Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

Mkuu wewe ni Mkenya?

Huo mfano wako wa shati haujazingatia upatanisho wa ngeli. Inapaswa kuwa:

Hili ndilo shati ulilokuwa unalitafuta?
Ndiyo hilo
Siyo hilo
Mimi ni mtanzania, mwenyeji wa pwani. Mfano niloutoa mimi uko sawa kabisa kama huamini peleka mfano wangu kwenye wingi uone na peleka mfano wako kwenye wingi uone, shati linaingia kwenye ngeli ya Ll-YA

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Na inashangaza kidogo kuona lugha inakopa neno kutoka lugha mbalimbali lakini lenye maana ile ile. Pengine swali la kujiuliza ni kama matumizi ya haya maneno yana hadhi sawa katika jamii
Si kweli ajabu lugha nyingi huwa na maneno tofauti. Tafuta "synonyms for money" utapata: "Synonyms for money, bread, [slang], , bucks, , cabbage, [slang], , cash, , change, , chips, , coin, , currency, , dough, , gold, , green, , jack, [slang], , kale, [slang], , legal tender, , lolly, [British], , long green, [slang], , loot, , lucre, , moola, (or moolah), [slang], , needful, , pelf, , scratch, [slang], , shekels, tender, , wampum"

Mababu wa Afrika ya Mashariki hawakuwa na pesa-hela kwa muda mrefu. Ilitumiwa kwenye pwani tu katika miji ya Waswahili, tena na wafanyabiashara si na watu wote. Imetiririka ndani ya jamii wakati wa koloni. Kwa hiyo ilikuwa jambo geni.

Hapa watu waliona kitu hiki kwa maumbo tofauti:
kwanza "paisa" ambayo ni sehemu ndogo (=visenti) za "rupia". Rupia ya Uhindi (koloni ya Uingereza) ilikuwa pesa kuu katika karne ya 19 kabla ya ukoloni, ilikuwa pesa rasmi pale Zanzibar . Haikuwa pesa ya pekee, kulikuwa pia ya "dollar" ya Maria Theresia. Ila tu wenyeji wengi hawakuwa na nyingi, kwao si rahisi kushika rupia, lakini waliweza kutumia "pesa" zake.

Wajerumani walipoanzisha ukoloni waliendelea kutumia rupia kama jina lakini kwa visenti vyao walileta jina "heller". Kumbe wenyeji walijifunza pia "hela". Sijafanya utafiti lakini nahisi pale Kenya labda neno hilo la "hela" halijulikani sana? Maana Waingereza walipoamua kuunda pesa yao kwa koloni walileta shilingi na senti.

Sasa fedha. Fedha ni metali adimu (silver). Thamani ya sarafu (vipande vilivyotumiwa) ilitegemea kiwango cha fedha ndani yake. Rupia ilikuwa na gramu 11.66; dollar ya Maria Theresia ilikuwa na gramu 23.386. Kwa hiyo dollar 1 ilikuwa sawa na rupia 2. Zilitumiwa kandokando kwenye miji ya Waswahili. Hapa inaonekana jina "fedha" lilishika zaidi kuliko majina ya rupia au dolar.
Jina fedha btw si Kilatini, ni Kiarabu فضة
 
Mifano uliyotoa kuhusu synonyms za money katika Kiingereza haisadifu kwa sababu hapa tunazungumzia matumizi rasmi tu na siyo slang wala lugha za mtaani; na hayo maneno yote sidhani kama yamekopwa.

Hoja kuu ni kwamba kwa nini lugha tajiri kama Kiswahili ikope maneno kutoka lugha mbili za kigeni kuelezea neno lile lile? Mpaka majuzi hapa tulikuwa tunatumia neno kansa kumaanisha ugonjwa wa "cancer". Leo tena tumekopa neno saratani. Nimeambiwa hili ni neno la Kiarabu. Earthquake tulikuwa na neno letu zuri tu "tetemeko la ardhi". Leo nasikia tumeanza kutumia zilzara (Kiarabu?). Kuna sababu gani kwa lugha kubwa na tajiri kama Kiswahili kufanya hivi?

Maelezo yako mengine ya kihistoria kuhusu fedha, pesa na hela nimeyakubali na asante sana.
 
Kila lugha inakopa. Je unajua lugha isiyokopa? Kiingereza na Kiswahili zote ni lugha ambazo zimechukua sehemu kubwa kutoka lugha nyingine (Kiingereza asilimia 50 kutoka Kifaransa / Kilatini, Kiswahili asilimia 25-30 kutoka Kiarabu). Je unaweza kusema maneno mangapi ya Kiswahili bila kutumia maneno yenye asili ya Kiarabu?
ukisema "Hoja kuu ni kwamba kwa nini lugha tajiri kama Kiswahili" maneno manne (rangi nyekundu) ni ya asili ya Kiarabu.
Ukisema zamani ilikuwa "kansa", leo unasikia "saratani" - yote ya kukopa - Kansa ni kiasili Kilatini, ilikopwa na Kiingeerza na kufika Kiswahili; saratani kutoka Kiarabu.
Tatizo ni nini katika kukopa maneno? Kama inafaulu, itakuwa neno la lugha yenyewe.

Kwa hela/ pesa: si ajabu. Kitu chenyewe kilikuwa kigeni kwa wenyeji, hivyo walitumia neno jinsi gani kitu hii kipya lilivyotambulishwa kwao. Hi si lazima, lakini imetokea kote duniani vile.
 
Ndio katika mfano wa tatu ni kitenzi kishirikishi (t)
 
Uko sahihi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masahihisho
Fedha ni Silver na neno la kiarabu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwahiyo Waziri wa Fedha tunaweza pia kumwita waziri wa Hela? Au waziri wa Pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…