Nini tatizo nchini kwetu mpaka waajira wapya wanawaza njia za upigaji hela ya serikali

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Aibu sana yaani kama vile takukuru haina makali maana hata waajiriwa wapya hawaogopi kabisa kufanya udanganyifu.michezo hii tunajua ipo kwa wakubwa huko ma senior waliozoea kazi ila cha kusikitisha mpaka mazungumzo ya vijana katika mataasisi ni namna ya kuwa katili ili kula hela ya umma.watoto wa nyoka wanaamua na wenyewe kuwa nyoka wengine kwa sura wapoleee ila wewe ngoja itokee mwanya wa kupiga hela hio mikakati hutaamini..

Ni kwamba mishahara haitoshi kiasi watu wafikirie vimeo au ni vijana kupenda mafanikio kwa pupa.ni mwendo wa kurithishana na kufudishana mbinu za kunywa pesa.

Nachokiona ni kwamba vigogo wangekuwa wanakula kwa urefu ila wasijionyeshe maana hata wa chini wanaona bora na wenyewe wapige tu.
 
Kula urefu wa kamba yako acha kelele
 
Watumishi wana stress Sana wanataka mambo makubwa Kwa haraka.

Huwa nikiwatazama watumishi wa Tz ni kama walikuwa na mategemeo makubwa kuliko uhalisia waliokutana nao kazini.

Wanatamani maisha makubwa wakati vipato vyao vidogo mwisho niupigaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…