Habari wanajamvi,mara baada ya salaam mimi ndugu yenu ni buheri wa afya,
Dhumuni la uzi huu ndugu zangu ni kuwaletea hiki nilichokiota usiku wa kuamkia leo, nataraji kupewa majibu mbalimbali miongoni mwa wachangiaji na niko tayari kuyapokea.
Usiku wa kuamkia leo nimeaota mkewangu akiwa amelala kitanda kimoja na mwanaume ambea hapo kabla nilishawahikuhisi wanamuhusiano ya kimapenzi lakini alipinga na kunipa vigezo ambavyo kwa upande mwingine nilijiridhisha, tangia hapo sikuona closeness yake na huyo mjamaa tena..
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi;
Kwakuwa naishi mbali na mkewangu kutokana na kutenganishwa na kazi niliamua kwenda kumtembelea na kusalimia familia hii nikutokana na kupata kazi mkoa wa jirani ambao sio mbali(km160 aprx), nilipofika nikashtushwa kumkuta mkewangu akiwa namgeni ambae amejipumzisha katika kitanda anacholala,mbaya zaidi ni yule ambaye nilikuwa na mashaka na uhusioano wao.
Kiukweli nilipata uchungu kwenye hiyo ndoto mpaka kufika hatua ya kulia ikiwa pia ndio mara ya kwanza kulia katika mapenzi tangia nizaliwe ikizingatiwa nilshaumizwa na binti ambaye naamin nilimpenda sana kushinda wote kwenye uhusiano lakini sikuwahi kutokwa chozi.
Japo mke alinicomfort nakujaribu kutaka kuamini lakini hali ilizidi kuwa mbaya pale mwanangu wa kike 2 years old,akinisimulia yakuwa mama alikuwa ana kiss na dady kitu kilicho niumiza twice, and sikupata conclusion katika hiyo ndoto.
Cha ajabu sasa mpaka kuomba msaada huu wa kiimani na kimaona na kiutaalam mbalimbali nikwamba,asubuhi ni meamka na hasira kama kweli kile kitu kimetokea na pia nimeshindwa kumpigia mkewangu sim wala yeye hajanipigia sim mpaka sasa wakati si kawaida...
Kunanini hapa?mimi nahofu, mara nyingi nimekua nikiota mambo au matukio na yanakuwa kweli