanaume ni wachache sana,ila wavulana ndo wengi balaa,ukiwaangalia kwa haraka unaweza fikiri wote ni wanaume LA hasha,wengine ni wavulana.
 
Nini kifanyike kuondokana na adha hii?
 
hainigii akilini.
Unataka kuniambia miaka ya nyuma walikuwa hawatongozwi na kurubuniwa?
Sema tu watoto wa kike hasa wa siku hizi hawana akili za kufikiria maisha wao wanawaza kuvuliwa tu.

Hivi kama ww umefundwa utakubali vp upewe mimba ilihali upo kwa wazaz wako hujatolewa mahali?!!

Tatizo wakiambiwa ww ni mzur wanaanza kuchekacheka na kuanza kuwashwa tayar.

Hata upande wa wazaz nao wanachangia sana,,
 
Mmomonyoko wa maadili.
Kitoto cha kike kinapenda starehe, ukikionya ndio kinabinua midomo.

Mkuu na most of them huwa wanalalamikiwa na wazazi wao au unakuta walishaonywa hapo kabla! wazazi wanaona ni bora kusitiri aibu kwa kukaa na wajukuu na binti maana hakuna namna nyingine ya kufanya. Hakuna mzazi anayependa mwanae azalie nyumbani hiku akiwa hana muelekeo mzuri.
 
naweza kusema wazaz huchangia kwa % flan japo sio sana. Ila ukweli ni mitoto yenyew haiambiliki yewnyew huwaza kuchanisha tu
 
hainigii akilini.
Unataka kuniambia miaka ya nyuma walikuwa hawatongozwi na kurubuniwa?
Sema tu watoto wa kike hasa wa siku hizi hawana akili za kufikiria maisha wao wanawaza kuvuliwa tu.

Hivi kama ww umefundwa utakubali vp upewe mimba ilihali upo kwa wazaz wako hujatolewa mahali?!!

Tatizo wakiambiwa ww ni mzur wanaanza kuchekacheka na kuanza kuwashwa tayar.

Hata upande wa wazaz nao wanachangia sana,,

Halafu piga picha jinsi mtoto atakavyolelewa. Inawezekana kweli mama akawa hanatulia halafu mtoto anayepitia kimalezi mikononi mwake akatulia? au anawezaje kumkanya mwanaye mambo ambayo yeye mwenyewe aliyafanya na japokuwa alionywa ila hakuacha?
 
naweza kusema wazaz huchangia kwa % flan japo sio sana. Ila ukweli ni mitoto yenyew haiambiliki yewnyew huwaza kuchanisha tu

Wazazi wanakosea kwenye upande wa malezi tu, ni mabinti wachache wanaopitia malezi mazuri ya kimaadili halafu wakengeuke baadaye.
 
kwa upande wangu wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa sanaaaaa. nina uthibitisho kwa mabinti kadhaa ambao nawajua, mmoja wapo akiwa sister wangu. sister wangu wakati yupo chuo kuna watu wenye heshima zao walikuwa walikuwa wanakuja nyumbani kutaka kumuoa lakini kikwazo kikubwa kilikuwa kinatoka kwa wazazi!! nakumbuka wazazi walikuwa wanasema "mtoto wetu bado mdogo, anasoma na visingizio vingine kama hivyo ambavyo walikuwa hawaviweki wazi (mfano jamaa anaetaka kumuoa akiwa hana pesa za maana) wazazi hao hao waliokuwa wanakataa asiolewe walikuwa hawajui binti yao ambao wao wanamuona mdogo kuingia kwenye ndoa, kumbe binti yao alianza mambo ya ngono tokea zamani. wamekuja kustuka mwaka wa tatu chuoni sister ana mimba!! akazalia nyumbani na jamaa aliyemtia mimba aliikataa mimba. mtoto mpaka leo hii yupo home analelewa na wazee.

na mi huwa nawachana live wazee kuwa wao ndio waliosababisha binti yao kuzalia nyumbani kwa kumuona ni mdogo kuwa hawezi kuingia kwenye ndoa. kumbuka wazee wetu walikuwa anaolewa bado wadogo sana (mfano bi mkubwa wangu anasimulia yeye aliolewa na miaka 18) sasa hapa ndio nashagaa kwanini walishindwa kumuozesha binti yao kwa kipindi kile ambapo alikuwa na miaka 22!!

