Shalom! Ingawa mimi sio mtumishi lakini tambua Mungu ameweka kusudi katika kila mwanadamu, hivyo nawe kwanza muombe Mungu akuonyeshe kusudi lake na usimame ktk hilo. Pili ktk kila jambo kuna muda na mahali maalumu Mhubiri 3:1-11. Tatu tambua kanisa ni mwili wa Kristo una nguzo zake kuu kama huduma mbalimbali, lakini pia karama tofauti ili kuujenga mwili wa Kristo kwa kufaidiana.
Kutokana na hayo hapo juu ninafikiri uliitwa kutumika kweli, lakini ktk kanisa la mwanzo, tatizo hukuwa na subira wala kumuuliza Mungu ukaenda kusoma? Na umeanza kutumika hapo. Lakini kwavile si kusudi la Mungu wewe kuwa hapo ndio unakutana na maono hayo unaitwa kule ulikokusudiwa na hivyo kujikuta huna amani na ufanyacho hapo. Kwamba unapofika kanisa la mwanzo unakuta mtu anahudumu hiyo sio kikwazo ni kuwa wakati wako utafika unaitwa ukakae miguuni kwa Mungu, ukakae chini ya mtu uikulie huduma yako ukiwa tayari utaitwa kutumika. Nakupa mfano wa Biblia watu ambao waliitwa, walipakwa mafuta na kuzijua kusudi zao lakini walikaa miguuni mwa Mungu chini ya watumishi wakijifunza ndipo wakaanza kutumika: mfalme Daudi chini ya Sauli, nabii Samuel chini ya Elli, Paulo na kanisa la Antiokia, Timotheo kwa Paulo. Nakushauri kaa chini muulize Mungu kusudi lako kusoma Theology sio kuijua karama yako. Kama mtumishi omba ujue kuisikia na kuijua sauti ya Mungu. Zaburi 27, uwe na ------. Blessings