Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

Kwenye kukubali na kukataa Ni
Ndiyo boss
Au siyo

Usipoweka Y unakuwa unakosea

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye kukubali na kukataa ni
Ndio na Sio. Mfano:
Swali: Ndio huyu mtu mwenyewe?
Hapana sio huyo
Ndio huyo

Ndiyo na siyo hutumika kwa vitu. Mfano
Swali: Hii ndiyo shati uliyokuwa unaitafuta?
Ndiyo hiyo
Siyo hiyo

Ijapokuwa utaona kuna mfanano kwenye matamshi ila utofauti upo kwenye maandishi.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Samahani kuuliza si ujinga. Kwenye hayo maneno hiyo Y imetokea wapi? Nijuavyo ni:
Ndio
Sio

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
Katika lugha kwa mujibu wa wanasarufi wakongwe Kuna kitu kinaitwa udondoshaji(hapa ndio utakutana na kioo kutoka neno kilolo,ndio /ndiyo)msingi unatokana na utashi wa mjuvi wa lugha,anataka kutumia mda mchache kuzungumza
 
Naomba kufahamu jinsi ya kutumia maneno yafuatayo

- pesa
- hela

Mf. Alimpa pesa au alimpa hela

- ndivo ilivo au ndivyo ilivyo





Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa ni neno ambalo limetoholewa kutoka kwenye neno la Kihindi "Paisa" ambalo likiwa na maana ya Sarafu.

Hela ni neno ambalo limetoholewa kutoka kwenye lugha ya kijerumani "Heller" likiwa na maana ya kilichokuwa kitengo cha pesa za Kijerumani kwa Afrika Mashariki (sarafu) mnamo mwaka 1904.hadi 1918. Waingereza baada ya kuchukua utawala wa koloni walibadilisha sarafu kuwa shilingi na senti lakini jina la "hela" lilibaki kwa ajili ya pesa kwa jumla.
200px-1_Heller_1913_A.jpeg

200px-1_Heller_ya_1913_B.jpeg

Maneno yote mawili humaanisha Pesa

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Naonge kishwahili na ni mtanzania na nimekulia Tanzania lakini Kila nikiandika sms nakose vitu Kama iv

Mf. Ivo, hivyo au ivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si vyema kuandika hivyo maana kuna maneno ukiondoa herufi moja unaongelea kitu kingine. Na kumbuka kuandika vimikato hivyo kwa mtu unayemheshimu kama mzazi ni dharau
 
Saint Anne, Hebu angalia kwenye mifano hii
1. Hii ndiyo nyumba yangu.
2. Weka alama ya ndio kwa mgombea wetu

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Hebu angalia kwenye mifano hii
1. Hii ndiyo nyumba yangu.
2. Weka alama ya ndio kwa mgombea wetu

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
Hapo umegeuzia mkuu
"Ndio" ilitakiwa iwe kwenye sentensi ya kwanza
Na" ndiyo" kwenye sentensi ya pili

"Ndio "hutumika kuelezea kitu
Yaani hapo ilitakiwa useme"hiyo ndio nyumba yangu"

Sentensi ya pili alama ya" ndiyo "yaani kukubali
Ungeandika "weka alama ya ndiyo kwa mgombea wetu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo mimi; hela, pesa na fedha ni maneno tofauti yenye maana moja (synonyms).

• Pesa ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kihindi (Paisa).

• Hela ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kijerumani (Heller).

• Fedha ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kilatini.

Yote yana maana moja.
Na inashangaza kidogo kuona lugha inakopa neno kutoka lugha mbalimbali lakini lenye maana ile ile. Pengine swali la kujiuliza ni kama matumizi ya haya maneno yana hadhi sawa katika jamii
 
Kwenye kukubali na kukataa ni
Ndio na Sio. Mfano:
Swali: Ndio huyu mtu mwenyewe?
Hapana sio huyo
Ndio huyo

Ndiyo na siyo hutumika kwa vitu. Mfano
Swali: Hii ndiyo shati uliyokuwa unaitafuta?
Ndiyo hiyo
Siyo hiyo

Ijapokuwa utaona kuna mfanano kwenye matamshi ila utofauti upo kwenye maandishi.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
Mkuu wewe ni Mkenya?

Huo mfano wako wa shati haujazingatia upatanisho wa ngeli. Inapaswa kuwa:

Hili ndilo shati ulilokuwa unalitafuta?
Ndiyo hilo
Siyo hilo
 
Back
Top Bottom