wazazi inabidi muwe makini sana kama mtu anakuja kutaka kumuoa mwanao kwa nini ukatae na unaweaza kuta mtu ana vigezo vyote vya kuoa lakini wazazi wanasigizia binti mdogo na mambo mengine!! matokeo yake aibu mtoto anazalia nyumbani. AIBU SANA!!!
 
mizazi ya siku hizi hovyo tuu.....as a parent u should be ashamed motto wako kuzaa nje ya ndoa. speaks poorly of u as a parent. mwanamke mwenye akili na aliye lelewa vizuri kamwe hawezi kuzaa nje ya ndoa.
 
kwa upande wangu wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa sanaaaaa. nina uthibitisho kwa mabinti kadhaa ambao nawajua, mmoja wapo akiwa sister wangu. sister wangu wakati yupo chuo kuna watu wenye heshima zao walikuwa walikuwa wanakuja nyumbani kutaka kumuoa lakini kikwazo kikubwa kilikuwa kinatoka kwa wazazi!! nakumbuka wazazi walikuwa wanasema "mtoto wetu bado mdogo, anasoma na visingizio vingine kama hivyo ambavyo walikuwa hawaviweki wazi (mfano jamaa anaetaka kumuoa akiwa hana pesa za maana) wazazi hao hao waliokuwa wanakataa asiolewe walikuwa hawajui binti yao ambao wao wanamuona mdogo kuingia kwenye ndoa, kumbe binti yao alianza mambo ya ngono tokea zamani. wamekuja kustuka mwaka wa tatu chuoni sister ana mimba!! akazalia nyumbani na jamaa aliyemtia mimba aliikataa mimba. mtoto mpaka leo hii yupo home analelewa na wazee.

na mi huwa nawachana live wazee kuwa wao ndio waliosababisha binti yao kuzalia nyumbani kwa kumuona ni mdogo kuwa hawezi kuingia kwenye ndoa. kumbuka wazee wetu walikuwa anaolewa bado wadogo sana (mfano bi mkubwa wangu anasimulia yeye aliolewa na miaka 18) sasa hapa ndio nashagaa kwanini walishindwa kumuozesha binti yao kwa kipindi kile ambapo alikuwa na miaka 22!!

wazazi inabidi muwe makini sana kama mtu anakuja kutaka kumuoa mwanao kwa nini ukatae na unaweaza kuta mtu ana vigezo vyote vya kuoa lakini wazazi wanasigizia binti mdogo na mambo mengine!! matokeo yake aibu mtoto anazalia nyumbani. AIBU SANA!!!

mwana umeogea bonge la point. wazazi ndio wakubebeshwa lawama
 
Hakuna ajira wala elimu, wanaona watumie uhuru wao wa kikatiba wa kujielezea kwamba wanapenda watoto bila complications za harusi, ndoa etc.

Na sera za Beijing zinawapa nguvu, wakiwezeshwa wanaweza.
 
Na kwa nini mimba zikataliwe?je kuna mtoto asiye na baba?msimamo wangu unabaki pale pale,wanaume ndo sbb,hats kama mtasema watoto wa kike wanapenda kuvuliwa,hata watoto wa Kiume nao wanapenda kuwavua wasichana hovyo,huku wakiwa bado watoto wa mama!narudi pale pale wanaume ni wachache wengi ni wavulana!!!
 
Hilo la wazazi kumchagulia mchumba binti halijaanza Leo toka enzi zileee,hakuna mzazi anayemtakia mtoto wake mabaya tatizo watoto ndo tumekuwa wajuaji kutaka kuwapanda vichwani wazazi!!sasa acha tule matunda ya ukaidi wetu!
 
mwana umeogea bonge la point. wazazi ndio wakubebeshwa lawama

ndio hivyo mkuu. japo kwa upande mwingine mabinti nao tunawalaume kwa kushindwa kukunja miguu yao. lakini bado lawama kubwa zinawaangukia wazazi/walezi.
 
Back
Top Bottom