nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,379
Ni vibaya...lakini kwa kuwa ni ngumu kuzuia ...you have to do it responsibly...Hata kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni vibaya pia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni vibaya...lakini kwa kuwa ni ngumu kuzuia ...you have to do it responsibly...Hata kufanya mapenzi kabla ya ndoa ni vibaya pia
Kawaida tu sema inaonekana jambo la ajabu kwasababu ya mazoea na tamaduni lakin ni jambo la kawaida sana. Mbona wanaume nao wapo wanaonazalisha wanawake kisha wanaume hao wanaachiwa watoto wadogo ambao wanakuja kuwa mzigo kwa wazee vilevile ila hawasemwi?
Usidhani kila mwanamke yupo kwenye hatari ya hilo janga.
Sio wote humu ni mabinti wadogo. Nilishavuka huko kitambo, wewe upo upande wa vijana wadogo wakati mimi nipo upande wa wazazi/ walezi.
Siwezi kunyamaza kwa mtoto wangu wa kiume eti kwa vile yeye hashuki thamani au haimuathiri.
Na lazima ujue kua hatuwezi kufanana mtazamo, kwangu hata mtoto wa kiume kuwa baba kwenye umri mdogo itanigusa.
Usilazimishe niwe na mtazamo wako wala kupinga mawazo yangu haibadilishi kitu.
Vyote vibaya...
Kizuri ni kuzaa mwenye ndoa...
Na jina lako linaonyesha u r among the top ten fools in the worldAvatar yako tu inaonesha kuwa wewe ni wale wale.
Rudia tena . Umesema??Na jina lako linaonyesha u r among the top ten fools in the world
Singo mazazHili halikuwepo miaka ya 90s kurudi nyuma, sisemi kwamba haikuwa ikitokea, la hasha! bali hata kama ilikuwa inatokea basi ni kwa asilimia ndogo sana tofauti na ilivyo sasa.
Katika maeneo ninayokuwa hasa kwa watu mbalimbali ninawafahamu, jambo hili linaonekana kukuwa zaidi ya mara dufu na inavyoonekana hali ikazidi huko mbele ya safari.
Mabinti wengi wanaozaa wakiwa bado hata hawajaposwa wamekuwa wakiwaacha watoto wao wakilelewa na babu&bibi huku wakiendelea masuala yao ikiwemo kuendeleza uhusiano na wanaume ambao unapelekea kuongeza idadi ya watoto kwa wazazi bila kujua ugumu wa kulea watoto.
Wanaume wamekuwa wakiwazalisha mabinti bila kuwaoa wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kulea badala yake mwanamke ndio anaachiwa jukumu la uangalizi wa mtoto ambaye naye anakabidhi majukumu kwa wazazi wake! kimsingi wazazi hawawezi kuwakataa watoto wa watoto wao.
Suala linaonekana kuwa mzigo hata kama mtoto atapewa mahitaji mengine kama kulishwa na kuvishwa kwa gharama za nje ya wazazi wa binti lakini suala la kuwaangalia watoto ni zito na linachosha maana linaonekana kuwasumbua wazee tu ambao jukumu lao la kuangalia watoto lilishapita tangu siku nyingi nyuma.