Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,508
Hapa tunapokaa nyumba tunayopeana nayo mgongo wana mashindano ya kuzalia nyumbani
Mdogo wao wa mwisho ana umri wa miaka 13 naye juzi juizi kajifungua kichanga
Duh!!!!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa tunapokaa nyumba tunayopeana nayo mgongo wana mashindano ya kuzalia nyumbani
Mdogo wao wa mwisho ana umri wa miaka 13 naye juzi juizi kajifungua kichanga
Ishu kama hizi ziko personally sana
Ishu kama hizi ziko personally sana
Hakuna cha kuwa personal wala nini. Issue ni kuwa maadili hakuna, wazazi wanaishi uzunguni ambapo wengi wanapaona kwenye series tu, vijana wanajifanya kujua kila kitu. Wazazi hawawafundishi watoto ipasavyo, watoto wanafumdishwa lakini hawasikii...! Kuzalia home ni aibu kwa wazazi..hakuna mzazi anayefurahishwa kuona binti analeta ujauzito ndani kabla hajaolewa. Ni aibu tupu..!
Kwahiyo watu wasiseme?
Swali la kiwak hili
Umesema ni swali la......?
Hili halikuwepo miaka ya 90s kurudi nyuma, sisemi kwamba haikuwa ikitokea, la hasha! bali hata kama ilikuwa inatokea basi ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na ilivyo sasa.
Katika maeneo ninayokuwa hasa kwa watu mbalimbali ninawafahamu, jambo hili linaonekana kukuwa zaidi ya mara dufu na inavyoonekana hali ikazidi huko mbele ya safari.
Mabinti wengi wanaozaa wakiwa bado hata hawajaposwa wamekuwa wakiwaacha watoto wao wakilelewa na babu&bibi huku wakiendelea masuala yao ikiwemo kuendeleza uhusiano na wanaume ambao unapelekea kuongeza idadi ya watoto kwa wazazi bila kujua ugumu wa kulea watoto.
Wanaume wamekuwa wakiwazalisha mabinti bila kuwaoa wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kulea badala yake mwanamke ndio anaachiwa jukumu la uangalizi wa mtoto ambaye naye anakabidhi majukumu kwa wazazi wake! kimsingi wazazi hawawezi kuwakataa watoto wa watoto wao.
Suala linaonekana kuwa mzigo hata kama mtoto atapewa mahitaji mengine kama kulishwa na kuvishwa kwa gharama za nje ya wazazi wa binti lakini suala la kuwaangalia watoto ni zito na linachosha maana linaonekana kuwasumbua wazee tu ambao jukumu lao la kuangalia watoto lilishapita tangu siku nyingi nyuma.
Nishajiulizaga sana hili tatizo linatokana na nini? Tena kwa baadhi ya mikoa hili tatizo ni kubwa sana...
Na kwenye uchunguzi wangu niligundua kuwa hili tatizo ni sugu kwa mikoa hasa yenye idadi kubwa ya waislamu.
Nenda kigoma sehemu za ujiji, mwanga na mwandinga unakuta kila binti kazaa mtoto na hajaolewa.' Wengine wanaishi kwao, wengine wamepanga.
Nenda mtwara, kisarawe, lindi, bagamoyo, chalinze na kule temeke hili tatizo ni kubwa mno.
Hujaelewa au unataka nirudie
Hakuna mzazi asiyependa wajukuu ila hilo la binti kuzalishwa kwao unadhani kuna mzazi anayelitaka kuliona?
Hakuna cha kuwa personal wala nini. Issue ni kuwa maadili hakuna, wazazi wanaishi uzunguni ambapo wengi wanapaona kwenye series tu, vijana wanajifanya kujua kila kitu. Wazazi hawawafundishi watoto ipasavyo, watoto wanafumdishwa lakini hawasikii...! Kuzalia home ni aibu kwa wazazi..hakuna mzazi anayefurahishwa kuona binti analeta ujauzito ndani kabla hajaolewa. Ni aibu tupu..!
na warogwe tu hasa wanaowakataa wanaowapa mimba"!!
......malezi yanachangia kwa kiasi kikubwa.
Mzazi ukimfundisha mtoto angali akiwa mdogo maadili mazuri awe wa kike au wa kiume hawawezi kubebeshana mimba ovyo na kuachia mzazi wake alee mtoto.
Unajua mnapoonge hebu jaribuni kurudi nyuma na kuuangalia mfumo wa maisha ulivyo....
Maadili yameshuka na hatuna Miiko...so lazima tujue chanzo cha mimba nini?
Chanzo cha mimba ni watu kushiriki ngono sasa ni nani ambaye akushiriki ngono wakat bado anaishi kwa baba...jibu ni hakuna..
Haya ndio maisha tuliyo chagua maana tunabaliki mahusiano ya kimapenz ya wadogo zetu bila kujali tunasubir kinuke ndio tuanze kulaumu.
Mfano halisi ninao.
Kuna msichana jiran hapa alikuwa na huusiano na kijana mmoja lakini ilikuwa inajulikana na wazaz wake walikuwa wanajua sasa juz kapata mimba ndio wanaanza kumlaumu.
Nakumbuka mie nmeanza kuwa na girlfriend tokea primary bt nmeaanza kushiriki sex form 2 na wote tulikuwa na mahusiano darasani na usipokuwa na mpenz utaonekana sio mjanja na kuna some kids walikuwa victim wa mimba ila maisha yaliendelea tu
Nenda kwa wamwera ndio utajua kua mtoto kupata mtoto kwao ni fahari. Nilifanya kazi huko, nilikua kituko maana nilikua na miaka 25 sina mtoto.
Wanakuuliza "eti kusubiri kumpata bwana(mume) wa kuoa?, hii mabwana wenyewe dada wako wapi?
Huko mama anaingia leba Nov, mwezi Dec anamsindikiza mwanae leba.
Wakati uchagani hata uwe na 40yrs ni marufuku na aibu kuzaa bila ndoa.
Kwahiyo inategemea na maeneo.