KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Hili tatizo halitakwisha mpaka pale wanawake watakapo badilika.......wanawake wengi wanaishi katika ulimwengu wa kufikirika ambao upo vichwani mwao pekee....wana ndoto za kuolewa na mtu ambaye hayupo katika ulimwengu halisi...wengi wao wana machaguo mengi mno wanapotafuta wenza huku fedha na mali vikiwa ndio dira yao kuu.....lakini bahati mbaya hawajiandai kuishi maisha ya ndoa....wanayalinganisha maisha ya ndoa na yale wanayoyaona kwenye tamthilia....kwa kuthaminisha pendo na kiasi cha fedha na mali ndio unakuta wengi wanatumika kama chombo cha starehe na mwisho wake huwa ni mimba na hatimaye maradhi.....hapo watoto wa mitaani hawawezi kuisha kwa kuwa wazazi wa aina huwa wanakuwa hawapo tayari kulea wala kupambana na majukumu kama mzazi........Vile vile kina dada waache kujirahisi kwa kuwa bidhaa rahisi huwa ina watumiaji wengi lakini haithaminiwi....wakati umefika umefika kwa wanawake kutambua thamani yao na kujua kwanini muumba aliona si vyema adamu abaki pekee yake bila ya msaidizi.....waondoe maisha ya kufikirika vichwani mwao na waishi katika ulimwengu halisi.....wapunguze machaguo yasiyo ya msingi mume bora ni yule anayeweza kukabiliana na majukumu yake na kuihakikishia mahitaji yote ya msingi kwenye kaya yake na si kwa uzuri wa sura au mwili uliojengeka kwa mazoezi au mrefu kuliko wote...........wasilinganishe penzi kwa kiwango cha fedha kwa kuwa true love is priceless..........