Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
naishukuru jf na nakushukuru na wewe pia,kwajinsi ulivyolichambua hili jambo hakika ni dhahiri,ni kweli nina ambition ya mafanikio kupita kiwango cha kawaida,ila tangu nazaliwa sijawahi kufikiria kupata mali kwa njia isiyo halali,nimeshawahi kujitoa kwenye mradi tulioanzisha na wenzangu ambao ulikuwa wa hela nyingi sababu kubwa ikiwa niliona kuna njia za udanganyifu wenzangu wanataka kuzitumia,sijawahi kuiba hata cent wala kufikiria kufanya hivyo,nina uamnifu wa hali ya juu,lakini naheshimu hapo uliposema sijawahi kutangaza,hakuna anayejua ambition zangu,ni mimi mwenyewe tu
wewe ni mtu mwaminifu. nauona uaminifu wako katika maneno yako. ila kufafanua kauli yangu labda niseme hivi. sijakuita mwizi. ila nimesema kwenye ngazi yako ya hurka ya ubinadamu ambayo imejificha, ambayo inaitwa sub-conscious, kunaweza kuwapo mambo nje ya utashi wako katika hali halisi. Na wewe hautakuwa wa kwanza kuwa na mgongano kati ya kilichopo kwenye hali halisi, nipaite concious level, na hurka iliyojificha (sub-conscious level). Binadamu wengi wanakuwa na tatizo hilo la vita kati ya conscious na sub-conscious.
Na pale vita hiyo inapokuwa kali sana kati ya hali halisi kupingana na hurka iliyojificha, binadamu wengine hupatwa na ugonjwa wa akili unaoitwa Neurosis kutokana na vita hiyo ya ndani kwa ndani. Unaweza kukuta mtu analewa kupindukia. Mwili upo katika vita hapo; inawezekana kabisa pombe inatumika kufunika hitaji katika hurka iliyojificha ambalo limekatazwa ha hali halisi. Au mwanamke, au hata mwanamume anaweza kuwa kitandani kavua nguo zote lakini mashine ikawa imegoma kabisaa.... Hapo uwezekano mkubwa ni kwamba kuna vita kati ya sub-conscious na hali halisi. Hizo ngazi mbili hazijakubaliana kuhusu kitu.
Now back to the topic: kwa maelezo uliyoweka awali, na haya ya sasa, napata picha kwamba conscious level yako, yaani hali halisi inayo upper hand katika maamuzi yako. Lugha ya kawaida wanasema umeweza kujitawala. Hilo ni jema. Lakini ndoto zako zinaonesha kuna kitu unataka. Ni vizuri kwamba umeweza kujitawala, ingawa hilo halina maana kwamba unaweza kujitawala kila wakati, ndiyo maana kunakuja hitaji la kuwa na kitu kinachokuwezesha kuwa na kipato ili kishawishi hiki kibaya kilichopo kwenye sub-conscious kisifike mahale kikapata upper hand. Ni wakati mzuri pia kuwaza habari za msaada kutoka kwa Mungu, kwani mafundisho mengi yaliyopo katika dini nyingi yanaelekeza kuzishinda hurka zetu za kibinadamu za ulafi. Katika Ukristo wanasisitiza sana neno 'kiasi'; kwamba uwe mtu wa kiasi, na uendelee hivyo. Maelezo yako ya pili yameonesha kuwa wewe umejitahidi sana kuwa mtu wa kiasi. Naomba Mungu akutie nguvu ili uendelee kuwa hivyo uishinde hii hurka ya ulafi wa utajiri kama wanayoonesha wabunge wetu kule Dodoma