Si kweli ajabu lugha nyingi huwa na maneno tofauti. Tafuta "synonyms for money" utapata:
"Synonyms for money,
bread, [slang], ,
bucks, ,
cabbage, [slang], ,
cash, ,
change, ,
chips, ,
coin, ,
currency, ,
dough, ,
gold, ,
green, ,
jack, [slang], ,
kale, [slang], ,
legal tender, ,
lolly, [British], ,
long green, [slang], ,
loot, ,
lucre, ,
moola, (or
moolah), [slang], ,
needful, ,
pelf, ,
scratch, [slang], ,
shekels,
tender, ,
wampum"
Mababu wa Afrika ya Mashariki hawakuwa na pesa-hela kwa muda mrefu. Ilitumiwa kwenye pwani tu katika miji ya Waswahili, tena na wafanyabiashara si na watu wote. Imetiririka ndani ya jamii wakati wa koloni. Kwa hiyo ilikuwa jambo geni.
Hapa watu waliona kitu hiki kwa maumbo tofauti:
kwanza
"paisa" ambayo ni sehemu ndogo (=visenti) za "
rupia". Rupia ya Uhindi (koloni ya Uingereza) ilikuwa pesa kuu katika karne ya 19 kabla ya ukoloni, ilikuwa pesa rasmi pale Zanzibar . Haikuwa pesa ya pekee, kulikuwa pia ya
"dollar" ya Maria Theresia. Ila tu wenyeji wengi hawakuwa na nyingi, kwao si rahisi kushika rupia, lakini waliweza kutumia "
pesa" zake.
Wajerumani walipoanzisha ukoloni waliendelea kutumia rupia kama jina lakini kwa visenti vyao walileta jina "
heller". Kumbe wenyeji walijifunza pia "
hela". Sijafanya utafiti lakini nahisi pale Kenya labda neno hilo la "hela" halijulikani sana? Maana Waingereza walipoamua kuunda pesa yao kwa koloni walileta shilingi na senti.
Sasa
fedha. Fedha ni metali adimu (
silver). Thamani ya
sarafu (vipande vilivyotumiwa) ilitegemea kiwango cha fedha ndani yake. Rupia ilikuwa na gramu 11.66; dollar ya Maria Theresia ilikuwa na gramu 23.386. Kwa hiyo dollar 1 ilikuwa sawa na rupia 2. Zilitumiwa kandokando kwenye miji ya Waswahili. Hapa inaonekana jina "fedha" lilishika zaidi kuliko majina ya rupia au dolar.
Jina fedha btw si Kilatini, ni Kiarabu
فضة